Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Mtume Mwamposa na jaribu la imani

Huo wa Bonnke nimeshajibu, ni mojawapo ya mifano duni mno. Nani hajui kikutano ya Bonnke ilikuwa ikilindwa na dola? Kwa nini polisi hawakuwepo hapo kwa Mwamposa?

Halafu hilo la bila kufunga mikanda, nani alikuambia wanaofunga mikanda wote hawafi? Pia iweje safari ianze bila polisi anayepaswa kuwepo kukagua mikanda kufanya hivyo? Pia muda wa kusafiri ukiisha polisi huzuia magaro yasiendelee na safari mapaka kesho yake, unaweza kueleza kwa nini haikufanyika hivyo?

Tatiza hamuelewi msingi wa mada. Sikuanzisha kupima kama Mwamposa yuko sahihi kutumia mafuta ama la, mimi naangalia chanzo halisi cha vifo ili kuondoa kauli ya waziri kwamba WAHUBIRI WAWE NA DIGRII MBILI. Kwamba hizo digrii zingezuia vifo? Kwamba hawa watumishi wasio na digrii iweje wawe na wafuasi maprofesa? Basi tuna haja ya kuupitia upya mfumo wetu wa elimu kwa sabau unazalisha wasomi wajinga!!

Elewa mada ujikite kwenye mada, mimi siko kwenye imani ya mafuta, naongelea chanzo cha vifo.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Kwa hiyo mkuu kama tukiweka imani pembeni chanzo cha kifo mimi na wewe na mtu yeyote humu hawezi kuwa sahihi,kama utasisitiza kwenye chanzo cha kifo mimi naona tusubilie ripoti ya madaktari kwakila mmoja aliyekufa.Ni Doctor pekee ndiye anaweza kusema chanzo cha kifo ni nini,sisi tunaweza sema walingukiana kumbe postmortem ikaonyesha kitu kingine.Sijui kama umenielewa?
 
Kilichofanyika kwenye ibada ya mwamposa,ni ushetani tu,hata utetee vp,hata wakatoriki tuna utaratibu wa kula mikate,na divai lakini hatukanyagani,na kuuana kama mang'ombe,kushiriki meza ya bwana,kama tunavyoita,ni utaratibu uliowekwa wazi,kwa kila muumini,

Ndugu, nani alikwambia hii ilikuwa meza ya Bwana? Ni vema ukajielimisha kwanza kuhusu tukio zima kabla ya kukurupuka. Pia ni wapi nilipoongelea uhalali wa ibada ya kukanyaga mafuta? Umekurupuka vibaya, soma tena uelewe lengo hasa la mada hii.

Anachofanya mwamposa,na wanaomfanana,ni kutafuta umaarufu,na pesa,wanauzia watu maji ya Tsh 500,kwa Tsh 10000,eti utapata baraka,wanakupa picha zao,uweke kwenye mlango wako nyumbani,eti utapata ulinzi,wakati huyo "nabii" anama body guard kumi,nyumba inampaka fensi za umeme,
Acha kutetea ujinga,

Mithali 26
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

Yaweza kuwa natetea ujinga, kama hicho ndicho ulichokielewa. Fine, lakini kwa sababu tumeagizwa na biblia kumjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake, wacha nikupe changamoto chache tu katika imani yako ya kikatoliki:

1. Mwamposa na wengine yaweza kuwa wanafanya biashara kweli kwa sababu karama na vipawa vya Mungu haviuzwi. Hebu nijibu hapa; umewahi kusikia habari ya kununua misa kwa ajili ya kuombea marehemu kwenye kanisa katoliki? Kwamba ukinunua misa ndugu yako marehemu anapunguziwa adhabu? Kwamba ili kuwa na uhakika wa kumkomboa nduguyo toka toharani yakupasa kuomba misa nyingi zaidi kwa sababu huna uhakika atateswa miaka mingapi?

2. Nijibu pia, je kule kuuza scapulari kwa maana ya kukulinda pale unapoivaa na nyingine zimeahidiwa kuwa ukifa umeivaa basi utakwenda moja kwa moja mbinguni. Hii sio biashara kwa jina la nguvu za Mungu?

3. Mauzo ya rosali yamepishana vipi na mauzo ya mafuta ya upako? Vyote hivyo haviwekwi daraja moja kwamba ukiumwa ukasali rozali autapona? Kwamba ukisali rozali utapata muujiza?

4. Je, kununua picha za bikira Maria na kuwa mnasali chini yake majumbani mwenu sio ibada sawa na kununua mafuta ukayaamini? Kwamba ziko picha kwa majira mbalimbali?

Yako mengi, ila nijibu katika hayo kwanza.

Mara ya mwisho,umesikia waumini wa kikatoriki,au lutheran,wamekanyagana,wakigombea meza ya bwana ni lini,hawa "manabii" wa sasa wameufanya ukristo kama biashara.
Ni majizi,tena majizi,tena majizi,

Sent using Jamii Forums mobile app

Kweli sijawahi kusikia wakatoliki wala walutheri wala waanglikani wakikumbwa na masahibu hayo. Ila hata kwa Mwamposa sijawahi kusikia hilo juu ya meza ya Bwana.

Kuhusu kuufanya ukristo biashara, basi jibidiishe ukasome kuhusu Banco Ambrosini na skendo za kanisa kwenye matumizi ya pesa. Usipende kukurupuka mkuu, usijihesabie haki hata kidogo.

Kama tatizo ni kufariki hao watu 20, nakiri hata mimi imeumia sana. Lakini yako maovu ya kuogofya zaidi huko kwa makasisi ambayo sipendi tuyajadili hapa kwani mtandao unaweza kuzima, nadhani umenielewa. Wako vijana maelfu wameharibiwa future zao, unawezaje kurusha mawe kwa nyumba ya jirani yako wakati kwako ni vioo juu chini?

Kama ni ushetani mbona ziko ibada za kishetani zimefanyika sana tu hapo St. Peters na ulimwengu unajua? Watu wamechinjwa kama kafara kuadhimisha black mass. Msome kasisi mwenye hofu ya Mungu Fr. Malachi Martins ujifunze zaidi uwe mweledi.

Kuhusu wizi nakushauri ukatazame upya huduma za kanisa mfano afya, elimu n.k. Utashangaa kuona kuwa huduma hizi ni ghali kuliko hata taasisi binafsi ambazo zinasimamiwa kwa misingi ya kibiashara.

Kumbe ni vema ukachunga sana kinywa chako na ukasome hoja na kuijadili kama ilivyo kuliko kuja na hasira zako.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Nabii ambaye ameshindwa hata kujua kwamba hili tukio litatokea,kwanini hakuoteshwa,tukio limetokea,akakimbilia Dar,watu wamekufa kanisani kwako,hata kubaki kutoa pole,wewe unakimbia unakimbilia Dar,kuogopa mikono ya polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Hawakufa kanisani kwake Kawe
2. Mungu hutenda apendavyo, sio utakavyo weww. Pia Mwamposa sio nabii
3. Mwamposa alikuwa mhubiri mwalikwa huko Moshi
4. Hakuwakimbia polisi. Wakati mchakato wa mafuta unaendelwa alikwenda aieport kuanza safari ya Dar kuwahi ibada ya jumapili. Huko nyuma majanga yakatokea

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Huo wa Bonnke nimeshajibu, ni mojawapo ya mifano duni mno. Nani hajui kikutano ya Bonnke ilikuwa ikilindwa na dola? Kwa nini polisi hawakuwepo hapo kwa Mwamposa?

Halafu hilo la bila kufunga mikanda, nani alikuambia wanaofunga mikanda wote hawafi? Pia iweje safari ianze bila polisi anayepaswa kuwepo kukagua mikanda kufanya hivyo? Pia muda wa kusafiri ukiisha polisi huzuia magaro yasiendelee na safari mapaka kesho yake, unaweza kueleza kwa nini haikufanyika hivyo?

Tatiza hamuelewi msingi wa mada. Sikuanzisha kupima kama Mwamposa yuko sahihi kutumia mafuta ama la, mimi naangalia chanzo halisi cha vifo ili kuondoa kauli ya waziri kwamba WAHUBIRI WAWE NA DIGRII MBILI. Kwamba hizo digrii zingezuia vifo? Kwamba hawa watumishi wasio na digrii iweje wawe na wafuasi maprofesa? Basi tuna haja ya kuupitia upya mfumo wetu wa elimu kwa sabau unazalisha wasomi wajinga!!

Elewa mada ujikite kwenye mada, mimi siko kwenye imani ya mafuta, naongelea chanzo cha vifo.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Brother napenda unaufahamu mkubwa sana,ROHO YA UFAHAMU iendelee kwa wingi ndani yako.shida ya wakristo tuliyonayo ndio hyo kwamba kila mtu anataka tuamini imani yake ndio sawa,wengine hawataki kuingia into detail ya tukio kwa sababu tu hawampendi mwamposa basi wanasema lolote.Nakuhusu ile kauli ya waziri baada ya kusikia ile kauli nikajua safari yake hata kwenye kile kiti cha uwaziri wa mambo ya ndani sio ndefu
 
Ndugu, nani alikwambia hii ilikuwa meza ya Bwana? Ni vema ukajielimisha kwanza kuhusu tukio zima kabla ya kukurupuka. Pia ni wapi nilipoongelea uhalali wa ibada ya kukanyaga mafuta? Umekurupuka vibaya, soma tena uelewe lengo hasa la mada hii.

Mithali 26
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

Yaweza kuwa natetea ujinga, kama hicho ndicho ulichokielewa. Fine, lakini kwa sababu tumeagizwa na biblia kumjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake, wacha nikupe changamoto chache tu katika imani yako ya kikatoliki:

1. Mwamposa na wengine yaweza kuwa wanafanya biashara kweli kwa sababu karama na vipawa vya Mungu haviuzwi. Hebu nijibu hapa; umewahi kusikia habari ya kununua misa kwa ajili ya kuombea marehemu kwenye kanisa katoliki? Kwamba ukinunua misa ndugu yako marehemu anapunguziwa adhabu? Kwamba ili kuwa na uhakika wa kumkomboa nduguyo toka toharani yakupasa kuomba misa nyingi zaidi kwa sababu huna uhakika atateswa miaka mingapi?

2. Nijibu pia, je kule kuuza scapulari kwa maana ya kukulinda pale unapoivaa na nyingine zimeahidiwa kuwa ukifa umeivaa basi utakwenda moja kwa moja mbinguni. Hii sio biashara kwa jina la nguvu za Mungu?

3. Mauzo ya rosali yamepishana vipi na mauzo ya mafuta ya upako? Vyote hivyo haviwekwi daraja moja kwamba ukiumwa ukasali rozali autapona? Kwamba ukisali rozali utapata muujiza?

4. Je, kununua picha za bikira Maria na kuwa mnasali chini yake majumbani mwenu sio ibada sawa na kununua mafuta ukayaamini? Kwamba ziko picha kwa majira mbalimbali?

Yako mengi, ila nijibu katika hayo kwanza.

Kweli sijawahi kusikia wakatoliki wala walutheri wala waanglikani wakikumbwa na masahibu hayo. Ila hata kwa Mwamposa sijawahi kusikia hilo juu ya meza ya Bwana.

Kuhusu kuufanya ukristo biashara, basi jibidiishe ukasome kuhusu Banco Ambrosini na skendo za kanisa kwenye matumizi ya pesa. Usipende kukurupuka mkuu, usijihesabie haki hata kidogo.

Kama tatizo ni kufariki hao watu 20, nakiri hata mimi imeumia sana. Lakini yako maovu ya kuogofya zaidi huko kwa makasisi ambayo sipendi tuyajadili hapa kwani mtandao unaweza kuzima, nadhani umenielewa. Wako vijana maelfu wameharibiwa future zao, unawezaje kurusha mawe kwa nyumba ya jirani yako wakati kwako ni vioo juu chini?

Kama ni ushetani mbona ziko ibada za kishetani zimefanyika sana tu hapo St. Peters na ulimwengu unajua? Watu wamechinjwa kama kafara kuadhimisha black mass. Msome kasisi mwenye hofu ya Mungu Fr. Malachi Martins ujifunze zaidi uwe mweledi.

Kuhusu wizi nakushauri ukatazame upya huduma za kanisa mfano afya, elimu n.k. Utashangaa kuona kuwa huduma hizi ni ghali kuliko hata taasisi binafsi ambazo zinasimamiwa kwa misingi ya kibiashara.

Kumbe ni vema ukachunga sana kinywa chako na ukasome hoja na kuijadili kama ilivyo kuliko kuja na hasira zako.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Ur deep
 
Nimekuelewa vizuri,na umenijibu vizuri na nimekufahamu kwa kisasi kuliko post yako ya kwanza ilivyokaa.Sasa kuhusu uhalali wa mafuta umesema siyo mada,niliheshimu hilo.
Lakini sijui kama umefika kwenye level ya ukimsikiliza mtumishi fulani kwa muda yanakuwepo mawasiliano na unashuhudiwa na Roho ya kuwa huyu anachofundisha ni kweli ingawa sikatai ya kwamba anaweza kukengeuka mbele ya safari.
Ukisikiliza video za walionusulika wanasema mambo yalikuwa safi ila walipoanza kukanyaga mfuta ndiyo shida ikatokea,nielewe nilipoandika Mungu muda mwingine huongea na wanadamu ila hushindwa kumwelewa.
Niliposema issue ya Mwamposa yule mtumishi wa Mwanza (Malisa) ameilinganisha na Ayubu pale hakutumia maandiko kwa usahihi kwa sababu Ayubu alipoteza watoto wake wa damu na mali zake hapo Kilimanjaro Mwamposa hajapoteza watoto wake wa damu au mali zeke kama ambavyo Ayubu alipoteza.Nilitaka upate picha ambavyo muda mwingine Neno la Mungu linatumiwa vibaya.Sikumanisha lile siyo jaribu kwake,na kama tunaliita jaribu kama ulivyosema ,je maandiko yanasemaje kuhusu majaribu kama ulivyoliita?Je Mungu humjaribu mtu au shetani?Au tamaa zake mwenyewe?
Kuna swali mitume na manabii wengi hawapendi kuulizwa?Swali hili ni muhimu kwa kila anayejiita mtumishi wa Mungu ajue majibu yake.

Mathayo 16:13-17

":13 Yesu alipofika pande za Kaisarea Filipi, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasema Mwana wa Mtu kuwa ni nani?” 14 Wakamjibu, “Wengine wanasema kuwa ni Yohane mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.” 15 Yesu akawauliza, “Na ninyi je, mwasema mimi ni nani?” 16 Simoni Petro akajibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” 17 Yesu akasema, “Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana si binadamu aliyekufunulia ukweli huu, ila Baba yangu aliye mbinguni. "

Leo kwa mfano useme jina la mtumishi fulani wa Mungu,watu watakuambia huyo ni tapeli,huyo ni mwizi.
Je watanzania wanasema Mwamposa ni nani?Yesu tofauti na watumishi wa siku hizi alikuwa tayari kujua watu wanasema yeye ni nani,kama angekuwa Yesu ni tapeli tungeambiwa lakini walisema ni Eliya,wengine Yohana mbatizaji etc,baada ya kupata majibu ya watu wa nje,akawauliza wafuasi wake.Simoni Petro akapatia,ya kuwa Yesu ni Kristo.Heri wewe Simoni mwana wa Yona, kwa maana si binadamu aliyekufunulia ukweli huu, ila Baba yangu aliye mbinguni. ,sasa unasemaje wewe binafsi juu ya watumishi ambao watu wanasema ni matapeli,wapiga madili?Je tuyapuuze majibu ya hawa watu ikiwa Yesu mwenyewe alitaka kujua watu wanamsemaje sisi tunaojiita watumishi hili eneo hatutaki kusikia watu wanasemaje?Something is not right somewhere. Nakubaliana na uliyoandika ila nimalize kwa kuwaonywa wakristo hizi ni nyakati za hatari,kuwa makini na mahali unapoabudu,tumia muda wako kujifunza Neno la Mungu kwani ni taa na litakuponya.

Niliposema baba zao wa kiroho tunaweza kuwajua?Sikuwa na maana kama baba zao wako sahihi au hawako sahihi,lengo langu ni tujue chanzo cha imani hizo ,tujue lini mafuta yalianza,na nani alianza kuwapa watu mafuta.
Mimi sijafuatilia kujua Mwamposa historia yake ,lakini wengine kama Prophet Shillah atakuambia baba yake ni prophet Bushiri,sasa kama kuna mwingine baba yake ni TB Joshua watu wanaojua watujuze.Ukijua baba yake ni rahisi kujua mtoto alivyo amejifunza wapi.
Nakubaliana na wewe ya kwamba Roho mtakatifu ndiyo mwalimu sahihi,na ni kweli maandiko yanataka tuongozwe kwa Roho,lakini kabla huyo Roho hajakuongoza si kuna mtu alikufundisha Neno,si Kuna mtu alikuongoza sara ya Toba,si kuna mtu alikuchunga na kukulea katika mambo ya imani huyo ndiyo nilimanisha.Tukijua imani yake ilivyo tutajua kama ni sahihi au si sahihi kwa kutumia maandiko.
Taifa la Nigeria mambo ya dini yameleta shida sana,mpaka kuna kipindi watoto wadogo walikuwa wanatuhumiwa uchawi,kwa hiyo matangazo ya wanaojiita watumishi wa Mungu yakabadilika wanakuambia "tunanguvu za kuwashinda wachawi,njoo kwetu".
Hata kama lengo lako ni chanzo cha vifo lakini kumbuka ni nani anaweza kumfanya mtu afe kwa sababu yoyote ile.Na niliposema polisi tusiwalaumu,naomba unielewe na najua wewe unajua ya kwamba "mambo yote huanza katika ulimwengu wa Roho na baadaye kutokea katika ulimwengu wa mwili" kwa hiyo hata hivyo vifo vilianza katika ulimwengu wa Roho,polisi yeye mambo ya Rohoni hawezi kuyazuia ndiyo maana huwezi peleka polisi kezi ya kulogwa.Wewe unachofanya unaongea kama mtu unayeijua kweli na pengine unaweka kweli pembeni na kuongea katika utaratibu wa kawaida wa maisha.Ombi langu kwako unganisha knowledge yako kwenye spiritual issue na physical kisha toa maoni yako ili watu wapone.Hapa tunataka watu wapone,unajua kuna watu hata Mungu akiongea hawaelewi?Kuna Mchungaji alikutwa amelewa chakali video zikasambaa lakini bado wafuasi hawaelewi hata Mungu anapofunua yaliyo sirini.Kuna muda wa kuwaombea watu na kuna muda wa kuwaonya na kuwaambia yawapayo kutenda.
kanisa la Mungu limeingiliwa pale tunapoweza kusema hatutakiwi kukaa kimya,Kunaandiko agano la kale sikumbuki mstari lakini linaeleza kitu kama "je mambo haya yalikuwepo enzi za babu zenu?"Mambo ya mafuta ya upako je yalikuwepo miaka ya 80,90?Hapa watumishi hujitetea kwa kusema wamefunuliwa na Roho Mtakatifu na tena watakuletea na mistari kussuport,kuna mtu amesema sikumbuki kama ni wewe ya kwamba Yesu aliponya mtu kwa mate.Ni kweli lakini Yesu alikuwa na njia nyingi,na alipoondoka alituambia tuombe lolote kwa jina lake.Unataka watu wafunguliwe,omba kwa jina la Yesu,unataka mtu apone omba kwa Jina la Yesu,sasa siku hizi hizi technologia wanatudanganya wameombea mafuta kisha mafuta yatatuponya.Hapo watu wanaondolewa taratibu katika kumtegemea Mungu wanaenda kwenye vitu.Hii ni sawa na mkristo anayecheza kamali taratibu anaanza kutegemea nguvu ya buku badala ya Mungu.Sikatai ya kwamba kuna mafunuo lakini mafunuo ni kitu cha kutumiwa sehemu fulani kwa kadri ambavyo Roho wa Mungu ameona lakini haimanishi ni fundisho.Namanisha kama wewe Mungu ulipokuwa unamwombea mtu fulani,Mungu akakufunulia ombea maji kisha mpe anywe na yule mtu baada ya kunywa akapona.Hii haimanishi kila mgonjwa uombee maji umpe anye.Tunahitaji kuongozwa na Roho Mtakatifu.kama kuna mtu alifunuliwa mafuta basi haikutakiwa kuwa katikakila jambo.Yesu mwenyewe kuna wengine hata hakuwaombea,aliwaambia tu "imani yako imekuponya".Kwa hiyo njia za kupokea uponyaji au muujiza ni nyingi lakini njio yoyote ikitumika inatakiwa isiwe kinyume na neno la Mungu na kama njia hiyo inatoka kwa Mungu aliye wa kweli italeta amani kwa watumishi wengine ila kama haitoki kwa Mungu wa kweli friction itakuwepo.Na kwa nini wanaotuhumiwa hawaziachi hizo njia na kutumia jina la Yesu?Jina laYesu ili litende kazi kuna jinsi ambavyo anayelitumia anatakiwa kuwa si kila mtu,ndiyo maana wale watoto waliwaiga wanafunzi wa Yesu wakayaamulu mapepo yatoke,yakwaambia Yesu tunamju na Paulo tunamju,yakawapiga.Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote ambaye atakuwa tayari kutii na kufuata maagizo ya Mungu.
Ni kweli doctrine zinaweza kutofautia lakini kuna yale mafundisho ya msingi,biblia ndiyo msingi wetu.Roho Mtakatifu ni mzuri hutufundisha.Yesu aliwaambia wanafunziwake watakuwa mashahidia kuanzia uyahudi,samaria mpaka mwisho wa nchi,injili ya mfuta ya upako,chumvi ya upako etc haikubaliki kwenye maeneo mengi ya dunia hii inaifanya isiye injili ya kweli kwani kuna maeneo haipokelewi siyo na wapagani,haipokelewi na watumishi wa Mungu,kwa sababu ina ukakasi ndani yake.Mwenye masikio na asikie.
Hawa jamaa ambao ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo wana network kubwa,na kwa sababu wanawatu wengi tunakoelekea na kwa kuwa ni unabii unatimia watawapata wengi yamkini hata wateule kama ambavyo maandiko yanasema.
Watumishi wa siku hizi wengi waovijana wanapenda publicity,wanapenda kutabiri hata kwenye mambo ambayo yanaonekana wazi.
Mo alivyopotea,kuna watumishi wanakuambia "mimi pekee ndiyo niltabiri kuwa atapatikana siku ya Ijumaa " wakati huo kuna wenzake naye anasema mimi pekee(hapa unajua hapo kuna shida,Roho hapingani).Sasa hapo hata kwa akili ya kibinadamu unaona kuna shida.
Tusome bibilia zetu,tumwombe Roho Mtakatifu atufundishe na tuache unafiki wa kuingia makanisani na wakati huo huo tunaiba,tunasema uongo,tuko fiesta na kwenye singeli hapo utakuwa unapoteza muda wako.Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu atamhukumu kila mtu sawasawa na matendo yake.
Mnaojiita watumishi wa Mungu mnatakiwa mjue watu wanasema wewe ni nani na usipuuze majibu yao.Kama wakikuita wewe ni mwizi,tapeli etc basi angalia umekosa wapi,fanya toba na umwombe Mungu akusaidie,tukumbuke hao watu pia wameumbwa kwa mfano wa Mungu.

Unahitaji kumpokea Yesu leo?Njoo inbox

Kimsingi nakushukuru kwa andiko lako lenye kufunza na kuonya. Naomba niweke maoni yangu sehemu moja tu, hapo kwenye andiko ulilonukuu MATHAYO 16:13-17. Mimi napenda kuyachunguza maandiko kuona kweli yake, lakini nnakubali wakati mwingine huwa najifunza zaidi kwa wengine pia.

Yesu aliposema damu na nyama hazikumfunulia Petro, alimaanisha huo ushuhuda haukutoka kwa wanadamu, wala katika hali yake ya kibinadamu. Nina ujasiri katika hili kwa sababu Yesu mwenyewe alikataa kata kata kupokea ushuhuda wa wanadamu. Tusome:

Yohana 5
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
Yohana 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³¹ Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
³² Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.

Hii ni standard aliyoweka Yesu ambayo wengi tumeikanyaga kabisa. Hakuna kujihesabia haki mbele za Mungu kwa sababu hatupaswi kujisifu wenyewe hata mbele ya wanadamu wenzetu.

³³ Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli.
³⁴ Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.

Standard nyingine ni kupokea ama kutafuta ushuhuda wa wanadamu wenzetu watusifie. Tunatafuta kukubalika na wanadamu lakini tunakatalowa na Mungu. Kumbuka mambo yote yafanyike sirini, tusikae na kupiga panda kwenye njiapanda ili watu watusifu. Tuwahubirie watu waokoke wala si kutaka kusiwfiwa na wao. Hata Yesu alikataliwa na hata kuuawa na hao hao ambao baadaye Simon Petro aliwashuhudia.

³⁶ Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkubwa kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma.
³⁷ Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.

Sasa Kristo ana ushuhuda mkubwa zaidi. Yeye ametupa sisi huo ushuhuda kwa sababu akaa ndani yetu. Kumbe basi hata sisi haitupasi kupokea ushuhuda wa wanadamu. Kitakachotushuhudia ni kazi alizotupa Baba (sio tunazompa Yeye kutaka azifanye), hizo ndizo tukizitenda zitajenga ushuhuda. Ndio matunda ambayo yatupasa kutambuliwa kwayo. Kwamba hizo kazi zikiwa zinamshuhudia Mungu ndipo itaonekana Yeye ndiye aliyetutuma sisi. Kama kazi zetu zitatushuhudia sisi wenyewe kama ilivyo hii leo, basi ushuhuda wetu ni wa wanadamu na ni wa uongo.

Halafu Baba naye atushuhudia kwamba tu watenda kazi shambani mwake.

⁴¹ Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu.
⁴² Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.
⁴³ Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
⁴⁴ Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?

Ni vibaya kutafuta utukufu wa wanadamu, kwani hao ndio hutupa kiburi na majivuno. Wanadamu huweka daraja kwa kadri nya matakwa yao. Ndio maana leo hii kuna wahubiri wakubwa na wadogo, wenye Mungu mwenye nguvu na wenye Mungu dhaifu.

Kwa hiyo Yesu aliposema damu na nyama hazikufunua huo ushuhuda, alikusudia kuwa umetoka kwa Baba. Hakuna hata mara moja Yesu alitafuta ushuhuda wa wanadamu. Ndio sababu pia hakuna mahali amesema moja kwa moja kuwa MIMI NI MUNGU kwa sababu amesema haipaswi kujishuhudia mwenyewe.

Watu hupata taabu pale wanapoulizwa, "ni wapi Yesu amesema MIMI NI MUNGU?" Kuanzia leo ndugu zangu katika Bwana, msitaabishwe na maswali ya namna hii. Kristo alishasema hajishuhudii mwenyewe, atakaye kuujua uungu wake na atazame kazi zake. Ndivyo itupasavyo sisi pia, kazi zetu na zitushuhudie, hakika watu watasema huyu ni mtumishi wa Mungu kwa ushuhuda wa mbinguni (Roho Mtakatifu).

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Nimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.

Chanzo cha vifo ni kipi hasa?

Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.

1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.

2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.

3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.

Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.

Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.

4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.

Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.

Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.

Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.

Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
.. Tapeli amekutuma uje umsafishe au sio, mapumbavu kama wewe nawaangaliaga nabaki hiiiiiiii, janjaruka mjinga mkubwa wewe.
 
Kwa hiyo mkuu kama tukiweka imani pembeni chanzo cha kifo mimi na wewe na mtu yeyote humu hawezi kuwa sahihi,kama utasisitiza kwenye chanzo cha kifo mimi naona tusubilie ripoti ya madaktari kwakila mmoja aliyekufa.Ni Doctor pekee ndiye anaweza kusema chanzo cha kifo ni nini,sisi tunaweza sema walingukiana kumbe postmortem ikaonyesha kitu kingine.Sijui kama umenielewa?

Umeanza kuongea pumba,embu acha wenye kitu cha kuongea waseme tuwasikilize “unataka ripoti gani wakati wametangaza sababu ni kukanyagana”
 
Umesahau BABU wa LOLIONDO na kikombe cha plastic na maji taka; ni Mlutheri yule. Hatumfahamu Mungu kwa madigirii/PHD etc.; wasingekuwa walevi, wavuta sigara wazinzi, wapigadili wa kawaida dhambi lukuki. Neno la Mungu ni ROHO na linatambulikana kwa ROHO mtakatifu sio kwenda shule za kidunia. Yako makanisa yanayofundisha kweli yote ya biblia na Mcchungaji anajua kusoma na kuandika tu. Hawa wamepita chuo gani?; Mwakasege, Mzee Kulola(RIP)
Ofcourse una point
Ila tafadhali mtumishi wetu Mwl.Mwakasege ana degree ya Uchumi..kichwa kile yuko vizuri sana
 
Ndugu, nani alikwambia hii ilikuwa meza ya Bwana? Ni vema ukajielimisha kwanza kuhusu tukio zima kabla ya kukurupuka. Pia ni wapi nilipoongelea uhalali wa ibada ya kukanyaga mafuta? Umekurupuka vibaya, soma tena uelewe lengo hasa la mada hii.

Mithali 26
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁵ Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

Yaweza kuwa natetea ujinga, kama hicho ndicho ulichokielewa. Fine, lakini kwa sababu tumeagizwa na biblia kumjibu mpumbavu sawa sawa na upumbavu wake, wacha nikupe changamoto chache tu katika imani yako ya kikatoliki:

1. Mwamposa na wengine yaweza kuwa wanafanya biashara kweli kwa sababu karama na vipawa vya Mungu haviuzwi. Hebu nijibu hapa; umewahi kusikia habari ya kununua misa kwa ajili ya kuombea marehemu kwenye kanisa katoliki? Kwamba ukinunua misa ndugu yako marehemu anapunguziwa adhabu? Kwamba ili kuwa na uhakika wa kumkomboa nduguyo toka toharani yakupasa kuomba misa nyingi zaidi kwa sababu huna uhakika atateswa miaka mingapi?

2. Nijibu pia, je kule kuuza scapulari kwa maana ya kukulinda pale unapoivaa na nyingine zimeahidiwa kuwa ukifa umeivaa basi utakwenda moja kwa moja mbinguni. Hii sio biashara kwa jina la nguvu za Mungu?

3. Mauzo ya rosali yamepishana vipi na mauzo ya mafuta ya upako? Vyote hivyo haviwekwi daraja moja kwamba ukiumwa ukasali rozali autapona? Kwamba ukisali rozali utapata muujiza?

4. Je, kununua picha za bikira Maria na kuwa mnasali chini yake majumbani mwenu sio ibada sawa na kununua mafuta ukayaamini? Kwamba ziko picha kwa majira mbalimbali?

Yako mengi, ila nijibu katika hayo kwanza.

Kweli sijawahi kusikia wakatoliki wala walutheri wala waanglikani wakikumbwa na masahibu hayo. Ila hata kwa Mwamposa sijawahi kusikia hilo juu ya meza ya Bwana.

Kuhusu kuufanya ukristo biashara, basi jibidiishe ukasome kuhusu Banco Ambrosini na skendo za kanisa kwenye matumizi ya pesa. Usipende kukurupuka mkuu, usijihesabie haki hata kidogo.

Kama tatizo ni kufariki hao watu 20, nakiri hata mimi imeumia sana. Lakini yako maovu ya kuogofya zaidi huko kwa makasisi ambayo sipendi tuyajadili hapa kwani mtandao unaweza kuzima, nadhani umenielewa. Wako vijana maelfu wameharibiwa future zao, unawezaje kurusha mawe kwa nyumba ya jirani yako wakati kwako ni vioo juu chini?

Kama ni ushetani mbona ziko ibada za kishetani zimefanyika sana tu hapo St. Peters na ulimwengu unajua? Watu wamechinjwa kama kafara kuadhimisha black mass. Msome kasisi mwenye hofu ya Mungu Fr. Malachi Martins ujifunze zaidi uwe mweledi.

Kuhusu wizi nakushauri ukatazame upya huduma za kanisa mfano afya, elimu n.k. Utashangaa kuona kuwa huduma hizi ni ghali kuliko hata taasisi binafsi ambazo zinasimamiwa kwa misingi ya kibiashara.

Kumbe ni vema ukachunga sana kinywa chako na ukasome hoja na kuijadili kama ilivyo kuliko kuja na hasira zako.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
DUUUUU!
 
Mungu ana namna yake ya kuwaumbua matapeli na ndivyo alivyoumbuka huyu tapeli mkubwa.
 
Kuna mwanangu tulikuwa tunakunywa nae fungi vibaya mno eti Siku ni nabii huko mbeya juzi kanitembelea Dom tumekata kilaji mbaya afu ananambia eti ni amekuja kutoa huduma za kinabii Dom maana tangu limekuwa jiji fursa kibao😂😂😂
 
Iman ya katoliki sio iman ya bibilia so kila mtu haeshimu imani yake

Ni sawa kumbuka chimbuko la imani ya waprotestant imezaliwa ndani ya kanisa katoliki na hapo ndipo ninapowaonaga wapotestant mnapuyanga ila sio kosa lenu ni hao mitume na manabii wenu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nimekuwa nikitafakari kile kinachoendelea kufuatia tukio la vifo vya watu 20 vilivyotokea huko Moshi kwenye kongamano la Mtume Boniface Mwamposa "Bulldozer." Baada ya tukio hilo kumekuwa na maoni mengi na mitazamo tofauti kwa ujumla kutokana na jinsi ukio hilo lilivyotokea, nami nimeona nitoe mtazamo wangu juu ya jambo hili.

Chanzo cha vifo ni kipi hasa?

Hapa nimeona nichambue kwa kina tatizo hasa ni nini. Kumekuwa na mitazamo hasi kuhusiana na chanzo hasa cha vifo kiasi kwamba kumekuww na hasira kali juu ya imani ya baadhi ya watu.

1. Je vifo vimetokana na mafuta?
Ukitafakari kwa kina utaona hili si kweli. Mafuta hayakusababisha hivyo vifo kwa sababu hayuko hata mmoja aliyetumia mafuta hayo na kufariki. Mafuta hayo yamekuwa yakikanyagwa mara nyingi, kwa miaka mingi pasipo kuwa na madhara kwa watumiaji.

2. Je vifo vimesababishwa na mafundisho?
Ni muhimu kupima mafundisho kama ndio chanzo hasa cha vifo hivi. Kwamba kile kilichohubiriwa siku hiyo ndicho kilichopelekea watu kukanyagana hata vifo kutokea. Kama siku hiyo waliambiwa watakuokuwa wa kwanza kukanyaga mafuta watapokea upako kiasi cha kuwalazimu waamini kugombania nafasi ya kwanza basi hilo ni tatizo. Lakini kama fundisho lilikuwa ni kwamba kukanyaga mafuta tu ni kupokea baraka, basi haijalishi kama ni wa kwanza ama ni wa mwisho.

3. Je vifo vimesababishwa na mafundisho potofu?
Hili ni suala pana kwa sababu limelenga mambo ya kiimani. Nilishangaa jana pale nilipomsikiliza waziri Simbachawene akielezea jinsi ambavyo huwa anaangalia baadhi ya mafundisho na kujiuliza kama kuna Mungu pale. Siamini kama ni jukumu la waziri kupima wapi pana Mungu wa kweli na wapi hapana Mungu.

Mwenye jukumu la kupima usahihi wa mafundisho ni nani hasa linapokuja suala la imani? Nimesikia hoja yabkuwa na wahubiri wenye digrii ya teolojia. Je, ni sehemu gani kwenye Biblia ambapo Yesu alianzisha chuo cha teolojia ama kuagiza kianzishwe? Teolojia ni elimu ya kimfafanua Mungu KWA MTAZAMO WA ANAYEFUNDISHA. Hili ni tatizo. Tukifika hapo itabidi waprotestanti, wasabato, wakatoliki, moraviani, waanglikana na walutheri wakalishwe chini kuamua mafundisho yapi ni ya Mungu wa kweli. Itabidi tuamue teolojia ipi ni ya kweli na ndiyo hasa anayoikubali Mwenyezi Mungu.

Labda tujiulize mafundisho potofu ni nini? Hapo ndipo penye mgogoro na si vinginevyo. Sisemi haya kutetea mambo ya mafuta na maji ya upako, hasha. Nasema kwa sababu naona suala hili linachukua mkondo wa kidunia zaidi, kumpima Mungu kwa elimu ya kidunia wakati kumbe elimi ya Mungu wala haichangamani na hiyo.

4. Je, vifo vimesababishwa na usimamizi mbovu?
Nadhani hapa ndipo penye tatizo. Kilichotokea ni wazi kuwa ni usimamizi mbovu, ama uzembe kwenye kusimamia uendeshaji wa tukio la kukanyaga mafuta. Habari ya kwa nini watu wanaamini katika mafuta haina uhusiano hata kidogo na vifo hivyo. Ni sawa na kuhoji kwa nini watu wanaamini katika mkate na divai, ama katika kuchoma udi n.k. Tatizo liko kwenye utaratibu wa waamini kukipata kile wanachokiaminia.

Mambo ya kiimani yanabaki kuwa juu ya mhusika mwenyewe, hivyo ni ujinga kumwona anayeamininhayo kuwa mjinga. Nikutafuta kuwaingizia wengine imani yako kwa lazima, hivyo kuondoa maana ya uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria. Kama sheria imevunjwa, sio sheria ya kukanyaga mafuta bali sheria ya kushindwa kusimamia kusanyiko kwa usalama.

Hivyo basi hoja yangu imelenga kuonyesha kuwa sio sahihi kuanza kushambulia imani ya watu kwa vigezo vya nini sisi wengine tunakiamini, bali yatupasa kuwafundisha uzuri wa imani zetu na ubaya wa imani yao ili waamini habari zetu waachane na hayo yao.

Ni makosa makubwa kuwaaminisha wau kuwa tukio la mwamposa inashabihiana na lile la Kibwetee wa Uganda. Hii ni namna ya kutafuta kushambulia imani nyingine kwa mgongo wa nyuma na ndipo hoja za wenye imani tofauti zilipojikita. Mpaka sasa sielewi ni kwa vipi tukio la Moshi limefanana na lile la Kibwetere. Ni uongo na uzushi mkubwa wa wenye kuishambulia imani.

Nawasihi utafakari kwa kina tatizo lilipo, tuachane na mihemkoa bali tuwe wakweli kwani kweli itatuweka huru.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Nakubaliana na hoja ya usimamizi kuwa ndio chanzo cha vifo kwenye mikusanyiko mingi sio ya kidini tu,Nakumbuka viliwahi kutokea vifo kwenye mapokezi ya Kakobe mwaka fulani,,mwaka Jana kuna vifo vilitokea kule Israeli kwenye Sherehe ya kidini ya Wayahudi nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom