Mtu kupenda kuishi maisha yaliyo juu ya uwezo wake

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,936
3,958
Maisha ya maigizo yapo sana mitaani. Kwa mfano unakuta mtu yupo radhi anunue simu ya milioni moja ili tu aonekane na yeye ni class la juu. Au anunue gari ili watu wamuone ana gari,cha ajabu unakuta gari yenyewe ya mkopo. Tukubali maisha tuliyo nayo mana unapolazimisha mambo utajiumiza halafu mwisho wa siku unakosa vyote. Kama una mpenzi hana pesa komaeni mtafute wote ili hivyo unavyotamani uwe navyo uvipate mana siku hizi hata kama mtu kaolewa akihongwa kidogo tu anagawa penzi. Tumshukuru Mungu kwa maisha tuliyonayo,tusilazimishe.
 
Kama haujakopa katka maisha bado hujawa na maisha unayoyataman maishani mwako labda kama unafanyakaz za wiz na madeal
 
Kama haujakopa katka maisha bado hujawa na maisha unayoyataman maishani mwako labda kama unafanyakaz za wiz na madeal
Mkuu kukopa sikatai ni kitu kizuri..Nnachosemea hapa ni mtu kukopa ili kufurahisha watu na yeye aonekane ana kitu kumbe kiuhalisia hana.
 
Nakubaliana na we we kidogo mkuu lakn maisha yalivo kwa sasa ni ya kuforce ,na hao ni wengi sana tena sana , yupo jamaa ukimkuta na kigari chake utasema jamaa amewin life lakn nenda nyumban kwake sebleni mashimo, kapeti imechanika yaan maisha anayoishi nyumban hayalingan na personality yake njiani,
Mkuu kukopa sikatai ni kitu kizuri..Nnachosemea hapa ni mtu kukopa ili kufurahisha watu na yeye aonekane ana kitu kumbe kiuhalisia hana.
 
Mwingine anaweza fanya hivyo kujifurahisha yeye mwenyewe lakini binadamu mkajudge tofauti so si kila anaefanya hivo vitu ni kwa ajili ya kuwafurahisha wengine wengine wanafanya hivo because mioyo yao imeridhia kufanya hivo na si kwa ajili ya kufurahisha wengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom