Butola
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 2,290
- 756
.. Na pengine tuanzie kwenye mzizi wa tatizo lilopo leo kwakua umeamua kuja mwenyewe, tuzungumze kwa faida ya watanzania kwa ukweli bila kutia chumvi,....HIVI NINI TOFAUTI YA UCHAGUZI, KWA MAANA YA KANUNI NA TARATIBU ZILIZOTUMIKA KWENYE UCHAGUZI WA MEYA ARUSHA NA ZILE ZILIZOTUMIKA KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA HAI???
Kama hujui tofauti kati ya Hai na uchaguzi wa Meya wa Arusha basi tunahitaji kwenda shule upya. Ndiyo msingi wa kusema unaishi ahera, maana walioko ulimwenguni wanajua msingi wa mgogoro wa Arusha, na jinsi ccm ilivyo chanzo na sasa kupitia Mkuchika ndio mmeingia zaidi, kwa waziri kujiegeuza kuwa Mahakama.
Jamii inataka kujua ukweli, ni haki yao.
Dr.Slaa..
Naamini kuna watanzania wengi tulio bado duniani na tumeshatoka shule lakini hatujui bado tofauti ya uchaguzi wa Meya wa Arusha na ule wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, kwa mantiki kuwa kote huko vyama CCM-Arusha na CHADEMA-HAI walipeleka Wabunge wa Viti Maalumu wasio wakazi wa wilaya husika kuviwakilisha vyama hivyo kwenye halmashauri hizo, na kimsingi itakubalika kisheria.
kwa maana hiyo swali hili la Nape ni muhimu sana kwa kujadili mgogoro wa Umeya wa Arusha kwa ukweli na uwazi pasi kupigapiga chenga za kisiasa ambazo wewe mwenyewe umesema zimepitwa na wakati na ni vyema sasa ufanye kwa vitendo, naamini mjadala huu aliouanzisha Nape utaisaidia sana jamii ya Watanzania kuufahamu ukweli na kuuishi.