1. Niambie wewe basi, sababu ya shootings za unarmed blacks ni nini.
Sababu haipo moja tu na ndiyo maana hata Civil Rights Division ya Justice Department inayoongozwa na mama mweusi, Loreta Lynch na iliyokuwa inaongozwa na mtu mweusi mwingine, Eric Holder, ikifanya uchunguzi huwa inapendekeza no charges kwa officers involved na kwa wengine inapendekeza charges.
Mfano ni mauaji ya Michael Brown kule Ferguson, Missouri. Unadhani ni nani alifanya uchunguzi wa yale mauaji na matokeo yake yalikuwaje? Unaweza kunipa jibu au utakwepa?
Na yule polisi [Michael Slager] aliyemmiminia risasi za mgongo yule jamaa wa South Carolina [Walter Scott] unajua amekuwa charged na kosa gani?
Sasa sikatai, kwa sababu sababu zipo nyingi na tofauti tofauti na zingine zikiwemo ubaguzi wa rangi. Lakini kamwe huwezi kusema sababu zote ni ubaguzi wa rangi. If you do that you would not only be wrong but also downright disingenuous.
Au wewe bila hata uchunguzi, bila hata kusikia side of the story ya hao officers involved ushahitimisha kuwa ni ubaguzi wa rangi kuwa ndo sababu? You can't be serious.
2. Nitatafuta namna ya kukutumia hiyo ripoti. Na swala la kwamba inawezekana hiyo ripoti imeandikwa kisiasi, hata baadhi ya link ulizoweka hapa zinaonekana zimeegemea upande mmoja.
Ndiyo. Mwelekeo wa kisiasa upo hata kwenye hizo, hilo wala sikatai. Lakini licha ya mwelekeo wa kisiasa kuwepo, ukweli wa kwamba hao watu wameuliwa na polisi haufutiki. Kilichopo ni namna tu ambavyo ukweli huo unavyokuwa spun ku support upande wako.
Swali kwako, je, wewe unakubali kwamba hiyo ripoti yako imeaongezwa chumvi za kisiasa au unakataa?
Kuhusu uhalifu, kwa hiyo unataka kuniambia watu weusi wanapigwa risasi unarmed kwa sababu wanashukiwa ni wahalifu au wanaishi maeneo yaliyoshamiri kwa uhalifu?
Hapana, sijataka kukuambia hivyo.
Halafu, kwa taarifa yako tu [maana naona hujui], kuna mapolisi weusi wengi tu wanaowapiga risasi watu weusi na kuwaua. Hilo unalizungumziaje? Au hakuna mapolisi weusi Marekani wanaowaua watu weusi wasio na silaha? Hao nao ni wabaguzi?
3. Ni kweli tunajali yanayotokea marekani lakini pia na kwingineko. Mauaji yanayotokea India ya watu weusi tunayapigia kelele kila siku.
Ah wapi...kelele mmpigazo kuhusu weusi wanaouliwa India wala hazilingani na kelele mpigazo kuhusu Marekani.
India na Marekani wapi na wapi?