Muasisi awashukia 'wabaya' wa CHADEMA

Muasisi awashukia 'wabaya' wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Mgogolo mnaukuza wenyewe, hakuna heshima ktk chama, mdogo kumtukana mkubwa, kulumbana ktk media na viongozi wana like badala ya kukemea, usipojiandaa kushinda jiandae kushindwa.

Body without head
 
teh teh,mkuu kuliko ccm?

katika karne hii kuwa na vijana wenye mawazo km ya vijana wa lumumba ni simanzi kwa taifa,vijana ndio chachu ya mabadiliko ya kweli popote pale duniani,sasa kuwa na vijana wanaokumbatia mfumo uliofeli for the last 50 yrs ni tatizo kubwa,vijana ambao hawataki mabadiliko ni aibu,lazima tukubali kuwa ccm is tired and there is no way we can grab something worth from them any how,they have to give chance peaceful to a new set of mind which can move us from here to somewhere else,huo ndio ukweli
 
Ndo maana NYERERE ALIMFUKUZA,mbinafsi sana huyu babu,alimlazimisha ZITTO ajitoe,akapite mkwee bila kupingwa,lkn bado ZITTO munaendelea kumfanyia fitna na mjungu,mfukuzeni kama hamumtaki,ila roho yake Mumwachie.Na kila CDM inavyosambaa mikoani ndivyo umiliki wa WACHAGGA unavyayayuka.
 
Bila kuifanya chadema chama cha kitaifa kwa kuleta uwiano sawa kwa nchi nzima hakifiki popote
 
Kwa upeo wako huo hata siku moja hutaweza kujua kipi cha maana na kipi sio...
Mkuu Baba V, Ze Macopolo na Mingo pesa za mafisadi zimewaondoa ufahamu kiasi kwamba mafisadi wakiwagiza watembe uchi mtaani kuipinga CHADEMA watakuwa tayari kuvua.
 
KITAIFA


mtei+px.jpg


Mwasisi wa Chadema,Edwin Mtei.PICHA|MAKTABA


Na Moses Mashalla, Mwananchi

Posted Jumanne,Novemba12 2013 saa 24:0 AM

KWA UFUPI

Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema kuna baadhi ya watu kutoka Chama Tawala cha CCM wanahakikisha wanatengeneza mifarakano kila kukicha ili kukivuruga Chadema.




Mwasisi wa Chadema,Edwin Mtei amesema kuna baadhi ya watu nchini wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanafanya njama za kukidhoofisha na hata kukipoteza kabisa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.



Mtei,alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kikiwa katika wakati mgumu baada ya baadhi ya viongozi wake kushambuliana kupitia mitandao ya kijamii, huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha,Samson Mwigamba akisimamishwa kwa madai ya kukiuka kanuni za chama hicho.



Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema kuna baadhi ya watu kutoka Chama Tawala cha CCM wanahakikisha wanatengeneza mifarakano kila kukicha ili kukivuruga Chadema.



Alisema mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli kuwa huenda CCM ikang”oka mwaka 2015, baadhi ya makada na viongozi wameanza kukesha wakifanya mbinu ya kukivuruga ili Chadema kisishike dola.



“Kuna watu wa CCM wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanatuvuruga, ili tusishike dola mimi nasema hawatuwezi”alisema Mtei



Hatahivyo,alisema kitendo cha kusimamishwa na hata kufukuzwa baadhi ya makada wa Chadema kimetokana na usaliti ndani ya chama hicho huku wengine wakikubali kutumiwa na CCM.





 
Mzee Mtei umeongea kweli tupu...

Nasari aliposema wataka kujitenga kanda ya kaskazini kuwa Jamuhuri,kwanini hakumkemea??Matamko yanataka kwa kumlenga ZITTO!!!MTEI ANAZEEKA VIBAYA.
 
Mzee Mtei ndiye
- Mwasisi wa (The Chagga Development Manifesto) hivi sasa Chadema.
- Mkwe wa mwenyekiti Mbowe.
- Ndiye anapanga safu ya juu ya uongozi chadema.
- Ni muasisi wa siasa za ukabila na udini
- Alipinga uchaguzi wa tume ya katiba kwa madai imejaa waislamu
- Alipinga kuungana na CUF kuunda kambi ya upinzani kwa madai ni waislamu
 
wachaga kubalini iki chama cha chadema kishakuwa cha kitaifa sio cha kaskazini tena...la sivyo wengi sana watakuwa wasaliti haiwezekani kila asiyetoka kaskazini mnasema haaminiki mjitafakari mna ka-nationalism flani kakipuuzi sana
 
wachaga kubalini iki chama cha chadema kishakuwa cha kitaifa sio cha kaskazini tena...la sivyo wengi sana watakuwa wasaliti haiwezekani kila asiyetoka kaskazini mnasema haaminiki mjitafakari mna ka-nationalism flani kakipuuzi sana
Sikubaliani na wewe kuwa Chadema ni chama cha kidini au cha kikabila hiyo ni propaganda za CCM,ila kwenye Chadema kuna kaudhaifu kidogo ambao bila viongozi wa juu kukaa chini na kuangalia hawa vijana wana waharibia maana hawajui siasa wao ni kufokafoka kama nyimbo za kizazi kipya,Mzee Mtei hebu waite wakina Pro Beregu,Pro safari, hata wakina Mabere ili wawafunde Hawa vijana wanaoleta vurugu,waige vijana wa NCCR niwapinzani lakini sio kama wakina Lema yani kweli sisi wapiga kura tunafedheeka sana.
 
Sikubaliani na wewe kuwa Chadema ni chama cha kidini au cha kikabila hiyo ni propaganda za CCM,ila kwenye Chadema kuna kaudhaifu kidogo ambao bila viongozi wa juu kukaa chini na kuangalia hawa vijana wana waharibia maana hawajui siasa wao ni kufokafoka kama nyimbo za kizazi kipya,Mzee Mtei hebu waite wakina Pro Beregu,Pro safari, hata wakina Mabere ili wawafunde Hawa vijana wanaoleta vurugu,waige vijana wa NCCR niwapinzani lakini sio kama wakina Lema yani kweli sisi wapiga kura tunafedheeka sana.

Mzayo,Lema ni janga la taifa.
 
Lema anapata kiburi cha kuropoka mitandaoni kwa sababu yeye ni kijana wa Mtei.

Mtei alikataa kushiriki kupigania uhuru, akakata kujitolea kuitumikia nchi katika kipindi kigumu na sasa anataka kuivuruga nchi kwa kupitia Chadema!!!

Ubinafsi mbaya sana...

View attachment 120937 hii picha mkuu iangalie vizuri tena angalia kwenye macho yao utajifunza kitu
 
Mwasisi wa CHADEMA Edwin Mtei amesema CCM wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanaivuruga CHADEMA ili isishike dola lakini ameapa kamwe hawatafanikiwa.

Amesema kuna watu kutoka chama tawala cha CCM wanahakikisha wanatengeneza mifarakano kila kukicha ili kukivuruga CHADEMA.

Mwasisi huyo mwenye heshima na ushawishi mkubwa ndani ya chama chake amesema kitendo cha kusimamishwa na hata kufukuzwa baadhi ya makada wa CHADEMA kimetokana na usaliti ndani ya chama hicho huku wengine wakikubali kutumiwa na CCM.

Source:Mwananchi.
 
maneno ya mitandao haina athari kwa chama ila labda athari za kisaikolojia kwa watu binafsi na wale wanaoanzisha THREAD HIZO kwani naona tayari wamechemsha.
 
Kweli baba, hii ni mcihongo ya MACCM inabidi kuwastukia kwa nguvu zote, ila nimesikitishwa hadi Mkumbo kunasa kwenye mtego huu!

Tafadhali daktari saikolojia yako ni kubwa kulishinda hili, angalia usiwe chanzo cha kufifisha matumaini ya watanzania, huyo best wako Zitto careful with him huenda anatumika bila kujijua, but something is very very wrong with him!
 
mtei amevurugwa. anawaacha wahuni wa chama chake akina lema, nasari na wengine wanavuruga chama anakurupuka kuilaumu ccm. akili ya kuku hii
 
mtei ee, hawa ni wana ccm ????? unazeeka vibaya

Viongozi Chadema wazipiga kavukavu kwenye mkutano wa Mbowe

Arusha. Mkutano wa Baraza la Uongozi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini juzi uligeuka ukumbi wa ngumi, baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kushushiwa kipigo.
Mwigamba alishushiwa kipigo hicho na baadhi ya viongozi wenzake wa chama kwa madai ya usaliti na tayari amesimamishwa uongozi kwa muda usiojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas jana alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na viongozi hao wa Chadema kufikishana polisi.
Alikutwa na zahama hiyo mbele ya viongozi wakuu wa Chadema Taifa, Mwenyekiti, Freeman Mbowe na mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei katika Hoteli ya Coridal Spring.
Viongozi hao wamekuwa wakifanya ziara za aina hiyo nchi nzima, kuimarisha chama na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani na uchaguzi mkuu ujao wa Rais na wabunge mwaka 2015.
Habari kutoka ndani ya mkutano huo zinaeleza kuwa hatua hiyo ilifuatia tuhuma kwamba Mwigamba alituma ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums, unaodaiwa kukichafua chama hicho.
Tukio hilo la aina yake lilitokea wakati viongozi wote wa juu wa chama hicho, wakiongozwa na Mbowe walipokuwa wakijadili mustakabali wa chama hicho, mkutano ambao ulihudhuriwa na wabunge karibu wote wa Chadema wa kanda hiyo.
Hata hivyo, wakati mijadala ikiendelea baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwamo Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema walimtuhumu Mwigamba kutuma ujumbe kwenye mtandao huo, uliokuwa ukizungumzia ufisadi ndani ya chama hicho, wakidai alitaka Mwenyekiti Mbowe kukubali kuchunguzwa.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwigamba alisema kuwa baada ya Lema kutoa tuhuma hizo aliungwa mkono na viongozi wengine na vijana waliokuwa wameimarisha ulinzi, kumvamia na kuanza kumpiga pamoja na kumnyang'anya kwa nguvu kompyuta mpakato (Laptop), aliyokuwa nayo, kisha kumpeleka Kituo Kikuu cha Polisi, mjini Arusha.
"Wamenipiga sana na kuniweka ndani, ila nashukuru Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Arusha (OCCID), alikuja na kunitoa saa 5:00 asubuhi," alisema Mwigamba.
Alisema kuwa leo katika mkutano wake na waandishi wa habari ataeleza yote yaliyotokea na hatua atakazochukua, kwa kuwa yeye ni kiongozi wa juu wa chama.
Hata hivyo, alieleza kwamba bado anashauriana na wanasheria wake kuona kama anaweza kuwachukulia hatua waliompinga.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom