Mtunza bustani ashtakiwa kwa kumtusi Magufuli, kwamba anaendesha nchi kinyume na maumbile

Mtunza bustani jijini Dar es Salaam amefikishwa kizimbani jana kwa tuhuma za kumtusi rais Magufuli na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu.

Taarifa zinaripoti kuwa akiwa maeneo ya Leaders club mtunza bustani huyo aliwatusi rais na makamu wake kwa kuwatuhumu kwamba wanaongoza nchi kinyume na maumbile

My Take:

Jamani tujizuie kumtusi kiongozi wetu, lakini pia kamata kamata ya polisi inawatia hamu watu kuzidi kutukana. Maana toka watu waanze kukamatwa matusi mapya ndio kwanza yanazidi
Afungwe tu.
 
Huyo jamaa ni mwanafasihi.. Fasihi huwa inatumia lugha ya picha ambayo kila mtu anakuwa na tafsiri yake... Hiyo kesi hata bila wakili jamaa anashinda, labda dola ndo iamue na si mahakama...
 
Ngoja tusubiri mwendesha mashtaka wa serikali na wakili upande wa mtuhumiwa watatupa tafsiri gani mbele ya Mahakama na Hakimu atakubaliana na tafsiri ipi.

Mifano mingi mmojawapo kiongozi akisema ''nitawanyoosha'' wa-Tanzania ! Kufuatana na maumbile ya kibinadamu mtu mzima mwenye akili zake kuambiwa ''atanyooshwa'' hatakuwa radhi kukubali kimawazo anaweza kuambiwa hivyo na binadamu mwenzie na atabaki anasoneneka.
Unarukaruka tu kama maharage kwenye sufuria mwisho kuiva tu. Badala ya kumchangia apate mawakili wazuri unahangaika na justification za ajabu ajabu hapa.
 
Ha haaa haaaa kinyume na maumbile! khaaa watu wanavituko sana!
Ushauri wangu aachane na mambo mengine madogo madogo kwani kila siku linazaliwa tusi jipya! Tangu waanze kukamata mbona watu hawaogopi?
Kwahiyo waache kukamata? Majambazi wabakaji wauza madawa majangili n.k wameogopa na kuacha uhalifu wameanza kukamatwa lini? Kama kigezo ni makosa kuendelea basi mahakama zifungwe kwa sab makosa mengi yameanza kufanywa hata kabla ya uhuru
 
Ingekuwa kukamatwa na kupeleka mahakamanindio funzo la watu kutoendelea kutukana basi watu wangekuwa wamisha acha maana waliopelekwa mahakamani kwa kosa hilo ni wengi lakini bado watu wanaendelea kutokana-cha msingi mtukanwa ajirekebishe
Majambazi nao mbona wanaendelea?
 
Back
Top Bottom