Mufti: Waislamu acheni KULALAMA, tafuteni ELIMU

Status
Not open for further replies.

Sr. Magdalena

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
803
472
[h=3]Mufti: Waislamu acheni kulalama, tafuteni elimu[/h]
Na Faida Muyomba, Geita

MUFTI wa Tanzania, Shekhe Mkuu Issa Shaban bin Simba amewataka waumini wa dini ya kiislamu nchini waache kubweteka na kutoa lawama kwa
serikali badala yake wajikite zaidi kwenye elimu ili kukomboa maisha yao.

Alisema hayo jana wakati akihutubia waumini wa dini hiyo mkoani Geita, ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya ujenzi wa mabweni ya wasichana na bwalo katika Shule ya Sekondari ya Islam.

"Huu ni muda mwafaka kwa waislamu kuanza kujikita na kukazania zaidi suala la elimu, na si kubaki kulialia pekee kuomba kuchaguliwa na kupewa vyeo serikalini, hivyo tuchangamke tusiendelee kubaki nyuma tupige hatua kama wenzetu," alisema Mufti.

Alisema waumini wa dini hiyo nchini wako nyuma kwenye suala la kuwaandaa watoto wao katika elimu, jambo alilosema kuwekeza katika ujenzi wa misikiti pekee hakusaidii, kwani iko hatari ya misikiti hiyo kubaki kama maghala ya kutunzia vyakula.

Alisema mwislamu yoyote anayetaka kuwa mfuasi wa kweli wa dini hiyo lazima ajikite katika elimu kwa sababu ndio mahali pazuri pa kuwekeza na si kwingineko.

Mufti pia alizungumzia namna ya kupata walimu wazuri, akisema huwezi kuwapata bila kulipa mishahara mizuri.

SOURCE: MAJIRA
 
As you know Tribes were there before all this kind of religions... so we need to be very careful...

As you know religious identity is not as strong as tribal identity, so if we started regime of addressing a religion rights to the country which has a tribal identity more linear than religions.

This will lead to genocide, discrimination, prejudice, cleansing...

We all have equal access to all institutions in TZ why Muslims are causing this kind of discrimination?
We need to get rid of this polarizing politicians who caused immense problems they only mind and think about their elections...
 
Mufti: Waislamu acheni kulalama, tafuteni elimu

Na Faida Muyomba, Geita

MUFTI wa Tanzania, Shekhe Mkuu Issa Shaban bin Simba amewataka waumini wa dini ya kiislamu nchini waache kubweteka na kutoa lawama kwa
serikali badala yake wajikite zaidi kwenye elimu ili kukomboa maisha yao.

Alisema hayo jana wakati akihutubia waumini wa dini hiyo mkoani Geita, ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya ujenzi wa mabweni ya wasichana na bwalo katika Shule ya Sekondari ya Islam.

"Huu ni muda mwafaka kwa waislamu kuanza kujikita na kukazania zaidi suala la elimu, na si kubaki kulialia pekee kuomba kuchaguliwa na kupewa vyeo serikalini, hivyo tuchangamke tusiendelee kubaki nyuma tupige hatua kama wenzetu," alisema Mufti.

Alisema waumini wa dini hiyo nchini wako nyuma kwenye suala la kuwaandaa watoto wao katika elimu, jambo alilosema kuwekeza katika ujenzi wa misikiti pekee hakusaidii, kwani iko hatari ya misikiti hiyo kubaki kama maghala ya kutunzia vyakula.

Alisema mwislamu yoyote anayetaka kuwa mfuasi wa kweli wa dini hiyo lazima ajikite katika elimu kwa sababu ndio mahali pazuri pa kuwekeza na si kwingineko.

Mufti pia alizungumzia namna ya kupata walimu wazuri, akisema huwezi kuwapata bila kulipa mishahara mizuri.

SOURCE: MAJIRA
Hapo kwenye red pamenifurahisha sana. Safi sana Mufti wachape mdomo hawa watu.
 
Hongera kwa kuliona hili...ila kama vile umechelewa nina uhakiaka kama ungeanza na ushauri huu tangu uwe mufti kungekuwana mabadiliko makubwa sana kwenye jamii ya kiislam.....
 
Hamchoki kutuchokonoa! Sasa Mufti kasema inahusiana vipi na siasa....Mtatufuata hadi vyumbani.
Zaidi ya yote hayo kama kweli wakristu wamesoma na kusoma kwenyewe matunda yake ni haya, basi hiyo elimu siitaki.
 
haya ni matunda ya hotuba ya jk aliyoitoa siku ya idd kwenye msikiti wa gadhafi pale dodoma! bakwata ikiwa kama 'tawi' mojawapo la ccm hawana budi kutii maoni ya mwenyekiti wa chama.
 
Habari ya zamani sana..acheni kuchakachua mambo enyi wagalatia mlio..wapu...
 
Da kaazi kweli kweli,alikua wapi kuyasema haya wakati wote wa utawala wake? Mbona wenzake wangekua wamefika mbali lakn anasubiri mpaka Jk amuelekeze nae ndio anasema hii hatari.
Kiongozi mzuri ni yule anaesimamia kile anachokiamini.
 
Hamchoki kutuchokonoa! Sasa Mufti kasema inahusiana vipi na siasa....Mtatufuata hadi vyumbani.
Zaidi ya yote hayo kama kweli wakristu wamesoma na kusoma kwenyewe matunda yake ni haya, basi hiyo elimu siitaki.

Mkandara wewe mzee mwenzangu , unapinga Wakristo kusoma ? Unakosea wamesoma na umewakubali ndiyo maana hujaenda Uarabuni kwa waislam wenzio ila uko huko kwa Wakristo wasomi na umepata elimu leo wewe ni muislam mjanja msomi.Ongelea wakristo wa hapo ulipo .Wa Tanzania ni ma CCM wamechanganyika na waislam wanatumaliza .
 
Yale yale ya wasiokuwa na elimu.. Waarabu ni race sio dini na wazungu ni race sio dini..Ukiweza kuelewa hivyo kidogo elimu yako ya kuelewa inaweza kupanuka. Mbona Wachina wamesoma na sii wakristu?
 
Hamchoki kutuchokonoa! Sasa Mufti kasema inahusiana vipi na siasa....Mtatufuata hadi vyumbani.
Zaidi ya yote hayo kama kweli wakristu wamesoma na kusoma kwenyewe matunda yake ni haya, basi hiyo elimu siitaki.

Kaka Bob heshima mbele mkuu,

Naona umekuja kiimani zaidi leo, lakini ni matumaini yangu haujaingizwa kwenye ule mkenge wa mtandio.
 
Ndio maana nikasema hawaishi kutuchokonoa, lakini mwisho wa yote haya utakuja onekana nina mashaka sana kama hutafika ilipo Nigeria leo!

Ndugu zangu tuweke tofauti ya dini pembeni na tuangalie mstakabali wa Taifa letu,Katu hatuwezi kuwa kama Nigeria
 
Kabisaa elimu tu itawakomboa na kuwapa vyote wanavyotaka na kuwaepushia kuonekana waajabu kwa kuwalaumu wakristo kila kukicha,
 
huyo mufti akafanye kazi za ccm tu, hana msaada wowote kwa waislamu wa tz. yeye kama kiongozi kafanya nini kuhakikisha waislam wanasoma. mitaala yao mibovu kabisa ktk shule za msingi na sekondari kiasi kwamba havimwandai mwanafunzi kupata elimu ya mazingira inavyopaswa na kuishia kuwa na matokeo mabovu kabisa kuliko shule zote huku wao wanakula kodi za walala hoi tu huko na kuwakandamiza waislamu. fumua bakwata na iundwe upya au kuanzisha taasisi nyingine yenye mtizamo chanya kwa waislamu
 
Ndugu zangu tuweke tofauti ya dini pembeni na tuangalie mstakabali wa Taifa letu,Katu hatuwezi kuwa kama Nigeria
hatuwezi kuangalia msitakabali wa taife letu wakati tabaka moja linajiona ni superior kuliko jingine. watu wanashangilia kuona waislamu wanakosa elimu sababu ya mfumo mbovu kabisa wa kiutawala
 
Toeni huu upuuzi hapa!
Tz inasikitisha katika kila nyanja!
Kama ni udini, mbona tuna viongozi wa ngazi za juu kabisa wa dini zote........wame/wanafanya nini kuiokoa Tz??!

toeni upuuzi huu!! Ccm inajua kwa dini zenu na makabila yenu, wanaweza kuwachezea wanavyotaka coz imani imewafumba macho!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom