Naona biashara ya mayai inazidi kudharaulika,
Nadhani ni vizuri unapoongea biashara kama uko serious uongee kwa kueleweka, yes bila shaka unaweza kupata mayai hata kwa chini ya bei hiyo inategemea mambo yafuatayo, na si kwa mayai tu nadhani hili jukwaa ni zuri kama tutaweza kulitumia kwa kufanya mambo ya maana, toa taarifa zifuatazo kama kweli unataka kufanya biashara:
1. Bidhaaa _ Mayai ya kuku? Kwale? Bata?
2. Tray ngapi kwa muda gani?
3. Mahali ulipo -
4. malipo yatafanyika vipi - terms of payment
5. kama kuna swala lolote kuhusu quality ya kitu unachotaka, yawe makubwa etc
6. Contact number and time
Nadhani ukianzia hapo utaweza kupata majibu yatakayokuwezesha kusonga mbele, maana kama wewe ni supplier pengine pi utatakiwa utoe taarifa huko katika muda fulani, kwa mfano kwa sasa huu mjadala wa biashara ndogo ya tray 100 kwa wili leo ni siku ya pili je huyo mteja bado anasubiri tu? mteja mwingine wa mayai ni Serena Hotel, anahitaji tray 270 kwa wiki, lakini hataki supply ya kukatika katika, nafahamu watu watatu waliojaribu hapo wameshindwa na bado mpaka hivi karibuni hakukua na mtu aliyepatikana. Pia kuna tender ya maparachichi kwa anayeweza ku supply atufahamishe, kwa sasa chakula kinalika sana mwenye shamba halali njaa, mimi nina ndimu na malimao kilo shs 5000, nina malimao pia,