Muda wa kurejea kupima H-PYLORI

Muda wa kurejea kupima H-PYLORI

Abdull hameed

Senior Member
Joined
Jan 29, 2025
Posts
106
Reaction score
191
Wakuu habari za kwenu njooni munipe muongozo juzi kati nilikutwa na h-pylori kipimo kilotumika ni cha damu,nikapewa dawa za kutumia amoxicillin,metronidazole na pantroprazole nimetumia siku 8 zimeisha hivi natakiwa nikae muda gani ili nirudi tena kuhakikisha kama nimepona?
 
Mbona hujamaliza dozi
Mana ilipaswa utumie kwa siku 14 kisha uendelee na pantoprazole kwa mwezi mzima
Baada ya kumaliza pantoprazole unakata week 2 ili ukapime tena
 
Kiongozi izo dawa nilopewa nimemaliza zote na daktari kaandika kabisa siku 7 na dawa zote zimeisha nilopewa
 
Ukisoma maelekezo yangu utaelewa wapi kwenye makosa panapotakiwa kurekebisha
 
Ili
Wakuu habari za kwenu njooni munipe muongozo juzi kati nilikutwa na h-pylori kipimo kilotumika ni cha damu,nikapewa dawa za kutumia amoxicillin,metronidazole na pantroprazole nimetumia siku 8 zimeisha hivi natakiwa nikae muda gani ili nirudi tena kuhakikisha kama nimepona?
Uliacha kumuuliza daktari unakuja kuuliza humu jukwaani? Kuna shida sehemu
 
Wakuu habari za kwenu njooni munipe muongozo juzi kati nilikutwa na h-pylori kipimo kilotumika ni cha damu,nikapewa dawa za kutumia amoxicillin,metronidazole na pantroprazole nimetumia siku 8 zimeisha hivi natakiwa nikae muda gani ili nirudi tena kuhakikisha kama nimepona?
Mkuu, huyo daktari kwa nini alitegemea kipimo cha damu tu? Ubaya wa kipimo cha damu ni kwamba huwezi kutofautisha kama una infection sasa hivi. Kitu wanachofanya kwenye kipimo cha damu ni ku-test antibodies za H-Pylori (kinga ya kupigana na hawa bacteria) kama unayo mwilini. Sasa kuwa na hizo antibodies ina maana either unao, au ulishaugua zamani na kupona na zimebakia tu antibodies. Kipimo wanachosema ni cha uhakika ni kile wanakupa chemical fulani unakunywa halafu unapewa mfuko wa nailoni unapumulia ndani wanaona kama hewa yako ina carbon dioxide, basi wanajua una hao bakteria. Au unapima choo. By the way Bongo nyoso. N hospital nyingi sana wanabambikia watu kuwa wana hawa bacteria bila kuwa nao. Ukweli ni kwamba wengi hawajui kupima sawasawa.
Kuhusu muda wa kupima tena ni wiki nne na kuendelea na ukipima damu inaweza kuonyesha unao wakati huna.
 
Nimeelewa vizuri sana ahsante kwa maelezo mazuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom