Muasisi awashukia 'wabaya' wa CHADEMA

Muasisi awashukia 'wabaya' wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kitila kila wiki alikuwa anafanya makongamano ya vijana pale Mlimani leo kaambia alipewa rushwa ya laki mbili na CCM kukisaliti chama.

Wamemtumia. Sasa wanadhani hawamuhitaji tena

Nadhani kuna haja ya kulifikisha hili kwa msajili wa vyama...
 
Mkuu ZeMarcoPolo, umesomeka. Sasa hebu weka jamvini CV za Mbowe, Lema V/s Zitto, tudadavue nani kati yao alimudu umande na kupevuka kielimu ili Wadau tuchambue pumba na mchele!
 
Mzee Edwin Mtei ni muasisi na mmiliki wa Chadema.

Godbless Lema ni kijana wa Mtei.

Freeman Mbowe ni mkwe mpwa wa Mtei. Yaani huyu ana ukaribu na Mtei kama mme wa binti yake, lakini pia anamuita Mtei mjomba.

Godbless Lema na Mbowe ni marafiki wa karibu na ni binamu wa mbali - 6th cousins.

Uwepo wa Lema na Mbowe kwenye nafasi za juu za maamuzi ndani ya Chadema ndio kitu pekee kinachomfanya Mtei atulie shambani kwake Tengeru bila hofu. Anajua Chadema bado iko mikononi mwake. Maamuzi yote yanafanyika Tengeru halafu vikao vinakaa kuyapitisha tu.

Baada ya kijana wa Mtei, Godbless Lema kumshambulia mitandaoni mbunge mashuhuri kuliko wote Tanzania - Zitto Kabwe, ililazimika ajibiwe.

Baada ya Lema kujibiwa, ikaonekana hana hoja na momentum ikawa upande wa Zitto. Jambo hili limemsononesha sana Mtei na kumtia hasira. Pia imempa Mtei hofu kuu kuona kwamba upo uwezekano wa wanachama kukichukua chama kutoka mikononi mwake! Kutoka Tengeru chadema ingepelekwa matawini. Jambo hili Mtei ameshindwa kulivumilia.

Zitto alianza kushutumiwa na Chadema alipotangaza kugombea uenyekitu katika uchaguzi uliopita. Kabla ya hapo alionekana ni mtumishi mwema, alisifiwa na kupigiwa makofi anapoongea. Kosa lake lilikuwa kuhatarisha nafasi ya mkwe mpwa wa Mtei, Mbowe.

Zitto ameadhibiwa kwa kupinga maneno ya Lema kwenye mitandao. Pamoja na kwamba Zitto ni kiongozi wa Lema, lakini Lema ni more insider than Zitto in today's Chadema.

Kitila Mkumbo alitumiwa na Mzee Mtei kubadilisha matokeo ya viti maalum ili mabinti wa Mtei, Ndesamburo na wengine wanaowataka wapate Ubunge. Yeye Kitila hakuingiza mtu yeyote wake. Kura zilizopigwa na wajumbe zikafutwa na wabunge wakateuliea kwa kufuata vigezo vilivyotengenezwa kwa umakini wa hali ya juu na Kitila Mkumbo. Alichotaka Mtei kikafanikiwa.

Kosa la Kitila ni kumsema hadharani Henry Kilewo kwa kusambaza waraka wa majungu dhidi yake. Henry Kilewo alishirikiana na viongozi wengine wa Chadema kusambaza waraka wenye lengo la kumchafua Zitto na kutaja jina la Kitila. Waraka huu ulitolewa baada ya Lema kushindwa kwa hoja na Zitto. It is therefore reasonable to presume kwamba Lema anahusika na waraka huu.

Mzee Mtei alitaka Kitila akae kimya ili Zitto abaki peke yake. Lakini Kitila aliandika mitandaoni kuwa Zitto ni rafiki yake wa siku nyingi na kama mtu mzima hawezi kuchaguliwa rafiki. Jambo hili limemsononesha Mtei na kuhatarisha nguvu zake juu ya Kitila. Lema na Mbowe hawawezi kupinga jambo lolote analotaka Mtei. Ndio maana hata pale Mtei alipitoa unpopular comment kuhusu composition ya tume ya katiba, Mbowe aligoma kama mwenyekiti kudenounce kauli ya Mtei. Akamtuma Mnyika atoe tamko la kiujumlajumla kuwa Mtei ana haki ya kutoa maoni yake binafsi hata kama ni ya kibaguzi na yanahatarisha umoja wa kitaifa.

Tukumbushane tu kuwa Mtei alikuwa kijana msomi wakati harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika zikiendelea. Mtei aliombwa mara kadhaa kusaidia katika harakati hizo lakini alikataa. Mtei alikuwa mtumishi mtiifu wa wakoloni. Uhuru ulipopatikana, Mtei aliombwa tena kushiriki ujenzi wa Taifa.

This time Mtei alikubali kwa masharti kwamba alipwe mshahara sawa na waliokuwa wanalipwa wakoloni. Nyerere alikubali kwa shingo upande kwa vile hakukuwa na mtanzania mwingine aliyekuwa na elimu ya uchumi kama Mtei. Mtei akawa analipwa mshahara mkubwa kuliko Rais Nyerere.

Baada ya vita vya Uganda, uchumi wetu ulitetereka. Wananchi wakatakiwa kufunga mikanda (kuvumilia hali ngumu). Mtei hakutaka kuvumilia hali ngumu. Akamshauri Nyerere serikali ichukue mikopo mikubwa IMF na World Bank kwa masharti yao. Nyerere alikataa ukoloni huo mamboleo. Mtei akasusa kuwatumikia watanzania bila malipo manono. Akajiuzuru...

Ndio maana kijana wa Mtei, Lema hayuko tayari kuachia au kupunguza posho ya vikao. Hiyo ni falsafa aliyofundishwa na Mtei. Zitto anaadhibiwa kwa kupinga falsafa ya Mtei hadharani.
Lema ni kifaranga tu kilicho juu ya chungu lakini chini ya chungu hicho yuko Mtei.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai...
So Lema Alipokuwa TLP alikuwa ni kijana wa nani mpaka leo awe kijana wa Mtei??
 
Hv kweli mtoto aliekufa nilizaa mimi au nilipakaziwa tu? maana rafiki yangu analia kuliko mimi mfiwa naisitoshe wakati niko safari rafiki yangu huyu alikuwa karibu sana na familia yangu.

Marehemu ni mtoto wangu wa halali kweli au nilipakaziwa tu?
 
Chacha Wangwe alionekana adui kwa kugombea uenyekiti wa Chadema. Zitto naye tangu aonyeshe nia ya kugombea uenyekiti anaonekana mbaya.

Uchaguzi unaahirishwa. Ratiba ya uchaguzi mpaka atoe Mzee Mtei Tengeru.

Hiki chama ni kizungumkuti...
 
Mkuu ZeMarcoPolo, umesomeka. Sasa hebu weka jamvini CV za Mbowe, Lema V/s Zitto, tudadavue nani kati yao alimudu umande na kupevuka kielimu ili Wadau tuchambue pumba na mchele!

CV za Mbowe na Lema zinatosha kwenye kiganja. Ndio maana jina la Lema linasikika Kwenye vurugu tu na Mbowe yuko "too local"...
 
Hv kweli mtoto aliekufa nilizaa mimi au nilipakaziwa tu? maana rafiki yangu analia kuliko mimi mfiwa naisitoshe wakati niko safari rafiki yangu huyu alikuwa karibu sana na familia yangu.

Marehemu ni mtoto wangu wa halali kweli au nilipakaziwa tu?

Kijana hodari hupendwa na jamii hata kama baba yake alimtekeleza.

Ndio maana Obama alitelekezwa na baba yake lakini wamarekani wamempigania mpaka amekuwa Rais.

Mpo aina ya baba msiojali watoto mliozaa kwa hofu, wivu na kuwakosea heshima wake zenu eti inawezekana sio watoto wenu!
 
Kitila alirisk ajira yake kwa ajili ya Chadema. Leo anaonekana hana thamani kwa sababu kuna watu wanadhani mafanikio yameshapatikana!
alirisk ajira yake kivipi.., wakati ndo alipandishwa cheo kabisa. kada wa chadema wa majukwaani kabisa unaweza pewa ukuu wa chuo cha serikali (DUCE)?????. muulize kilichompata prof Baregu baada ya mkataba wake kuisha UDSM, walliachana nae wakati ndo mtaalam gwiji wa international relations pale department ya PSPA. watu tushajua kitambo, kuwa hawa si wenzetu
 
Hivi kuna mpenda maendeleo/ nabadiliko ambaye bado anaiona chadema kama eti ni mkombozi?
 
Zitto akome na kiherehere cha Kutaka Uenyekiti bila ridhaa ya mmliki wa chama! Zitto aelewe Chadema sio ya Wanachama,chadema ni ya Mtei na Mbowe,anajua hela iliyotumika hadi chadema kufikia hapa leo???? Mtei alitoa hela zake mfukoni
 
alirisk ajira yake kivipi.., wakati ndo alipandishwa cheo kabisa. kada wa chadema wa majukwaani kabisa unaweza pewa ukuu wa chuo cha serikali (DUCE)?????. muulize kilichompata prof Baregu baada ya mkataba wake kuisha UDSM, walliachana nae wakati ndo mtaalam gwiji wa international relations pale department ya PSPA. watu tushajua kitambo, kuwa hawa si wenzetu

Kitila ni mchapa kazi. Hicho ndicho kilichomuwezesha kupata ukuu wa kitengo.

Labda nikuulize, ni kigezo gani kilichotumiwa na Chadema kumpa Kitila kazi ya kuandaa vigezo vya ubunge wa viti maalum kama sio uwezo wake? Au hujui kuwa kura zilifutwa na Kitila akapewa hadidu za rejea kuandaa vigezo?
 
wadau nimekuwa nikifuatilia kwa muda sasa siasa za chama hiki ambacho wewmgne hupenda kukiita cha democrasia ila wengne twakiita cha kiimla.

Ukiangalia kwa makini utaona wazi kuwa cdm haina tofaut na tawala zinazoendeshwa na wafalme na malkia maana kuna wateule mle ambao hawataraji kuachia madaraka labda itokee siku mungu awapende zaidi.
Sasa swali mkangu ni je nani mfalme pale kati ya slaa,mtei na mbowe? Na je hawa vijana wanaoburuzwa kina mnyika,lema,&co. wanakaa upande gan katika ufalme huu?
Naomba majibu ya watu wenye maono sio wale vijana wa bavicha wanaodhani kuwa cdm ni kushabikia na kushangilia kila upuuzi bila kupambanua uhalisia wa mambo
 
Zitto akome na kiherehere cha Kutaka Uenyekiti bila ridhaa ya mmliki wa chama! Zitto aelewe Chadema sio ya Wanachama,chadema ni ya Mtei na Mbowe,anajua hela iliyotumika hadi chadema kufikia hapa leo???? Mtei alitoa hela zake mfukoni

Ndio maana tenda zote za manunuzi ya Chadema ziko chini ya Mtei...
 
wadau nimekuwa nikifuatilia kwa muda sasa siasa za chama hiki ambacho wengne hupenda kukiita cha democrasia ila wengne twakiita cha kiimla.

Ukiangalia kwa makini utaona wazi kuwa cdm haina tofaut na tawala zinazoendeshwa na wafalme na malkia maana kuna wateule mle ambao hawataraji kuachia madaraka labda itokee siku mungu awapende zaidi.
Sasa swali mkangu ni je nani mfalme pale kati ya slaa,mtei na mbowe? Na je hawa vijana wanaoburuzwa kina mnyika,lema,&co. wanakaa upande gan katika ufalme huu?
Naomba majibu ya watu wenye maono sio wale vijana wa bavicha wanaodhani kuwa cdm ni kushabikia na kushangilia kila upuuzi bila kupambanua uhalisia wa mambo
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom