Mtwara kuchele, Bandari ya Mtwara yazidi kuleta neema

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mtwara.jpg

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeeleza kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inatekeleza Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) (2021/22 – 2025/26), unaolenga kuboresha bandari zote za Tanzania ikiwemo Bandari ya Mtwara.

Imeelezwa kuwa kupitia mkakati huo Serikali imekamilisha uboreshaji wa Miundombinu ya bandari na ununuzi wa vifaa vipya (Reach stacker, Mobile Harbour Crane, Terminal Tractors na Ship To Shore Gantry Crane (SSG)) ambayo inatarajia kuwasili nchini mwezi Agosti 2022 kwa ajili ya Bandari ya Mtwara.

Vilevile Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia kupitia TPA imeendelea kuitangaza Bandari ya Mtwara ili kuvutia shehena kutoka ukanda wote wa maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor) unaojumuisha nchi tano za Msumbiji, Malawi, Zambia, DRC na visiwa vya Comoro.

Aidha, Serikali kupitia TPA imepunguza tozo za bandari ya Mtwara kwa asilimia 30 kuanzia Julai, 2021.

Hivi karibuni tumeshuhudia meli kubwa zenye kushusha mizigo kama Pembejeo za kilimo na kupakia mizigo kama Makaa ya mawe na Korosho zikifanya shughuli zake moja kwa moja katika bandari ya Mtwara tofauti na ilivyokuwa zamani.

Hii ni habari njema kwa wananchi wa Kusini mwa Tanzania ambao watakuwa wanufaika wakuu wa maboresho na matunda yanayopatikana.
 
Japo ana madhaifu yake mengi Ila Magufuli alidhamiria kufanya decentralization ya kiuchumi kwa vitendo yaani "Sio kila kitu Dar"
Na ni vyema Mama Samia sasa anamalizia hizi projects
 
Back
Top Bottom