Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,252
- 113,647
Hayo ni maneno aliyoyatamka Tundu Lissu juzi kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.
Mimi bado kabisa sijashawishika kuwa rais Magufuli anaendesha nchi kwa hiyo misingi.
Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na wengine wanaosema au kuona kuwa tokea rais huyu aingie madarakani kumekuwepo unyanyaswaji wa wanasiasa wa vyama vya upinzani.
Nakubaliana na wanaoona kuwa kumekuwepo na jitihada za kuminya uhuru wa vyombo vya habari.
Nakubaliana na wanaoona kuwa kwenye baadhi ya mambo, iwe kwa matendo au kauli zake, huyu rais kaonyesha tabia za kidikteta. Hili nimeshawahi kuliandika humu kwenye moja ya mada zangu za kumpinga huyu rais.
Nakubaliana kabisa na wanaohoji ujengwaji wa kiwanja cha ndege huko Chato ambako ndiko nyumbani kwa rais. Sioni sababu yoyote ile iliyo ya msingi kutumia mahela mengi kujenga kiwanja cha ndege huko. Ni heri hizo hela wangezitumia hata kununua madawati ya shule na kuziboresha shule na hospitali za huko na kwingineko. Lakini li kiwanja la ndege? Hapana kwa kweli.
Kwa kifupi ni kwamba, kuna mambo mengi tu ninayoyapinga kumhusu huyu rais. Vilevile, yapo mengi au kadhaa ninayokubaliana naye. Hii ni hali ya kawaida sana hususan kama mtu uko huru kifikra na si mtu wa kuburuzwa buruzwa tu kama zuzu.
Inapokuja kwenye hili suala la yeye kuendesha nchi kwa misingi ya kifamilia, kikabila, na kikanda, hapo bado kabisa sijashawishika na sikubaliani na wote wanaodai hivyo.
Tuangalie suala la kifamilia:
Kuna huyo Dotto James ambaye ni katibu mkuu kwenye wizara ya fedha na mipango. Pia, Lissu kamtaka mdogo wa huyo Dotto ambaye ndo naibu wa Dotto.
Hawa, inasemwa kuwa ni watoto wa dada wa Magufuli. Sina hakika kama ni dada kweli [yaani wa mama mmoja baba mmoja au mama/baba mbalimbali]. Magufuli ana dada?
Suala la kikabila na kikanda:
Hapa aliwataja Medard[spelling?] Kalemani ambaye ni naibu waziri wa wizara ya nishati na madini na ambaye pia aliwahi kuwa mwanasheria wa wizara hiyo hiyo. Huyu naye sijui ana undugu na Magufuli....[sasa hivi Magufuli baada ya kuwa rais atapata ndugu wengi sana].
Mkuu wa majeshi Jenerali Venance Mabeyo - anatokea kanda ya ziwa [ni Msukuma huyu]
Mkuu wa polisi, Kamanda Sirro - anatokea kanda ya ziwa [silijui kabila lake].
Mwanasheria mkuu, George Masaju - anatokea kanda ya ziwa [huyu naye hata silijui kabila lake na aliteuliwa kwanza kuwa mwanasheria mkuu na rais mstaafu Kikwete na kabakishwa na rais Magufuli].
Hivi Frederick Werema naye alikuwa anatokea kanda gani huyu? Hiyo hiyo ya ziwa?
Mwendesha mashtaka - Biswalo Mganga - naye anatokoea kanda ya ziwa [sijui hata yeye ni kabila gani ila naye najua aliteuliwa kuwa mkurugenzi na rais mstaafu Kikwete na mpaka sasa rais Magufuli kambakisha].
Kaimu Jaji Mkuu - Ibrahimu Hamisi Juma - naye anatokea kanda ya ziwa [sijui yeye ni kabila gani].
Hivyo ndo 'vizibiti' alivyovitaja huyo 'wakili msomi' katika kuonyesha kuwa rais anaendesha nchi kwa hiyo misingi.
Now let's get down to the nitty-gritty so we can separate the wheat from the chaff.
1] Serikali ya Tanzania ina watumishi wangapi?
2] Wangapi kati ya hao watumishi ni Wasukuma na/au wanatokea kanda ya ziwa?
3] Tokea Magufuli awe rais keshateua Wasukuma na/au watu wa kanda ya ziwa wangapi ukilinganisha na idadi ya makabila na/au watu wa kanda zingine?
4] Kulinganisha na marais wa awamu zilizopita, rais Magufuli kateua Wasukuma na/au watu wa kanda ya ziwa wangapi?
5] Rais Magufuli ananufaikaje na kuteua watu wa familia, kabila lake [Magu kwanza wala si Msukuma..], na ukanda atokao?
6] Hao Wasukuma walioteuliwa na Magufuli na hao wengine watokeao kanda ya ziwa ni wangapi kati ya hawana sifa za kushika hizo nyadhifa walizonazo? Jenerali Mabeyo hana sifa za kuwa mkuu wa majeshi? Kamanda Sirro hana sifa za kuwa mkuu wa polisi? Biswalo Mganga hana sifa za kuwa mkurugenzi wa mashitaka? George Masaju hana sifa za kuwa mwanasheria mkuu? Hawa wawili wa mwisho waliteuliwa na rais Kikwete, btw.
7] Mnaoshadadia hiyo hoja ya ukabila na ukanda, ili msilalamike, mlitaka wawepo Wasukuma na watu wa kanda ya ziwa wangapi kwenye serikali ya Magufuli?
Katika hoja zote dhidi ya urais wa Magufuli hii ya ukabila, ukanda, na kwa kiasi fulani Ukatoliki ndo hoja dhaifu kuliko zote.
Mpaka hapo mtapokuja na takwimu madhubuti zinazothibitisha hayo mnayoyadai ndo labda mtapoeleweka.
Zaidi ya hapo hizo kelele ni sawa na tapatapa za mfa maji tu. Mfa maji atang'ang'ania chochote kile kilicho mbele yake kwa matumaini ya kwamba labda kinaweza kumwokoa asife maji.
Jumatano njema.