Sr. Magdalena
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 803
- 472
[h=3]Mufti: Waislamu acheni kulalama, tafuteni elimu[/h]
Na Faida Muyomba, Geita
MUFTI wa Tanzania, Shekhe Mkuu Issa Shaban bin Simba amewataka waumini wa dini ya kiislamu nchini waache kubweteka na kutoa lawama kwa
serikali badala yake wajikite zaidi kwenye elimu ili kukomboa maisha yao.
Alisema hayo jana wakati akihutubia waumini wa dini hiyo mkoani Geita, ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya ujenzi wa mabweni ya wasichana na bwalo katika Shule ya Sekondari ya Islam.
"Huu ni muda mwafaka kwa waislamu kuanza kujikita na kukazania zaidi suala la elimu, na si kubaki kulialia pekee kuomba kuchaguliwa na kupewa vyeo serikalini, hivyo tuchangamke tusiendelee kubaki nyuma tupige hatua kama wenzetu," alisema Mufti.
Alisema waumini wa dini hiyo nchini wako nyuma kwenye suala la kuwaandaa watoto wao katika elimu, jambo alilosema kuwekeza katika ujenzi wa misikiti pekee hakusaidii, kwani iko hatari ya misikiti hiyo kubaki kama maghala ya kutunzia vyakula.
Alisema mwislamu yoyote anayetaka kuwa mfuasi wa kweli wa dini hiyo lazima ajikite katika elimu kwa sababu ndio mahali pazuri pa kuwekeza na si kwingineko.
Mufti pia alizungumzia namna ya kupata walimu wazuri, akisema huwezi kuwapata bila kulipa mishahara mizuri.
SOURCE: MAJIRA