Mtwara: Watu watatu wamefariki baada ya kushambuliwa na nyati wakiwa shambani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Watu watatu wakazi wa kijiji cha Mahurunga kilichopo wilayani Mtwara, Mkoani Mtwara wamefariki baada ya kushambuliwa na nyati wakiwa shambani

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani humo ACP Nicodemus Katembo ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 20 Saa 5 Asubuhi wakati watu hao wakiwa shambani

ACP Katembo amewataja watu hao kuwa ni Rashid Bakari (40) Mkazi wa Kijiji cha Kitunguli, Salum Yusuf (46) na Said Musa (45) Wakazi wa Kijiji cha Mahurunga

Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi imeendelea kufafanua kuwa baada ya watu hao kushambuliwa taarifa zilifika kwa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanaolinda mpaka ambao walifika haraka eneo la tukio na kumuua Nyati huyo ambapo baada ya uchunguzi wa kitaalamu miili ya marehemu hao ilichukuliwa na ndugu kwa ajili ya mazishi na kuwataka wananchi kutoa taarifa wanapoona wanyamapori katika makazi ya watu
 
Si ajabu serikali hii ikatoa rambirambi ya sh.milioni 2 kwa kila familia iliyopoteza ndugu.
Nyara za serikali zimeua wananchi watii, serikali ilipite angalau sh.milioni 20 kwa kila familia.
Hapo hao watu wangemuua huyo nyati na kudakwa wangefungwa na kulipishwa mamilioni kila mmoja
 
Mungu awafariji wafiwa wote, huyo nyati auwawe na Askari wa Mali asili kisha aliwe nyama.
 
Huyo ni Nyati wa kutumwa haiwezekani Nyati awaue wote watatu mnamtazama tu. Ni kweli huyu mnyama hana mchezo ukimletea mambo sio.
 
Back
Top Bottom