Mtuhumiwa ampora bunduki askari, aua watu wawili, ajeruhi askari

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Watu wawili wamepoteza maisha na askari mmoja kujeruhiwa vibaya kutokana na shambulio la risasi kutoka kwa mtu ambaye alipora bunduki kutoka kwa askari polisi Jijini Cape Town Nchini Afrika Kusini.

Polisi wamesema aliyefanya matukio hayo ni mwanaume mwenye umri wa miaka 40 ambaye alifyatua risasi kadhaa baada ya kuimiliki silaha hiyo kwa muda.

Polisi walikuwa wamempeleka mshukiwa aliyehitaji matibabu katika Hospitali ya Somerset, karibu na V&A Waterfront, sehemu maarufu kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

Baada ya kumpora askari risasi alimfyatulia sehemu ya kichwani na kuua wagonjwa wawili waliokuwa karibu yake kabla ya askari wengine kuwahi na kumpora silaha.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na kesi za mauaji katika nchi ambazo hazipo katika vita

Mwaka jana takwimu za mauaji katika Jiji la Cape Town ndizo zilikuwa nyingi kuliko maeneo mengine yote nchini humo ikifuatiwa na Jiji la Johannesburg.

Source: Citizen Digital
 
Back
Top Bottom