Muendelezo Vita Dawa ya Kulevya: Masogange apelekwa kwa Mkemia Mkuu

Sasa wanamchunguza Masogange kama anasafirisha dawa za kulevya wakati alishakamatwa akisafirisha????? Halafu miaka yote walikua wapi wakati agnes anakamtwa south Africa???

Kweli hii ndio nchi ya "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA"..
hahahahaaa wanamkamata mara ya pili kwani kipindi kile walikuwa hawajui hahahahaaa hii ndo nchi ya matamko tu
 
Sasa bila hata hiyo jitihada ya "angalao" kudaka mmojam1, watapunguaje sasa?
Unapochangia, ainisha mbinu unazoona wewe zinafaa kama wangelizitumia. Lakini kubwabwaja bila kuonesha njia unaweza kuonekana kama ni mnufaika flani'iv!

Mkuu big dealers wa hizi biashara wameshatajwa sana . So sioni sababu ya kutoa maelekezo ya nini kifanyike wakati watu walishaongea sana kuhusu hilo.

Kama wanataka kukamata watumiaji kwa nini wanahangaika na hao watu ambao mpaka uwapime ndio ujue kuwa anatumia kwa nini wasipite kwenye vituo vya daladala wakawakamata wote wanaobembea na kusinzia kama kuku mwenye mdondo?

Hii haijakaa sawa kabisa .

Mimi familia yangu imepata athari ya haya madawa so kuwakamata hao kina TID wala hijanipa faraja kila nikimuangalia anko wangu jinsi alivyoisha kwa hayo maunga nasikia hasira sana hasa ninapoona na inajulikana kabisa mtu fulani ni tajiri na biashara yake kubwa ni unga lakini haguswi.
 
Wauzaji na wasambazaji wanaowajua ni watumiaji. Hivyo logically ukitaka kuwajua na kuwakamata wauzaji na wasambazaji hawa njia nyepesi ni kuanza na watumiaji ambao wako kila mahala na ni rahisi kuwabaini.

Au nalo hili ni ngumu kulielewa? Mkakati ni kuwa wabane barabara hao watumiaji (kwa mateso ikibidi) hadi wataje waliowauzia hayo madawa. Baada ya hapo kawabane sawa sawa hao wauzaji hadi wakutajie hao wasambazaji walikozipata hizo dawa. Baada ya hapo wakamate na kuwabana barabara hao wasambazaji wataje walikozipata hizo dawa. Na endelea hivyo hadi mwisho wa mnyororo (chain) ambao ni viwanda na mashamba yanayozalisha hayo madawa.Viwanda na mashamba haya yako nchi za nje. Kwa hiyo ushirikishaji wa interpol utahitajika kuanzia stage fulani. Kwa hiyo tumeanza na stage 1 ya akina Masogange na akina Manji. We are in the right track my friend, be relaxed. Hawa watumiaji wakishathibitisha walikozipata hizo dawa, wanakuwa upande wa serikali kama mashaidi: hawafungwi jela bali wanaanza kutibiwa na kuwa rehabilitate kuwa raia wema. Wale watumiaji (baada ya kuthibitishwa chemically) ambao watakaidi kuwataja waliowauzia lazima wataipate fresh na wanaweza hata kufungwa jela hadi watakapotoa ushirikiano.
you are grossly underestimating the fight my friend! if it was that easy mapambano dhidi ya madawa ya kulevya yangekuwa a history lesson in schools. it is a continuous struggle and if you want to make it a success story basi dhamira lazima iwe ya dhati na capability ya wale ambao wako kwenye battle front lazima iwe juu. kufikiria kwamba a one off operation itamaliza kila kitu ni kujiweka pabaya
 
Sasa wanamchunguza Masogange kama anasafirisha dawa za kulevya wakati alishakamatwa akisafirisha????? Halafu miaka yote walikua wapi wakati agnes anakamtwa south Africa???

Kweli hii ndio nchi ya "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA"..
Walikuwa wap hakina nani? Alikamatwa lini?
 
Mtoto ana mkxndx huyo, nimekula hapo, yaani, Tz imebarikiwa jamani, kuna mizigo...

Anyway back to topic... Hii vita inageuka toka wasambazaji wakubwa, wadogo hadi kuwa WATUMIAJI... Mbona mwelekeo unapotezwa kabisa..

Maana Manji, Gwajima, eti nao wanahisiwa watumiaji..? Yaani vita imegeuka kupunguzwa nguvu kabisa, sbb lengo kuu ni kuwamaliza DRUG LORDS, sio watumiaji... Maana sasa kila anaechunguzwa tunasikia kama anatumia, VIPI WASAMBAZAJI, DRUG LORDS WAKO WAPI...? Hayo madawa ya kulevya yanatoka wapi..? Mbona mnapunguza makali toka wasambazaji, wauzaji wakuu hadi watumiaji..?

Hii vita ukali umepungua kuna nn tena..? Wasambazaji, wauzaji wako wapi..? Kila anaekamatwa tunaambiwa mtumiaji, eehh..
 
Watu wengi nadhani hiyo habari hawajaielewa ilivyo, hebu watulize kichwa na kuielewa. Mkemia mkuu haendi kuchunguzwa kama anasafirisha bali ni sampuli ya damu kujua kama anatumia.

Kamanda wa Dar kasema wanamchunguza kwenye mambo ya kubeba, kusafirisha pamoja na kutumia. Haikumaanishwa kuwa vipimo hivyo vyote vinachunguzwa kwa Mkemia. Kipimo cha kutumia tu ndiyo anategemewa Mkemia, ila hayo mengine yaliyobaki ni yanafanywa na Polisi wenyewe. Uchunguzi huchukua namna nyingi, kisayansi na mbinu nyngine za kitafiti. Hakumaanisha hapo wanamfanyia uchunguzi tuhuma zote kwa namna moja.

Tukija hilo suala la kukamatwa kwake miaka ya nyuma na kutumia factor hiyo kama ni kianzio cha kumuweka ndani tangu mapema, kama aliachiwa kwa kukosa ushahidi utaanzia wapi. Mkumbuke sheria inaangalia ushahidi, mtu ukikosa ushahidi wa kumuweka nguvuni hata kama unajua kweli kafanya suala hilo haitosaidia kitu. Huu ni udhaifu wa kawaida na mkumbuke sheria hiyo imeandikwa na Wanadamu kama sisi, wana mapungufu kama ilivyo mimi na wewe. Sasa unategemea walichokitunga kitaweza kutimiza kila hitaji. Haitotokea kwa alichotunga Mwanadamu. Udhaifu mkubwa wa sheria, haiwezi kufanya kazi kwa Mtuhumiwa bila ushahidi yakinifu.

Mliyopo humu ndani mnaweza kusema sana kuwa huyo Binti Agness, eti alitakiwa akamatwe mapema sana kwani alishashikwa huko nchini Afrika ya kusini. Hamjiulizi ni kwanini yupo huru hadi sasa? Jiulize hilo ndiyo mtajua ni ngumu namna gani kumtuhumu kama mnavyofanya kwa vinywa vyenu mkiona ni jambo rahisi na sheria itatimiza. Nani asiyejua huko Afrika ya kusini huyu aliachiwa na kutozwa faini huku kile kilichobebwa kikionekana ni kemikali za kutengeneza madawa ya kulevya na si dawa zenyewe. Huyo binti alishikwa na Ephedrine, hii iliwahi kutumika kama dawa mahospitalini ila iliachwa na baadhi ya wataalam kutokana na kuleta uraibu kama zilivyo dawa za kulevya ila hadi sasa inatumika ila kwa kibali maalum cha Daktari kwa baadhi ya nchi ilikuwa ikitumika kama dawa yakutuliza pumu.
 
Back
Top Bottom