Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,797
- 12,239
Dalili hizi zimeanza kuonekana baada ya Shehe Mkuu wa BAKWATA Mufti Zuberi kuzitaka mamlaka kuharakishwa kusikilizwa kwa shauri lao. Ni dhahiri shahiri serikali haiwezi kupuuza ombi lake na hivyo DPP ama atashauriwa kulifuta shauri hilo au ataanzisha mchakato wa kusikilizwa shauri hilo haraka.
========
Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mkutano wa viongozi wa dini waliokutana kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.
Alisema ni miaka mingi sasa tangu kesi hiyo ianze kusikiliwa na kuomba wenye mamlaka ya kusimamia kesi kufanya haraka kusikiliza ili ifikie muafaka.
“Hatuwezi kuingilia mambo ya kisheria, lakini ninachoweza kuomba ni uharakishwaji wa kusikiliza kesi yao, kesi hii imekaa miaka mingi, suala hili niombe mamlaka husika ziharakishe kuisikiliza kwa sababu imekaa miaka mingi,” alisema Mufti na kuongeza:
“Usikilizwaji wa kesi kwa haraka na hukumu ikatolewa itajulikana nani ana hatia gani na achukuliwe hatua gani na nani hana, kuliko kukaa ndani muda mrefu bila kufahamu hatma yao.”
Miongoni mwa mambo mengine ambayo viongozi hao wa dini walizungumzia ni kuhusu vitendo vya ukatili vinavyoendelea kwa watoto na kuwataka wazazi kuwajibika katika malezi ya watoto wao.
“Hawa watoto ndiyo viongozi wa nchi tunaowategemea kesho, kwa hiyo tusipowajibika katika kuwatunza na kuwalinda tunakuwa tunaharibu taifa letu, ni vema kila mzazi, mlezi na jamii yote iwajibike katika kumlinda mtoto,”alisema Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)Jimbo la Mashariki na Pwani, Dk. Alex Malasusa.
Alisema: “Asilimia kubwa ya watoto huharibika tabia kutokana na kukosa uangalizi wa wazazi ambao wanabanwa na shughuli za kila siku, hivyo wanapaswa watenge muda wa malezi. Tuombe kwamba kila unapobarikiwa kupata mtoto, uwajibike pia na katika kumlea na kumlinda.”
Machi 28, mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan wakati akipokea taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020, aliiagiza kuharakishwa kwa kesi, kuziondoa zisizo na msingi ili kuondokana na idadi kubwa ya kesi ambazo serikali imekuwa ikishindwa.
Vilevile, Juni 13, mwaka huu, viongozi wa dini Zanzibar, walimwomba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi, kuangalia suala la viongozi hao wa uamsho ambao wako mahabusu kwa muda mrefu.
Miongoni mwa mambo waliyomwomba ni kuangalia kama wana hatia au la, badala ya kuendelea kusota rumande bila kujua hatima yao.
Chanzo: Nipashe