Mtu wa kunisaidia kutrack simu

Mtu wa kunisaidia kutrack simu

john_thesmart

Senior Member
Joined
Jan 20, 2022
Posts
145
Reaction score
392
Simu yangu imepotea juzi kati. Nilikuwa nimeenda sehemu kupata chakula, na tangu wakati huo sijafanikiwa kuipata. Nikiangalia kupitia portal ya "Samsung Find My Mobile", kwa kuwa nilikuwa nimeSet kuweza kuifuatilia hata ikiwa offline, naona imekuwa ikionyesha maeneo fulani ambayo nayafahamu na ambayo hayako mbali sana na sehemu niliyokuwa nimeenda kula.

Tatizo ni kwamba mfumo hauonyeshi nyumba au eneo exactly ilipo simu. Simu bado ni mpya, hivyo nahitaji msaada wa mtu mwenye uzoefu wa kufuatilia na kutafuta simu ili tuweze kuipata.

Nitakuwa tayari kumpoza atakayenisaidia kuipata. Pia, tutakapompata mtu aliye nayo, atawajibika kulipa gharama nyingine kutokana na mazingira yanayoashiria kuwa simu iliibiwa badala ya kupotea kwa bahati mbaya.

Nipo Dar es Salaam.
 
polisi wana watu wao ila utoe hela

kama simu inazidi milioni au ina vitu vya thamani ifatilie
ila kama ni chini ya laki 6 achana nao
maana utaliwa ela za kutosha
Bora atafute watu mtaani tu,atawalipa ikipatikana siyo kuchunwa huku huna hata uhakika wa kuipata.

Sema issue ni kumface stranger umwambie,"naomba simu yangu"!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom