muaji ni nani3

muaji ni nani3

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
1,982
Reaction score
2,934
Inaanzi hapa Alikaa gerezani miaka 20 akisubiri kunyongwa kwa mauaji ambayo hakuhusika.
i

Emily akiwa na wanafunzi wake anapewa picha zilizopigwa eneno la tukio wakati wa kukusanya ushahidi. Katika picha hizo wanaona koti la kuzuia baridi lililokuwa pembeni ya mwili wa Twila. Koti hilo lilikuwa ni kubwa likiwa na size kati ya 44-46, hii ilikuwa nisize kubwa kwa Skinner kwakuwa hakuwa na umbo kubwa la kuvaa koti kubwa kiasi hicho. Mtaalamu wa masuala ya kukusanya ushaidi eneo la tukio aliyekusanya ushahidi siku ya mauaji alisema bila shaka mhusika alikuwa kava koti hilo wakati akitenda mauaji hayo kutokana na sababu kwamba, sehemu ya mikono ya koti hiyo ilikuwa imelowa damu na pia koti zima lilikuwa lina madoa ya damu.

Kwa kuhisi huenda lile koti lilikuwa limevamiliwa na Uncle Bob, wanafunzi walifanya mahojiano na Beborah Ellis jirani yake Uncle Bob. Deborah ndiye aliyekuwa akimwangalia mkeweUncle Bob ambaye alikuwa mgonjwa asiyejiweza. Yafuatayo ni mahojiano baina ya wanafunzi na Deborah.

Mwanafunzi akimpa picha ya koti hilo Deborah: Hii ni picha ya koti lililokutwa eneo la tukio.

Deborah: Sijui lilifikaje eneo hilo ila hili ni koti la Robert donnell, nina hakika juu ya hilo. Na sikuwahi tena kumuona Robert akiwa kava koti hili baada ya kutokea mauaji hayo. Sikuwahi hata siku moja.

Pia Deborah anakumbuka kumuona Uncle Bob akilifanyia usafi gari lake asubuhi sana baada ya usiku wa mauaji. Anadai kuwa Bob alitoa kila kitu kwenye gari ikiwemo viti na makapeti na alifanya usafi ambao hakuwahi kumuona akiufanya kwenye gari hilo. Na Deboraha anadai mke wake Donnell alikuwa anahisi kuwa mumewe kahusika kwenye mauaji hayo na alikuwa kaimuuliza mara kwa mara ni nini kilitokea kwa kwa Twila na watoto wake na kama alikuwa kahusika.

Deborah anadai mke wake Bob alimwambia kuwa Bob alimwambia kama hatofunga mdomo wake na kuacha kumuuliza kuhusu masuala hayo atapata kilichowapata na atamfanya kama vile alivyowfanya watu hao anaowaulizia. Hii kauli ina maana alikuwa anamwambia kuwa atamuua kama alivyowaua akina Twila.

Miaka mitatu baada ya mauaji hayo, Robert Donnell alikuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa sana alipovamia trela la trekta na kuligonga, alifia pale pale kwenye ajali. Hivyo muda huu hakuwepo kuhojiwa wala kujitetea jambo ambalo aliyekuwa Mkuu wa kituo na aliyechunguzqa kesi hiyo na kumkamata Skinner Kachero Stubblefield anadai kwamba Donnell hakuwahi kuwa mshukiwa, hivyo kwakuwa alikuwa tayari amekwishafariki Skinner aliamua kumtuhumu mtu ambaye alijua wazi hawezi kujitetea maana ni marehemu tayari.

Kutokana na ugunduzi huu, mwanasheria ajulikanaye kama Robert Owen anaamua kuungana na wanasheria wake kukata rufaa dhidhi ya hukumu aliyopewa. Hallen pia ambaye alikuwa ni mkufunzi katika chuo Kikuu cha Texas, alishangaa kugundua kuwa lile koti halikuwahi kupelekwa maabara kwa ajili ya kupima DNA la aliyekuwa kalivaa. Anadai kuwa lile koti lilikuwa na nywele, jasho pia damu kitu ambacho ilikuwa ni rahisi kupata DNA kutoka kwenye koti lile. Lakini polisi hawakuwahi kufanya hivyo.

Owen aliamini alikuwa na sababu tosha zitakazomwezesha kukata rufaa kwakuwa waendesha mashitaka walishindwa kufanyia vipimo vya DNA lile koti na kuna ushahidi mwingine ambao hawakuuzingatia. Hapo sebuleni polisi walikuwa kuna mfuko wa plastiki mweusi wa takataka ambapo ndani yake kulikuwa na kisu na taulo kwa ajili ya kukaushia mikono baada ya kunawa. Pia vitu hivi polisi hawakuvifanyia vipimo. Pia kulikuwa na kisu kingine kilichopatikana kwenye mlango wa mbele wa kuingia kwenye nyumba ya Twila ambacho ndicho kinahisiwa kuwa ndicho kilitumika kuwaua Randy na Scooter, pia polisi hawakufanya vipimo pia.

Mwaka 2001 wanasheria wa Skinner waliomba mahakama itoe kibari cha kufanyia vipimo vya DNA, ushahidi uliokusanywa kutoka eneo la mauaji. Mwanasheria mkuu wa Wilaya John Man alikataa kwa kupinga ombi hilo kwamba kwenye kesi hilo hawakuhitaji kupima DNA kwakuwa walikuwa na ushahidi wa kutosha unaoonyesha kwamba Skinner ndiye alihusika na mauaji hayo. Hivyo walikuwa na sababu zote za kuamini kuwa watashinda pasipo kuhitaji kufanya kipimo cha DNA.

Skinner alisema tatizo ni kwamba Mwanasheria wa Wilaya alikuwa amekwishafanya maamuzi yake moja kwa moja usiku huo alipfika kwenye eneo mauaji hayo yaliyotokea. Alikuwa amekwisha hitimisha kwamba Skinner ndiye aliyetenda kosa hilo hivyo hawakutazama uwezekano wa kuwepo kwa mtu mwingine ila walikuwa wanafanya upelelezi wao wakilenga matokeo yahitimishe majibu kwamba Skinner ndiye muaji. Aliendela kusema kuwa kuna ushahidi kuwa mwanasheria alizungumza mara kadhaa na vyombo vya habari akimtuhumu kuwa Skinner ndiye muaji hata kabla ya Mahakam kumkuta na hatia hiyo. Mfano kuna chombo cha habari kilimnukuu John akisema kuwa ataiomba mahakama imhukumu kunyongwa Skinner kwa kosa alilotenda.

Skinner alizidi kudai kwamba, ni vigumu kwao kukiri kuwa walifanya makosa na kukubari upelelezi na ushahidi ufanyike upya. Alidai jambo ambalo wanqataka kwa muda huo ni yeye kunyongwa na habari ili habari yake iishe bila makosa yao kuonekana na anahisi watafanikiwa katika mpango huo.

John anadai kwamba mwanasheria wa mwanzo aliyemsimamia Skinner alikuwa anajua kuhusu ushahidi wa koti na visu na kwamba polisi hawakuufanyia vipimo, ila nay eye aliamua kutoomba ufanyiwe vipimo.

Emily baada ya kuona ,wamasehria wa wilaya kagoma kuruhusu vipimo vya DNA kufanyika hivyo ni vigumu rufaa ya Skinner kusikilizwa, aliamua kugeukia vyombo vya habari kwa kulipeleka hili swala katika vyombo vya habari ili lipate umaarufu na kuifanya msukumo wa kutaka ukweli ujulikane utoke kwa jamii ili kuilazimu serikali kuangalia upya hii kesi. Kila chombo cha habari kilichopata kusikia kisa hiki kutoka kwa Emily kilirusha habari hiyo.

Mwendesha kipindi wa Tv moja ajulikanaye kama nancy Grace aliwaalika Emily na mkufunzi mwenzake Profesa Protas pamoja na Mwanasheria wa wilaya Bwana John aktika kipindi chake ili apate kuwahoji na washindane kwa hoja. Hii ni baadhi ya shemu ya mahojiano:

Grace: Inawezekanaje Skinner akawa an damu kwenye nguo zake kama siyo muuaji na hakuwepo eneo la tukio.

Prof Protas: Skinner hakatai uwepo wake wakati mauaji yanatokea, bali anadai kwamba alikuwa hajitambui na alikuwa kalal kwenye kiti na ripoti ya vipimo vya ulevi inaonyesha kweli alikuwa kalewa. Pia wanafunzi wangu walihoji watu mbalimbali ambao wanaunga mkono kuwa Mjomba wake Twila ndiye anaweza kuwa muuaji halisi katika kesi hii.

John: Tulipata anfasi na tulikuwa na taarifa zote hizo unazosema, Donnell alifuatiliwa na akaonekana hakuwa na uhusika wowote. Unaongea tu habari ulizosikia kutoka huko mtaani ila nakwambia Skinner ndiye mhusika na kapata haki yake ambayo ni kunyongwa.

Prof Protas: Bwana John samahani, kuna alama za vidole zenye damu zilikutwa kwenye mlango na pia kwenye kisu. Je unaweza kuungana na mimi kwa kukubari kufanyika vipimo vya ushahidi uliokusanywa kutoka eneo la mauaji kabla ya mtu huyu asiye na hatia hajanyongwa?

Baada ya mwezi mmoja toka hicho kipindi cha mahojiano kirushwe, John alibadiri msimamo wake na kukubari kufanyika kwa vipimo vya DNA kimya kimya bila kuhusisha jopo la wanasheria wanaomtetea Skinner. Alichukua baadhi ya vitu na kuvituma kwenye maabara na kuwapa maelekezo nini wapime kutoka kwenye vitu hivyo.

Kati ya vitu alivyotuma kwa ajili ya kufanyia vipimo zilikuwemo neywe ambazo zilikutwa katika kiganja cha Twila. Kutokana na DNA majibu yalirudi kua nywele zile siyo za Skinner ila ni nywele ambazo mwenye nazo atakuwa na undugu naTwila upande wa mama. Nywele zile zilionekana toka mwanzo kuwa siyo za Twila wala watoto wake kutokana na kwamba zilikuwa nywele tatu zenye rangi tofauti japo kwa mbali ungehisi zina rangi moja. Hivyo wakina Emily walitegema aktika hali ya kawaida Mahakams ianze kufikiria kuwa mwenye hizo nywele huenda akawa Donnell. Lakini kwakuwa haikuweza kuthibitika moja kwa moja kuwa zile nywele zilikuwa za Donnell, mwanasheria wa wilaya alifunga kabisa uwezekanao wa kufanya DNA kwa vitu vingine kwakuwa yeye na wenzake walidai huenda zile nywele zilikuwa za watoto wake.

Stubblefield yeye alikuwa anahisi Skinner anajua kabisa kuwa alitenda kosa hilo ila tu anajaribu kukata rufaa moja baada ya nyingine akiwa anaamini kuwa kukata kwake rufaa kutamsaidia mahakama ya Texas kumwondolea hukumu ya kifo apewe hukumu ya maisha.

Skinner yeye anadai swala la kuthibtisha nani aliua siyo kazi yake hiyo ni kazi ya polisi, yeye kazi yake ni kuthibitsha kuwa hakuua na kupitia huo ushahidi ambao hawataki ufanyiwe vipimo vya DNA.

Mwaka 1996, mwanaharakati wa ufaransa mpinga adhabu ya kifo, mwanamama Sandrina O’jeoj alianza kuwa anaawaandikia barua baadhi ya wafungwa wanaosubiri kunyongwa kwenye gereza la Texas, mmoja kati ya wafungwa aliokuwa akiwandikia barua alikuwa Skinner. Andai kwamba Skinner ni mtu anayependa kujichanganya, ana huruma japo mara nyingine ni mkali. Anasema walianza kuwa wanaandikiana barua na Skinner alimuadikia kuhusu kisa chake na moja kwa moja alianza kuona kuwa kuna mashaka juu ya uhusika wake kwenye mauaji yale.

Akifanyiwa mahojiano na kituo cha TV cha CNN Sandrina aliuliza na mwendesha kipindi kwanini anaamini kuwa Skinner hakuhusika wakati hakuwepo eneo la tukio. Sandrina alijibu kwamba hii ni kutokana na sababu kwamba ushahidi uliokuwa eneo la tukio koti na kisu kilichotumika kuwaua watoto mpaka leo havijawahi kufanyiwa kipimo cha DNA.

Akiwa na shauku ya kutaka kujua ni kwanini John hakuwa amepeleka huo ushahidi kufanyiwa vipimo, Sandrina anaamua kusafiri kwenda Pampa kwa ajili ya kukutanana John. Alama za vidole vyenye damu zilizokuwa kwenye mlango na kwenye kisu hazikuwa za Skinner, je zilikuwa za nani na kwanini mwendesha mashitaka hafanyi juhudi kupima ili ijulikane ni alama za nani.

John alidai kwamba kukataa kwake kufanyaia DNA kwakila kitu ilitokana na sababu kwamba huwezi kumpakazia marehemu kuwa amehusika kwenye mauaji kwa kusingizia kwamba kuna vitu ambavyo havikupimwa DNA. Aliendelea kudai kuwa wanasheria wa Skinner hawakutaka kusisitiza vipimwe DNA kipindi cha kesi kwakuwa walijua kuwa isingemsaidia ila yeye baaada ya kusikia kuwa Donnell kafariki ndipo alianza kudai DNA kwa kuwa aliona ni njia itakayomsaidia kupata rufaa na kuanza kukata rufaa ikishindikana anakata nyingine na hiyo kweli ilimsaidia maana angekuwa amekwisha nyongwa kufikia wakati huo.

Owen yeye anadai kwamba , huo utetezi ni wa ajabu ukichukulia kwamba kuna mtu ambaye anasubiri kunyongwa nab ado anadai kutohusika kwake kwenye mauaji hayo, kwanini ili kuondoa mashaka wasipime kila kitu.

Mwaka 2005, Owen alikata rufaa akidai kwamba John alikosea kwa kutofanya vipimo vya DNA kwenye ushahidi uliokusanywa eneo la tukio, jambo amabalo lilifanya ushahidi kutokamilika. Pia John aligundua kwamba mwanasheriahuyo hakupeleka majibu ya vipimo vya pombe aliyofanyiwa Skinner mahakamani. Mtaalamu aliyepima kiwango cha pombe kwenye damu ya skinner aliandika kwenye ripoti yake kwake kiwango cha pombe kwenye damu ya Skinner kilikuwa 44 ambacho kinatosha kumfanya azimie na kutojitambua. Lakini John anapinga kwa kusema kwamba Skinner alikuwa kavunjika mbavu miezi miwili nyuma na alikuwa akitumia dawa za kutuliza maumivu ambazo zinaweza kuonekana kama pombe kwenye kipimo ndiyo maana hakuona umuhimu wa kupeleka majibu hayo mahakamani.

Kuthibitisha haya Mahakam ilimuita Daktari Michael Chimales ambaye alikuwa amemtibu Skinner majeraha ya kuvunjika mbavu nne miezi miwili kabla ya mauaji. Dakatari anadai kwamba Skinner alimwambia kuwa dawa za maumivu alizokuwa akimpatia hazimsaidii bado anahisi maumivu, aliamua kumuanzishia dawa zenye nguvu sawa na dawa za kulevya zijulikanazo kama Nacotics. Akiwa hapo hospitali anakumbuka kutokana na nguvu za dawa hiyo aliwamwambia nesi kuwa anataka akae amefungua mlango wa wodi alipokuwa kalazwa Skinner na awe anamtazama mara kwa mara, na nesi alikuja kumwambia dakatari kuwa alimuona Skinner akichomoa sindano ya drip kutoka mwilini mwakae na kuiweka kwenye mfuko wa suruali lake. Daktari anadai kuwa Skinner alikuwa mjanja sana hakutaka kununua madawa mtaani.

Owen anadai kwamba kutokana na maelezo ya daktari ni kwamba Skimmer alikuwa hapendi kununua dawa za kulevya mtaani na ndiyo maana hata dawa za maumivu ziliposhindwa kumsaidia alimfuata daktari ampe dawa mwenyewe, hii inaashiria kwamba ahkuwa mtumiaji wa mara kwa mara wa dawa za kulevya. Anaendelea kudai kwamba pombe na Nacotics alizokuwa akimeza lazima zilimfanya apoteze fahamu siku ile ya mauaji kwa kipimo cha 44, njia pekee ambayo ingeweza kumfanya asipoteze fahamu ni kama angekuwa mtumiaji wa dawa za kulevya mara kwa mara.

Skinner mwenyewe anasema walikuwa na tafrijajioni ile, alitumia dawa zakea na akanywa pombe baada ya hapo alianza hisi kizunguzungu, hakuweza kutembea vizuri hakuweza kuongea hivyo alijivuta mpaka sebuleni kajitupa kwenye kiti ambapo hakumbuki chochote mpaka alipokuja kushituka akakuta Twila amelala sakafuni na kuna mtu kasimama mbele yake na kisu.

Mahakama inakubariana na Owen kwamba, John alipashwa kuleta ripoti ya vipimo vya pombe mahakamani wakati wa kesi lakini waliongeza kuwa ripoti hii isngebadilisha maamuzi ya mahakama. Pia wanakubariana na John kwamba maamuzi yake ya kutopima DNA baadhi ya vitu ilikuwa ni njia sahihi nay a kisheria wakati wa kujaribu kumtia hatiani mtuhumiwa.

Owen anadai kila ushahidi waliokuwa wakiiuleta mahaka ilikuwa inadai usingeweza kubadilisha maamuzi ya mahakama kwakuwa haukuwa na nguvu. Owen anadai haukuwa na nguvu kwakuwamahakama ilikuwa ikitazama ushahidi kama kitu kimoja kimoja lakini ingeutazama kwa vitu vikiwa pamoja, kuna sababu ya kuwa na mashaka juu ya hukumu aliyopewa Skinner.

Kabla hata ya DNA kupimwa, mahakama inapanga tarehe ya Skinner kunyongwa ambayo ni tarehe 24, mwezi wa 5 mwaka 2010.

bonyeza link hapo chini subiri sekunde tano click next kuendelea na sehemu ya mwisho
Earn money on short links. Make short links and earn the biggest money - shorte.st
 
************************************Itanedelea*************************************
Hapa umefanya jambo jema mkuu tunakusubiri
 
Back
Top Bottom