Muasisi awashukia 'wabaya' wa CHADEMA

Muasisi awashukia 'wabaya' wa CHADEMA

Status
Not open for further replies.

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,742
Mwasisi wa Chadema,Edwin Mtei amesema kuna baadhi ya watu nchini wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanafanya njama za kukidhoofisha na hata kukipoteza kabisa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mtei,alitoa kauli hiyo wakati chama hicho kikiwa katika wakati mgumu baada ya baadhi ya viongozi wake kushambuliana kupitia mitandao ya kijamii, huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha,Samson Mwigamba akisimamishwa kwa madai ya kukiuka kanuni za chama hicho.

Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema kuna baadhi ya watu kutoka Chama Tawala cha CCM wanahakikisha wanatengeneza mifarakano kila kukicha ili kukivuruga Chadema.

Alisema mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli kuwa huenda CCM ikang"oka mwaka 2015, baadhi ya makada na viongozi wameanza kukesha wakifanya mbinu ya kukivuruga ili Chadema kisishike dola.

"Kuna watu wa CCM wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanatuvuruga, ili tusishike dola mimi nasema hawatuwezi" alisema Mtei

Hatahivyo, alisema kitendo cha kusimamishwa na hata kufukuzwa baadhi ya makada wa Chadema kimetokana na usaliti ndani ya chama hicho huku wengine wakikubali kutumiwa na CCM.

Chanzo: Mwasisi awashukia

Moja kati ya madai aliyoyatoa mheshimiwa aliyekuwa makamu wa mwenyekiti ni kwamba mzee mtei anawachagulia viongozi hili ni suala serious kuzungumzwa na kiongozi mkubwa kama huyu kama lingezungumzwa mitaani ingekuwa hakuna haja ya kujibu lakini majibu yako yanaitajika katika hili.

kuhusiana na sababu zingine alizozitoa kuhusiana na kuhujumu wagombea na watu kushindwa kurudisha kadi ni suala la kiutendaji zaidi kuliko hujuma kwani alilalamikiwa na viongozi wenzake huko Rukwa na siyo makao makuu kwahiyo kuja kuwalalamikia wenzake makao makuu naona kama ilikuwa ni excuse zaidi ya kutaka anayoyataka mwenyewe labda kwa kutumiwa au sababu binafsi.

binafsi naamini aliyekuwa makamu wa mwenyekiti alikuwa na matatizo ya utendaji kwani sijawahi kusikia akiongea bungeni wala kusikia kaitisha mkutano wa chama mahala popote kujaribu kujenga chama kwahiyo ushauri wangu kwa chadema muwe makini katika uteuzi wenu mjitahidi kutumia record ya mtu ktk kukitumikia chama na siyo majina yao mtu kama alikuwa dormant wakati akiwa ni mwananchama wa kawaida msitegemee akichaguliwa ndio ataanza kuifanya kazi huko ni kujidanganya au mtafanya makosa kama haya ya arfi.
MANENO YA MTEI Kuhusu Arfi kujiuzulu

Akizungumzia akiwa nyumban kwake tengeru kuhusu hatua ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Saidi Arfi kujiuzulu,
Mtei alisema kuwa inafaa kiongozi huyo ajitazame upya na kujisahihisha badala ya kuwa mlalamikaji kila siku.

"Aache kulalamika kwa sababu, wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti mimi nilisimamia uchaguzi. Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa mwenyekiti wa Chadema taifa alipaswa kujichunguza kwanza," alisema.

"Naunga mkono uamuzi wote wa Kamati Kuu, kuwasimamisha na kuwavua uongozi Naibu Katibu Mkuu wetu Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo."

Source: Mwananchi
 
Lema anapata kiburi cha kuropoka mitandaoni kwa sababu yeye ni kijana wa Mtei.

Mtei alikataa kushiriki kupigania uhuru, akakata kujitolea kuitumikia nchi katika kipindi kigumu na sasa anataka kuivuruga nchi kwa kupitia Chadema!!!

Ubinafsi mbaya sana...
 
Mtei hata uzima wake hauna tija kwa chama huwezi kumwacha lema anapiga watu matofari kwenye vikao wala haambiwi kitu halafu anasema ndani ya chadema kunawasaliti huu ni uhuni na kuwabeba baadhi ya watu ndani ya chama mfano lema.
 
CHADEMA itambue mamlukuki walojifanya wanaikimbia CCM na kuhamia CHADEMA hasa waliokuwa na nyadhifa za juu ndani ya CCM wengi sio kwa nia njema bali ni kwa kazi moja tu kuiba siri za chama na kukivuruga KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015. Kuweni macho viongozi na makamanda wote.
 
Mtei hata uzima wake hauna tija kwa chama huwezi kumwacha lema anapiga watu matofari kwenye vikao wala haambiwi kitu halafu anasema ndani ya chadema kunawasaliti huu ni uhuni na kuwabeba baadhi ya watu ndani ya chama mfano lema.

Neno usaliti/wasaliti ni ngonjera inayoimbwana Mtei, Slaa, Lema na Mbowe.

Hii ngonjera wanaitumia kama karata pekee ya kumchafua Zitto. Wamekosa hoja na wanajua wakienda kwa hoja Zitto atakitoa chama Tengeru na kukipeleka kwa wanachama.

Mtei anahofia his grip is loosening.
 
Lema anapata kiburi cha kuropoka mitandaoni kwa sababu yeye ni kijana wa Mtei.

Mtei alikataa kushiriki kupigania uhuru, akakata kujitolea kuitumikia nchi katika kipindi kigumu na sasa anataka kuivuruga nchi kwa kupitia Chadema!!!

Ubinafsi mbaya sana...

Can you Prove? Au umeropoka tu story za udaku.
 
ZITTO KABWE NI MWANACHADEMA DAMU MWENYE DHAMIRA YA AJABU NDANI YA CHAMA,KAMA KIONGOZI KWANINI MIGOGORO HII ISIMALIZWE KWA VIKAO VYA DHARURA NDANI YA CHAMA KAMA VIONGOZI WENYE BUSARA?what can i say there brain are not mature enogh,KUKIMBILIA KTK MITANDAO NA MAGAZETINI KWA WANAUME KAMILI HAKUTALETA TIJA,NAKUWA NAFANANISHA NA MIPASHO YA MAMA ZETU KTK TAARABU ni wakati muhafaka katibu mkuu kuitisha kikao cha dharura kumaliza TAARABU hizi na UKIKEKIKE huu, <namaanisha mwanamke akishindwa kumkabili mwenzie humvalia khanga ili ujumbe umfikie badala ya kukaa na kumaliza tatizo>, god bless CHADEMA
 
Lema anapata kiburi cha kuropoka mitandaoni kwa sababu yeye ni kijana wa Mtei.

Mtei alikataa kushiriki kupigania uhuru, akakata kujitolea kuitumikia nchi katika kipindi kigumu na sasa anataka kuivuruga nchi kwa kupitia Chadema!!!

Ubinafsi mbaya sana...
Wewe humfahamu MTEI,Endelea kuwa kuchi wa mtaani hapo ulaya,kama una uchungu na nchi hii usingezamia
huko kuukimbia umaskini ulioasisiwa na ccm
 
Lema anapata kiburi cha kuropoka mitandaoni kwa sababu yeye ni kijana wa Mtei.

Mtei alikataa kushiriki kupigania uhuru, akakata kujitolea kuitumikia nchi katika kipindi kigumu na sasa anataka kuivuruga nchi kwa kupitia Chadema!!!

Ubinafsi mbaya sana...

Chuki zako zimekufumba macho huoni tena ukweli, zimekukengeusha na kukufanya uwe mtumwa wa kile unachokipenda tu... this won't change the fact and you still have a wrong way to go...!!!
 
Kasome siasa vizuri, ni Uhuru upi ambao hakuupigania? kama likuwa ndani ya serikari hadi CCM inazaliwa, alafu unasemaje hakupigania uhuru?

Back
Top Bottom