Mtwara bado ni "Cinderella Province"

Mtwara bado ni "Cinderella Province"

Unajua serikali yetu imeshajiaminisha kabisa kwamba wananchi wa Tanazania ni watu wa kusahau, hatufikiri na hatuwezi kufanya kitu. Ahadi hizi wanazozitoa kuhusu Mtwara ni usanii wao wa kutaka kupunguza hasira na fujo zinazoendelea Mtwara ili utekelezaji wa mradi wa gesi uanze huku wakijua kabisa kwamba hawatatekeleza wanachokiahidi.

Wakati huo huo wanasahau kwamba wameahidi vitu vingi sana maeneo mengi ya Tanzania, wananchi wakishupalia ahadi hizo zitekelezwe na serikali patakalika? Ni dhahiri kabisa kwamba lengo hasa la ahadi hizi si kwa sababu serikali inawajali wana mtwara ila ni kufanikisha mradi wa gesi.

Inashangaza ahadi nyingi sana Mtwara. Nyingi Zkihitaji nguvu ya umeme. Mtwara haiko kwenye gridi ya taifa na kituo cha umeme hakijengwi Mtwara. Hivi viwanda na miradi iliyoahidiwa itaendeshwa na nini?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
EMT, Kiranga, THE BIG SHOW,

..tulishakuwa na mjadala wa gesi na mikoa ya kusini hapa JF.

..katika mjadala huo nilisisitiza kuboreshwa kwa sekta za ELIMU[to close achievement gap] na KILIMO, ili wananchi wa Mtwara waweze kupata uwezo wa kushiriki ktk uchumi mpya utakaotokana na gesi.

..ukisoma mchango wangu, na majibu niliyokuwa nikipata, hutashangaa kwanini tumefika hapa tulipo.

jokaKuu said:
AridityIndex,

..labda hujanielewa, but let me try one more time, then you can tell me why I am wrong.

..mimi sisemi wawekezaji walazimishwe kuajiri wazawa ambao hawako qualified au ni under qualified.

..pia hakuna mahali nimeelekeza kwamba vyuo vya elimu ya juu vichukue wanafunzi ambao hawana sifa.

..ninachopigania mimi ni kuwepo kwa mipango ambayo ita-reduce educational achievement gap kati ya hii mikoa ya kusini vs maeneo mengine ya Tanzania. kwanini shule bora ziwepo dsm,kilimanjaro,mbeya,na kagera?

..binafsi nimesoma na watu wa kusini, na wengine toka mikoa ya pembezoni. wana akili kama wa-Tanzania wenzao wengine. wakiweka mazingira bora watafanya vizuri.

..kingine ninachopigania ni kuwepo kwa sera na mipango ambayo itawezesha kuboreshwa kwa hali za maisha za wakulima wa maeneo ya kusini. tuhakikishe kwamba wanapatiwa pembe jeo, mbegu bora, maghala ya uhifadhi, mafunzo ya ukulima na ufugaji bora,masoko ya uhakika etc etc.

..tuhakikishe kwamba mkulima wa kusini halimi tena kwa kujikumu kwa chakula, bali analima kwa chakula na ziada anauza na kujipatia mapato ya kufanya shughuli nyingine za maendeleo.

..mkulima wa kusini akishaweza kuuza na kujipatia akiba, hapo ndipo atakapoweza kutamani mambo mengine kama elimu kwa watoto, nyumba bora, umeme na maji ndani ya nyumba,etc etc.

..ni kweli kila mtu inabidi abadilike[attitude change] kuanzia wananchi wa kusini wenyewe, watendaji na viongozi wa serikali,vyama vya siasa na kijamii etc etc.

..najua huko Kusini mmepigika mno kiasi kwamba mnadhani ni lazima mchukue BABY STEPS au MBEMBELEZE serikalini ndyo maendeleo yapatikane.

NB:

..hata kule kaskazini I am very uncomfortable with the fact kwamba shule zinazofanya vizuri zimejaa watoto wa wakubwa walioko DSM wakati wazawa wanaoishi karibu na shule hizo wameachiwa nafasi chache tu.

mjadala mzima uko hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/164542-mtwara-mkoa-masikini-unaoendesha-serikali-ya-tanzania-4.html
 
Last edited by a moderator:
Mtwara wamedanganywa kwa muda mrefu , na hata kwa hili la gesi mpaka sasa , kuna kila dalili wameshatekenyeka ,
kuwa na wasomi wachache wenye weledi na kukosa viongozi wazalendo na wanaoupenda mkoa wao ni tatizo kubwa la
watu wa Mtwara kwa sasa. Ukiangalia suala ambalo Mtwara wamelishupalia (UJENZI WA BOMBA LA GESI ), mpaka sasa
serikali imepiga propaganda kubwa , na JK amehitimisha kabisa kwa kuwalaghai watu wa Mtwara kwa ahadi nyingi wakati ujenzi wa bomba la gesi unaendelea .
Kama kweli serikali inaamini inachofanya ni sahihi , kwa nini wanishindwa kuwaambia watu wa Mtwara kwa uwazi bila kuficha kuficha maneno kwamba ujenzi wa bomba la gesi kwenda Kisarawe utaendelea ila nyie 'tutawajengea' viwanda
 
[video=youtube_share;7qDiI-sN3ug]http://youtu.be/7qDiI-sN3ug[/video]
 
EMT, Kiranga, THE BIG SHOW,

..tulishakuwa na mjadala wa gesi na mikoa ya kusini hapa JF.

..katika mjadala huo nilisisitiza kuboreshwa kwa sekta za ELIMU[to close achievement gap] na KILIMO, ili wananchi wa Mtwara waweze kupata uwezo wa kushiriki ktk uchumi mpya utakaotokana na gesi.

..ukisoma mchango wangu, na majibu niliyokuwa nikipata, hutashangaa kwanini tumefika hapa tulipo.

mjadala mzima uko hapa:

[/COLOR]https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/164542-mtwara-mkoa-masikini-unaoendesha-serikali-ya-tanzania-4.html

Mkuu hayo yamekuwa yakisema miaka na miaka lakini hakuna kinachofanyika.
 
Ninachoona mimi hapa ni mambo mawili

1. Kwanza ni uvivu wa serikali na watendaji wake muhimu katika kufanya utafiti kabla ya mipango yao.

2. Pili mipango [ahadi] ya kujenga mji wa Mtwara hauona tofauti yeyote na ahadi nyinginezo nyingi alizowahi kutoa mkuu wa kaya. Kwa vyovyote vile utekelezaji wake utakuwa wa mashaka sana
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hili suala la gesi ya Mtwara limeleta mengi. Watu wa mkoa wa Mara nao wananung'unika kwamba mbuga ya Serengeti ambayo asilimia mia moja iko mkoani humo inawanufaisha watu wa Arusha. Kwamba ndege zinatua KIA watalii wanapelekwa kwa magari ya matajiri wa Arusha kwenda kuona wanyama Serengeti na kisha kurudi Arusha. Wanasema Arusha imejengwa kwa kiasi kikubwa na Serengeti. Hivyo basi wanataka uwanja wa ndege wa Kimataifa Mkoani Mara ili watalii washukie Mkoani kwao na kupelekwa mbugani kutokea aidha Musoma au Serengeti na kama wanarudi basi warudi mjini Musoma ili kuimarisha uchumi wa mji huo.

Pia wanasema kuna tetesi kwamba wana Arusha wanshirikiana na Wakenya kupinga kujengwa kwa barabara ya lami toka Musoma kupitia mbugani! Nao wanataka wafaidi maliasili yao!

Kwa hiyo tukiwa tunashangilia gesi ya Mtwara tusisahau maliasili zingine.

Mkuu EMT kwa hali hii tutafika kweli?
 
Kama tutaendelea kuwa na bad management rasilimali zetu, then tunaweza tisifike. Kimsingi watu walio karibu na zilipo rasilimali wanalalamikia bad management.

Bad management kwa sababu jamii inayozunguka rasilimali hizo haihusiswi katika kuandaa taratibu na mipango ya ku-exploit hizo resources. Maamuzi yanafanywa mbali tena na watu ambao hawana connection na eneo husika.

Jamii zilizo karibu na rasilimali zina haki yak ku-device their management institutions and plans under the recognition by the government.

Viongozi ambao wako accountable kwa jamii lazima wazilinde hizo rasilimali na kuhakikisha kuwa zinakuwa exploited kulingangana na taratibu ambazo zimewekwa na kuwaathibu wale wote wanaovunja hizo taratibu.

Haya hayafanyiki na ndiyo maana kuna manung'uniko kila mahali.
 
banner14.jpg

Katika thread yangu ya Mtwara: Ilipotoka, ipo wapi sasa na inaelekea wapi nilizungumzia kitabu cha Michael Longfold kiitwacho “The Flag Changed at Midnight: Tanganyika’s Progress towards Independence” kilichochapishwa mwaka 2001. Katika kitabu hiki, Michael Longfold anaelezea ushuhuda wake wa macho akiwa kama mfanyakazi (District Officer - Mtwara) wakati wa utawala wa kikoloni miaka 10 ya mwisho kabla ya Tanganyika kupata uhuru. Kwenye Sura ya Nne yenye kichwa cha habari “Southern Province”, mwandishi anasema (nimetafsiri kwa Kiswahili):

“Mwanzoni, mji wa Mtwara ulikuwa umepangwa kusaidia maelfu ya wakazi wake hapo baadae na pia kuvutia wakazi wapya. Waingereza walikuwa na mpango wa kujenga mji maarufu wenye vitu kama maktaba, sehemu za kuombea, shule, hospitali, kumbi za sinema, n.k. Lakini mipango yote hii iliwekwa kapuni baada ya kuanguka kwa kilimo cha karanga.”

Kupata picha kamili ya Mtwara wakati wa ukoloni unaweza kusoma article ya Ronald M Munga: Makala toka Mtwara: Gesi na Maandamano; Nani haeleweki? na thread yangu ya Mtwara: Ilipotoka, ipo wapi sasa na inaelekea wapi?

Katika hotuba yake kwa taifa ya 31 Jamuary 2013, Rais Jakaya Kikwete amerudia yale yale yaliyosemwa na wakoloni zaidi ya miaka 60 iliyopita kwa kusema:

“Kupanga Mji wa Mtwara

Ndugu Wananchi;
Baada ya kutembelea bandari ya Mtwara na Chuo cha VETA, nilikaa na kuzungumza na viongozi wa Serikali na Manispaa ya Mtwara. Katika mazungumzo yangu nao niliwasisitizia umuhimu wa kuwa na
mpango kabambe wa kuendeleza mji wa Mtwara – (Mtwara Masterplan) Mpango ambao utawezesha kujengwa mji mkubwa wa kisasa unaokidhi mahitaji ya mji wa uchumi wa gesi. Niliwataka wahakikishe kuwa kuna maeneo ya viwanda, biashara, makazi, mahoteli, huduma za afya, elimu, mapumziko na burudani, viwanja vya michezo na kadhalika. Kazi ya kutayarisha Masterplan hiyo imeanza na Manispaa ya Mtwara inashirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi.”

Inaonekana alichosema Rais Kikweye siyo kipya. Mpango wa kujenga mji wa Mtwara kama mji mkubwa kusini mwa Tanzania ulianza tokea miaka ya 1950s. Ulikuwa ni mpango kabambe wa serikali ya kikoloni chini ya mpango mzima wa kilimo cha karanga. Mpango huu ulianzishwa na serikali ya Labour ya Uingereza iliyoingia madarakani mwaka 1945 chini wa Waziri Mkuu, Clement Attlee. Lakini madhumuni ya kuanzishwa kwa kilimo cha karanga Nachingwea ilikuwa siyo kwa ajili ya kujenga mji wa mtwara bali moja ya sehemu ya kutatua tatizo la utapiamlo nchini Uingereza; tatizo ambalo lilisababishwa na Vita Kuu ya Pili ya Dunia

Leo hii zaidi ya miaka 60 bado tunazungumzia kuujenga mji wa Mtwara. Tena hii ni baada ya gesi kugunduliwa Mtwara. Kama siyo hii gesi basi wala serikali isingekuwa na mpango wa kuuendeleza mji wa Mtwara. Kama siyo malalamiko ya watu wa kusini, gesi ungevunwa na kupelekwa Dar Es Salaam kutatua tatizo la utapiaumeme na Mtwara kubakia hivyo hivyo kama ilivyo Mwadui - Shinyanga. Sana sana Mtwara ingeachiwa mabaki ya gesi aka maganda ya karanga (kama wakoloni wangefanikiwa na kilimo chao cha karanga).

Ghafla Mtwara imekuwa tena a “Cinderella Province”
kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni. “Cinderella” maana yake ni “ mtu au kitu ambacho uzuri au uwezo wake haujatambulikana” au uzuri/uwezo wake unatambuliwa ghafla baada ya muda mrefu wa kutotambuliwa. Zaidi ya miaka 60, leo ndiyo serikali inashtuka kuwa Mtwara inahitaji kujengwa?

Mkuu kama ulisikia vizuri hotuba ya mwisho wa mwezi Januari aliyotoa Rais, kuna mameno mengi sana ya kukatisha tamaa. Ni mipango mipango mipango mipango na mipango, tuna mipango ya toka mwaka 1954. Kwa mtu aliyezaliwa mwaka 1954 huenda mpaka sasa atakuwa anajua kuna mpango wa kuundeleza mji wa mtwara. Lakini kinachotakiwa ni nini, mipango au kuona utekelezaji wa kweli wa mipango hiyo.

Ukweli ni kwamba mindset ya serikali ni kuwa Tanzania ni Dar es salaam, mikoa yote kwasasa inashuka na hata Dar es salaam yenyewe imeharibika sana ikilinganishwa na ile ya mwaka 1954, chafu zaidi, ovyo zaidi.
 
Soma mipango ya taifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013, mingapi imetekelezwa? http://www.mipango.go.tz/documents/MPANGO WA MAENDELEO final.pdf
 
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewaonya watu wanaosababisha uvunjifu wa amani nchini humo kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Onyo hilo linafuatia ghasia ambapo ofisi kadha, maduka na nyumba zimechomwa katika mkoa wa Mtwara ulioko kusini mashariki mwa Tanzania leo.

Akihutubia kupitia televisheni ya taifa, TBC1, Rais Kikwete amesema wale waliokamatwa na polisi wakati wa ghasia hizo watashitakiwa.
Ghasia hizo zilianza muda mfupi baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni.

Akizungumzia madai ya waandamanaji hao, Rais Kikwete amesisitiza kuwa raslimali za nchi ni mali ya taifa zima. Amesema mkoa wa Mtwara haujatelekezwa na kusema kwamba kuna mipango ya kutumia gesi hiyo kujenga viwanda vya mbolea na kutumia gesi hiyo asilia kuzalisha nishati ya umeme kwa mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma ili kuunganishwa katika gridi ya taifa.: http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2013/05/130522_mtwara_chaos_gas.shtml

Hapo kwenye red ni yale yale ya tokea zama za ukoloni.

Kwamba kuna mpango. Kila serikali ikiingia madarakani inakuja na gia ile ile kuwa kuna mpango.

Mpango mpango mpango mpango mpango ambao hautekelezwi kwa zaidi ya miaka 60 sasa?

cc Bongolander
 
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewaonya watu wanaosababisha uvunjifu wa amani nchini humo kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Onyo hilo linafuatia ghasia ambapo ofisi kadha, maduka na nyumba zimechomwa katika mkoa wa Mtwara ulioko kusini mashariki mwa Tanzania leo.

Akihutubia kupitia televisheni ya taifa, TBC1, Rais Kikwete amesema wale waliokamatwa na polisi wakati wa ghasia hizo watashitakiwa.
Ghasia hizo zilianza muda mfupi baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni.

Akizungumzia madai ya waandamanaji hao, Rais Kikwete amesisitiza kuwa raslimali za nchi ni mali ya taifa zima. Amesema mkoa wa Mtwara haujatelekezwa na kusema kwamba kuna mipango ya kutumia gesi hiyo kujenga viwanda vya mbolea na kutumia gesi hiyo asilia kuzalisha nishati ya umeme kwa mikoa ya Mtwara, Lindi, na Ruvuma ili kuunganishwa katika gridi ya taifa.: Kikwete akemea vikali vurugu Mtwara - BBC Swahili - Habari

Hapo kwenye red ni yale yale ya tokea zama za ukoloni.

Kwamba kuna mpango. Kila serikali ikiingia madarakani inakuja na gia ile ile kuwa kuna mpango.

Mpango mpango mpango mpango mpango ambao hautekelezwi kwa zaidi ya miaka 60 sasa?

cc Bongolander

No thanks,
Hell No..!!

Sisi sasa tumeghairi,hatutaki tena kuskia mipango yao hiyo ya kwenye vitabu na makaratasi...

Tunataka sasa wakae wasikilize mipango yetu sisi...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mkuu unajua wananchi wanakuwa wajinga kwa muda fulani, hawawezi kuwa wajinga kwa siku zote. So Nyerere alikuja na mapngo wake, Mwinyi na wake, Mkapa na wake, JK na mipango yake....lakini serikali hina mpango hata mmoja wa kuendeleza watu wa Lindi na mtwara, kama serikali ingekuwa na mpango bila shaka ungekuwa unatekelezwa na kungekuwa na kitu kinafanyika. Tunachokiona ni kuwa wananchi hawataki kuendelea kuwa lapdogs, wanatambua kuwa wao ni watu.
 
Mwaka 1905-1907 Kinjeketile Ngwale wa Ngarambe hakuwaongoza Wangoni tu bali aliongoza jamii mbalimbali za katikati na kusini mwa nchi yetu kupigana vita vya kumuondoa Mjerumani kwenye jamii yao baada ya kuingia kwenye maeneo yao na KUWALAZIMISHA KULIMA PAMBA NA KULIPA KODI. Ni maeneo mengi nchin Mjerumani alifanya kazi hizo kwa kutumikisha na kuwatesa watu,lkn ni eneo hilo la Kusini mwa Tanganyika waliweza kuungana kwa kiasi kikubwa sana na kupinga ukandamizaji wa Wajerumani.

Kihistoria vita hivi vya majimaji viliamsha uelewa na hari miongoni mwa Watanganyika ktk jamii zote na kuona haja ya kumuondoa Mkoloni huyo.

Kimsingi huwezi taja mapambano ya uhuru wa Tanganyika bila kutaja WATU WA KUSINI AU VITA YA MAJIMAJI.Kupitia majimaji watu walijifunza mengi sana hasa umoja,kwani wengi walikufa ktk vita ile lkn haikuwkatisha tamaa ktk kutafuta haki yao.

Yanayotokea leo Mtwara na sehemu ya Kusini mwa Tanganyika kwa sasa ni maswala ambayo Kihistoria yana nguvu.Eneo hilo ni eneo la Kimapinduzi.

My Take:
Kama jamii hizo ziliweza kumpinga tu Mjerumani kwa kuwalazimisha kulima pamba na kulipa kodi na hali aliwajengea babdari na reli, Ccm msitegemee watu hao watawaacha mchukue gesi kilaini kama mnasukuma mlevi.
SERIKALI KAENI MUONGEE NA WATU HAO,KUWENI VIONGOZI NA SI WATAWALA
JUENI KUWA ENEO LA KUSINI KIHISTORIA NI ENEO LA MAPINDUZI,ANGALIA MAPINDUZI YA KUIONDOA SERIKALI YENU YASIJEANZIA KUSINI KAMA HISTORIA INAVYOONESHA.
 
Mkuu sikio la kufa halisikii dawa, watayapuuza maneno yako. Bila kutumia busara taifa litaangamia. Imagine, nchi yetu iko kwenye misuguano na majirani, ilikuwa malawi na sasa tumeongeza M23 na washirika wake. Kwa ndani kuna udini na sasa kugombea rasilimali. Pia, mipaka yetu iko very loose, bahari ndo haina ulinzi watu wanaingiza bidhaa za magendo. Hivi kweli M23 wakiamua kupenyeza shehena ya silaha nchini tutasalimika kweli? Ushauri wangu, vijana wetu wako vitani sisi tuliobaki nchini tushikamane vinginevyo tunajichimbia kaburi letu wenyewe.
 
comon sense ni muhimu kweli.nimekubali rais alibaka uchaguzi uliopita.hekima hana kabisa.swala ni kuwasikiliza wananchi .sio kutumia mbinu ya zamani ya nguvu.kwani uoni ya huko syria,misri,Tunisia.HEKIMA HEKIMA HEKIMA IMETOWEKA .RAIS HANA HEKIMA.CCM TUMEIZIKA SASA VIZURI SANA.KILA MTU ATOE ELIMU KWA RAFIKI KIJIJINI KWAKE KUWA CCM LAZIMA ITOKE MADARAKANI UCHAGUZI UJAO.TUMA TEXT MSG KILA KONA YA NCHI JINSI YA KULINDA KURA NA WANANCHI WAKIPEWA PESA WACHUKUE KWANI NI ZAO ,NA WAPIGIE KURA CHADEMA.
 
Mkuu nahisi wachukue ripoti yako iwe sehemu ya sera ya gesi kwenye manufaa kwa mtwara na way forward kwa mikoa mingine.
 
Mtwara wamedanganywa kwa muda mrefu , na hata kwa hili la gesi mpaka sasa , kuna kila dalili wameshatekenyeka ,
kuwa na wasomi wachache wenye weledi na kukosa viongozi wazalendo na wanaoupenda mkoa wao ni tatizo kubwa la
watu wa Mtwara kwa sasa. Ukiangalia suala ambalo Mtwara wamelishupalia (UJENZI WA BOMBA LA GESI ), mpaka sasa
serikali imepiga propaganda kubwa , na JK amehitimisha kabisa kwa kuwalaghai watu wa Mtwara kwa ahadi nyingi wakati ujenzi wa bomba la gesi unaendelea .
Kama kweli serikali inaamini inachofanya ni sahihi , kwa nini wanishindwa kuwaambia watu wa Mtwara kwa uwazi bila kuficha kuficha maneno kwamba ujenzi wa bomba la gesi kwenda Kisarawe utaendelea ila nyie 'tutawajengea' viwanda

Uzalendo wa Nkapa kwa wana mtwara uko chini sana nahisi kwa vile ameoa uchagani nguvu ya kuelekea Mtwara haipo
 
Back
Top Bottom