Muafaka CCM, CHADEMA waiva

Muafaka CCM, CHADEMA waiva

Jogi na wenzako,

KWANZA NI VIZURI SANA KULIJUA TATIZO LA ARUSHA BILA USHABIKI WA KISIASA. HIVI NINI SABABU YA CCM NA CHADEMA KUKAA MEZANI HASA KWA VIONGOZI WA KITAIFA.. UGOMVI ULIOPO NI KATI YA CHADEMA NA MADIWANI WAKE WA ARUSHA....CCM INAINGIAJE HAPA?

NANI ASIYEJUA KUWA MKAKATI WA VIONGOZI WA CHADEMA TAIFA NI KUTUMIA MGOGORO HUU WA ARUSHA KUMALIZA KESI INAYOWAKABILI, HASA BAADA YA KUONA KUWA IMEWAKALIA VIBAYA? HILI LAO CCM HATUMO.

TUNAJUA MEYA KACHAGULIWA KIHALALI NA MANISPAA INAENDELEA KUJENGWA, IKIZINGATIWA KUWA ILANI INAYOTEKELEZWA NI YETU , HATUNA MUDA WA KUJADILI WALA KULUMBANA KWA MIGOGORO ISIYOTUHUSU...TUNASUBIRI HIZO SIKU 30 ZA WATANI ZANGU...

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE.

Ndugu Nauye Jr, mwana CCM mwenzangu, salaam.

Napenda kukupa tahadhari mdogo wangu, ili uwe mwangalifu na mambo haya unayovamia sasa.

Ni juzi tu CCM walikupiga marufuku kwenda Igunga kendesha harakati za uchaguzi wa ubunge, je kama wakikuzuia kwenda Arusha pia, kazi yako ya Uenezi itachukua asimilia ngapi za eneo la Tanzania? Je huoni utnaanza kuwa mfungwa kutokana na wadhifa wako katika kuitumikia CCM mpya ya Kikwete?

Sasa nakuomba uwe unatulia, jifunze kutoka kwa Mzee Wilson Mkama, yeye ameshasoma wind direction na sasa yupo kama hayupo. Huo ni ushauri wa bure tu, ukipenda kuudharau hiari ni yako, lakini andika kwenye note book ili uje kunikumbuka baadae.

Wassalaam
(sn2139)
 
Jogi na wenzako,
KWANZA NI VIZURI SANA KULIJUA TATIZO LA ARUSHA BILA USHABIKI WA KISIASA. HIVI NINI SABABU YA CCM NA CHADEMA KUKAA MEZANI HASA KWA VIONGOZI WA KITAIFA.. UGOMVI ULIOPO NI KATI YA CHADEMA NA MADIWANI WAKE WA ARUSHA....CCM INAINGIAJE HAPA?

Nape,

Mimi ni kijana mwenzako.

Kuwepo kwa wingi wa wapenzi wa CHADEMA au CCM hakutuzuii watu kama mimi tusiotaka kabisa kuwa na Chama tuhoji maswali ambayo mnaweza kudhani tunaegemea wapinzani wenu.

Kumbuka wengine tuna asili ya kudadisi kila kitu hadi kupata ukweli yaani kila kitu kwangu ni research. Nilimsikiliza kwa makini Prime Minister akijibu lile swali bungeni na yule dada (nimemsahau) aliyeuliza akaongeza kuwa "kwa kuwa CHADEMA ni waongo kuhusu Arusha, wewe kama Waziri Mkuu una ushauri gani kwa madiwani waliofukuzwa".

Hebu ona hapa. Huyu dada na sehemu ya kubwa ya bunge ni kama walituambia kuwa kinachotoka kwenye mdomo wa Pinda ndiyo definitive truth. Kuna tofauti gani na kusema "Zidumu fikra sahihi za Waziri Mkuu" . Sasa fikra hizohizo zimewatokea puani hata wiki mbili hazijapita. Leo truth holder yuleyule Pinda anasema angechukua uamuzi kuhusu Jairo, wiki mbili baadaye eti tunakuja juu kadhalilishwa. Binafsi nimefurahi yaliyotoke bungeni ili iwe fundisho kwa kauli rahisirahisi zinazohitaji tafakari kubwa.

Kinachozungumzwa kwenye thread hii ni kwamba barua imetoka kwa Tendwa inaenda CCM na CHADEMA. Wote wewe na CCM wenzako pamoja CHADEMA ni reciepient wa hiyo barua. Walichofanya wenzako CHADEMA ni ku-publicize content za barua ambapo na sisi walau tunajua kuwa chini ya Tendwa mtakutana timu za CCM na CHADEMA. Tulikuwa hatujui sasa tumejua kilichomo.

CHama Chako kiliwahi kuficha ukweli kwamba sera ya bunge bado ni serikali mbili. Pius Msekwa akatoboa mbele ya waandishi kuwa "sasa serikali tatu ni sera kamili ya bunge". NIlikuwa mdogo hiyo 1994 ikitokea hii a G55 lakini ninacho kitabu cha Nyerere kiitwacho "Uongozi wetu na Hatima Ya Tanzania", namini unacho na kifungue ukurasa wa 19 uone.

Tulidhani kijana mwenzetu utaondokana na hii fichaficha ambayo mwishowe ni kuumbuka tu. TUliamini hivyo ulivyoanza kwa speed na viwango kana kwamba unaondokana na fichaficha uliposimamia maamuzi ya NEC yako kuhusu magamba. Leo unarudi kulekule kwa kitu kidogo sana kwa barua ya Tendwa ambayo imesambazwa kwa wadaua wengi. Je, ingekuwa imesambazwa kwako tu ingekuwaje?

Kinachojadiliwa humu ni content za barua ile. Nimesema sina haja ya kupendwa na CCM au CHADEMA. Ukinithibitishia kuwa CHADEMA wanaongopa kwamba content za barua si kama wanavyoeleza basi mimi binafsi nitaanziasha thread nyingine ikisema NAPE AIUMBUA CHADEMA KUHUSU BARUA YA TENDWA.

Na kama kweli hamuhusiki huko Arusha, hiyo barua inawataka nyinyi na CHADEMA mjadili nini. Kama unaamini kuwa mgogoro ni masuala ya ndani a CHADEMA na kwamba CCM mnaweza kualikwa basi ninakumbuka mwaka jana CCM mlialikwa kwa masuala ya ndani ya CHADEMA ambapo wewe ulkwenda na ukapokewa kwa furaha na vijana wa CHADEMA wakisema "njoo moja kwa moja" na wewe ukiwajibu "NImetumwa kumwakilisha Makamba". Hukukataa. Ulishiriki shughuli yao na sisi wafuatiliajia wa magazeti tukaona picha yako katikati ya wana-CHADEMA wakikushangilia.

Barua hiyo ya Tendwa siyo confidential. Wewe ni mwana JF nakupongeza kwa hilo. Hivyo kama CHADEMA ni waongo basi scan hiyo barua tutumie humu na kama nilivyosema nitakuwa wa kwanza kumlipua Slaa na wenzake.

Na kama hamhusiki kabisa, basi tutangazie wazi kuwa hakuna duniani mwene mamlaka ya kuwakutanisha nyie na CHADEMA hapa duniani kwa sababu mko kwenye mstari wa haki. Ukitutangazi hivyo nitakuwa wa kwanza kuwashambulia humu wanaokushambulia.

Jogi na wenzako,
TUNAJUA MEYA KACHAGULIWA KIHALALI NA MANISPAA INAENDELEA KUJENGWA, IKIZINGATIWA KUWA ILANI INAYOTEKELEZWA NI YETU , HATUNA MUDA WA KUJADILI WALA KULUMBANA KWA MIGOGORO ISIYOTUHUSU...TUNASUBIRI HIZO SIKU 30 ZA WATANI ZANGU...
TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE.

Tuletee kopi ya kanuni zote kuhusu uchaguzi wa meya Arusha. Hata kama ziko kanuni 200 wewe fanya jambo moja dogo sana. Tia tick kwenye kila moja kuonyesha kwamba CCM iliikamilisha kanuni ile bila utata. Mimi sina uvivu wa kusoma. Nimesema fanya hivyo hata kama ziko 200, lakini hata zikiwa 500 na nikaona tick yako imepita kwenye zote hizo bila hata moja kuvunjwa, basi nitakuwa wa kwanza kuwashambulia CHADEMA kuwa wamesababisha vurugu bure huko Arusha kiasi cha kufanya AICC ipoteze umaarufu kwa ukumbi wa Mlimani City wa pale Dar.

Ni hayo machache na ambayo ninaamini kwa uwezo wako kama kijana mwenzangu kwa nafasi yako nawe utayaona ni marahisi na utanitimizia.

Karibu na kidumu Chama Cha Mapinduzi.
 
eeeeeeh jamani chadema wanalazimisha ndoa bila shaka mshenga wa ndoa hìi ni tendwa yaani kweli ccm ina mvuto yaani cdm nao wanajigonga gonga kwa ccm.
 
Hii ni ishalla tosha kuwa chadema wanapenda amani, haki...hongera sana viongozi wangu wote wa chadema..dr slaa asante kwa ufafanuzi wako..nape asante kwa unafiki wako kama mlivyo ccm sijui kama kuna mtanzania atashangaa kwa unafiki wako maana hata mwenyekiti wako ni mnafiki lakini kama unataka kujua mziki wa baada siku 30, endeleeni na unafiki wenu safari hii hatutarudi majumbani mwetu mpaka tutakapo mngoa meya fake..mwambieni mbwa wenu andengenye aandae polisi wa kutosha..kutoka sehemu tofauti si arusha
 
eeeeeeh jamani chadema wanalazimisha ndoa bila shaka mshenga wa ndoa hìi ni tendwa yaani kweli ccm ina mvuto yaani cdm nao wanajigonga gonga kwa ccm.
chadema ni chama makini kuliko unavyoweza kufikiria...tunacho kitaka arusha ni haki itendeke kwa kufata kanuni na sheria za uchaguzi wa meya na si unafiki wa wajingawajinga kama pinda, mkuchika,makamba,nape na wengine..walivunja kanuni za uchanguzi kwa malengo yao leo wamegeuga mawakili hapo hapo mahakimu kwa waasi wa CDM..
 
Mazungumzo ya muafaka wa Umeya wa Arusha tofauti na ule wa CCM na CUF Zanzibar hayana msaada wowote kisiasa kwa CCM na wakati huohuo ni fursa muhimu ya kudhibitisha usahihi wa msimamo wa CHADEMA kwa wananchi, na hivyo kuidhoofisha CCM.

CCM watakuwa ni vipofu na wapungufu wa fikra kama watakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo kwa manufaa ya CHADEMA, nitawashangaa sana, katika hili msimamo huu wa Nape ndio msimamo sahihi kwa CCM.
 
Chadema wameshamalza kazi yao kutokana na kanun za katba yao. Inakuwa vp tena Tendwa anataka wakae pamoja!. Wanataka cdm watengue uamuz wao?. Madiwan si wamefungua kes mahakaman?. Naona kama Tendwa amekosa kaz ya Kufanya.
Ndo huyuhuyu Tendwa alosema kuwa uchaguzi wa Meya A town ulikuwa sawa, sasa anataka muafaka wa nini?
 
Jogi na wenzako,

KWANZA NI VIZURI SANA KULIJUA TATIZO LA ARUSHA BILA USHABIKI WA KISIASA. HIVI NINI SABABU YA CCM NA CHADEMA KUKAA MEZANI HASA KWA VIONGOZI WA KITAIFA.. UGOMVI ULIOPO NI KATI YA CHADEMA NA MADIWANI WAKE WA ARUSHA....CCM INAINGIAJE HAPA?

NANI ASIYEJUA KUWA MKAKATI WA VIONGOZI WA CHADEMA TAIFA NI KUTUMIA MGOGORO HUU WA ARUSHA KUMALIZA KESI INAYOWAKABILI, HASA BAADA YA KUONA KUWA IMEWAKALIA VIBAYA? HILI LAO CCM HATUMO.

TUNAJUA MEYA KACHAGULIWA KIHALALI NA MANISPAA INAENDELEA KUJENGWA, IKIZINGATIWA KUWA ILANI INAYOTEKELEZWA NI YETU , HATUNA MUDA WA KUJADILI WALA KULUMBANA KWA MIGOGORO ISIYOTUHUSU...TUNASUBIRI HIZO SIKU 30 ZA WATANI ZANGU...

TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE.
Kesi ya arusha imewakalia vibaya umejuaje mkuu??, au nawe unapewa data na mahakimu na njama zenu kuhakikisha mnawasafisha polisi walioagizwa kuua??? Kwanza utakuja lini arusha tunakusubiria kwa hamu sana mkuu, uje utoe haya majibu mbele ya umati wa wanaarusha tuliopigigwa risasi alafu utaona nini kitafuatia...
 
Dr. Slaa,

Kwanza nikiri kustushwa sana na kauli yako kuwa NAISHI AHERA!! BILA SHAKA MAANA YAKO NI KUWA MIE NIMEKUFA!!!! SASA SIJUI KAMA UNANITABIRIA KIFO AU VIPI SIJUI!!!

Any way tukiliacha hili la kunichuria wacha tuzungumze hili la Arusha.. Na pengine tuanzie kwenye mzizi wa tatizo lilopo leo kwakua umeamua kuja mwenyewe, tuzungumze kwa faida ya watanzania kwa ukweli bila kutia chumvi,....HIVI NINI TOFAUTI YA UCHAGUZI, KWA MAANA YA KANUNI NA TARATIBU ZILIZOTUMIKA KWENYE UCHAGUZI WA MEYA ARUSHA NA ZILE ZILIZOTUMIKA KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA HAI???
 
@Nape mnauye jr

unadhani uchaguzi wa meya Arusha ulikuwa halali?

kama ulikiukwa kanuni gani zilikiukwa na je uoni kukiukwa huku ni sababu ya maafa ya Arusha?

unaposema CCM haihusiki wakati mtu aliyewakingia kifua madiwani hawa ni kada wa CCM na kiongozi wa serikali je huoni kun mkono wa chama tawala?

Nape,
Ahsante. Sidhani nimekuchuria. Sisi ni viongozi, si vema tukafanya mambo kwa ushabiki. Kichwa cha habari chajieleza. Nilifikiri tunahitaji kujielekeza kwenye thread iliyoko mbele yetu.

Kama hujui tofauti kati ya Hai na uchaguzi wa Meya wa Arusha basi tunahitaji kwenda shule upya. Ndiyo msingi wa kusema unaishi ahera, maana walioko ulimwenguni wanajua msingi wa mgogoro wa Arusha, na jinsi ccm ilivyo chanzo na sasa kupitia Mkuchika ndio mmeingia zaidi, kwa waziri kujiegeuza kuwa Mahakama.

Msingi hapa ni kuwa Nimepokea Barua ya Tendwa na nimekwisha kuteua wajumbe kwa upande wa Chadema. Sasa mwenzetu ukisema ni majungu ni nani unamzuga?

Waziri Mkuu alijibu swali ndani ya Bunge, hadharani, na mimi nimetekeleza nilivyoandikiwa. Ulichotakiwa siyo kusema ni majungu bali kueleza CCM wamepata barua au vipi? Nadhani chenga zibaki kwenye uwanja wa "football", lakini siasa ziendeshwe kisasa, enzi za "politics is a dirty game" zimepita. Jamii inataka kujua ukweli, ni haki yao.

Dr. Slaa,

Kwanza nikiri kustushwa sana na kauli yako kuwa NAISHI AHERA!! BILA SHAKA MAANA YAKO NI KUWA MIE NIMEKUFA!!!! SASA SIJUI KAMA UNANITABIRIA KIFO AU VIPI SIJUI!!!

Any way tukiliacha hili la kunichuria wacha tuzungumze hili la Arusha.. Na pengine tuanzie kwenye mzizi wa tatizo lilopo leo kwakua umeamua kuja mwenyewe, tuzungumze kwa faida ya watanzania kwa ukweli bila kutia chumvi,....HIVI NINI TOFAUTI YA UCHAGUZI, KWA MAANA YA KANUNI NA TARATIBU ZILIZOTUMIKA KWENYE UCHAGUZI WA MEYA ARUSHA NA ZILE ZILIZOTUMIKA KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA HAI???
 
Nape,

Naona unaishi ahera.

i) kwa kauli hii ni dhahiri kuwa hujui mgogoro ulioko ni arusha unahusu nini. Chadema haina mgogoro na madiwani wake kwani iliisha kuwafukuza uanachama. Ni mtu asiyejua taratibu za sheria tu ndiye anaweza kutoa kauli kama ya kwako, au vinginevyo una agenda ambayo ni vyema ukaiweka hadharani

ii) Kesi cr/c. 5/2011 iliyoko High Court ya Arusha haina uhusiano na Madiwani bali ni kesi ya "unlawfull Assembly". Kesi iliyofunguliwa na Madiwani 5 ambayo hadi sasa sina namba yake inahusu "madiwani watano kuiomba Mahakama iwarudishie Uanachama wao". Hivyo hata wao wanajua kuwa wamevuliwa uanachama. Upotoshwaji wa aina hii ni wa ajabu, lakini tunaelewa kwa magamba hakuna lisilowezekana.
Unlawful assembly as pertaining to what?..Of course there's a connection between the Arusha mayoral election and the jan 5th illegal demo.
You have been(together with other CDM members) accused by Nape of trying to use the "mayoral election saga" as a tool to get the case thrown away,I personally don't think the route that you took was legal or even logical.Why are you trying to talk to the prime minister?,who is reaching out to the other?Is it CCM?
If you were not satisfied wth the way the election was conducted,why didn't you guys go to the court? How did Kaborou won kigoma elections back in the days? WAS IT THROUGH ILLEGAL DEMONSTRATIONS OR THROUGH THE COURTS?
As a prominent politician and a former pastor,can you tell us the reason(s) you guys chose not to go to court?....I'm a CCM member and I woldn't appreciate if my party will be dragged into this,unless the judiciary is involved.....keep the executive and the legislature out of this please,that sounds so absurd.And about Mipashos/vijembe/taarab......C'mon! you are better than that!
 
Dr. Slaa,<br />
<br />
Kwanza nikiri kustushwa sana na kauli yako kuwa NAISHI AHERA!! BILA SHAKA MAANA YAKO NI KUWA MIE NIMEKUFA!!!! SASA SIJUI KAMA UNANITABIRIA KIFO AU VIPI SIJUI!!! <br />
<br />
Any way tukiliacha hili la kunichuria wacha tuzungumze hili la Arusha.. Na pengine tuanzie kwenye mzizi wa tatizo lilopo leo kwakua umeamua kuja mwenyewe, tuzungumze kwa faida ya watanzania kwa ukweli bila kutia chumvi,....HIVI NINI TOFAUTI YA UCHAGUZI, KWA MAANA YA KANUNI NA TARATIBU ZILIZOTUMIKA KWENYE UCHAGUZI WA MEYA ARUSHA NA ZILE ZILIZOTUMIKA KWA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA HAI???
Nape unazidi kuchemka,1. unadai kuishi ni kumaanisha kufa? Sitaki kuamin kama hapo ndipo ukomo wako wa kufikiri ulipoishia. 2. Ni wewe uliyedai kwamba uchaguz ulikuwa halali, ni kazi yako kuthibitisha hili. Unapotaka kufananisha vitu visivyofanana unazidi kujichanganya kama siyo kuchanganyikiwa.
 
Dah Naona Nape kaingia mitini. Anapata mawaidha kutoka kwa Fisadi papa ajibuje swali lililoulizwa na Dr. wa Ukweli.
 
Swali kwa wanaofahamu.

Hivi jurisdiction ya Tendwa inakoma wapi? Samahani kwa kutumia lugha ya wenzetu kwa sababu Kiswahili hapo kimenipiga chenga.
 
is these two people real holders wa hayo majina au wanaigiza kama kweli vile. nape and slaa???
 
Back
Top Bottom