Sister Abigail
JF-Expert Member
- Sep 2, 2020
- 3,639
- 11,320
Sawa najua yako sikupangii matumizi, ila be present at the moment angalau itaonyesha utimamu wako.
Na ikikubidi omba udhuru kisha utarejea au kama hulitaki tukio usiende/usije/usishiriki. Inashangaza mtu anakuita Kwa maongezi lakini yuko busy mno na simu yake, focus yake imehama iko kwingine. Sasa ulimuitia nini mtu?
Mtu baada ya kupanga date na mtu, ukifika ye yuko busy na simu, wengine busy anachat huku anachekacheka we unabaki umeduwaa kakusahau😂
Hata kama una jambo la lazima basi mpe mwenzio hata dakika kumi mmalize alichokuitia kisha akuache na simu yako.
Unamuongelesha mtu badala akusikilize anahamia kwenye simu, unadhani bado anakusikiliza badala yake anaitika tu enhee, enhee...ulikuwa unasema? Halafu anarudi tena kwenye simu.
Tujifunze kuwa na kiasi, tusiruhusu hivi vifaa vitupelekeshe namna hiyo kuna muda wa kuwa busy kuperuzi, kuchat kwenye magroup na kuna muda wa kufocus kwenye mambo mengine nje ya simu. Shida Iko kwenye kubalance mzani.
Mzazi uko busy na simu hadi unamsahau mtoto, anakosa kampani na hata michezo toka kwako. Mahusiano yanakosa uhai, mwenza wako muda wote yuko busy na simu hamna muda wa kuongea mambo yenu. Mtu katoka mihangaikoni kwenye kazi zake, unaona huo ndio muda lakini bado yuko busy na simu mpaka kitandani busy na simu!
Watu mpaka zebra cross wanavuka huku wanaperuzi baadhi wanagongwa barabarani yote ni kukosa umakini. Ajali nyingine abiria mmelala dereva kule anachat huku anaendesha. Unaalikwa Kwa vikao/maongezi muhimu,we uko mbali unaperuzi.
Mtu anakusimamisha akuongeleshe jambo fulani unajibu huku unangalia simu, mambo mawili at the same time. Mpya zaidi siku hizi Kuna wanaozagamuliwa huku wanaperuzi kudadeki🤣🤣
NB: Sijaongelea kuacha matumizi ya simu, najua sio kuchat tu bali wengine kazi wanafanyia kwenye simu, biashara zinafanyika kwenye simu na mengine ya msingi. Ninachoongelea ni kubalance matumizi ya simu na matukio katika maisha halisi kuleta uwiano pande zote. Upande mmoja wa simu ukiwa na uzito Zaidi inaathiri upande wa pili.
Muwe na siku njema!
Sister Abigail♥️