Mtu kamili vs mtu nusu

Pyaar

JF-Expert Member
Feb 11, 2018
15,341
75,515
1.Mtu kamili.
Huyu ni yule afanyaye mambo yake kwa umakini, anakiamini kile anachotaka kukifanya/maamuzi anayotaka kuyaamua lakini kabla hajasonga mbele katika kutenda kile alichoamua anaruhusu mawazo ya watu ili kuthibitisha usahihi wa kitu/jambo taraji kufanyika.

2.Mtu nusu.
Huyu yeye kila kitu/jambo kwake ewala!
Anasimamia alichokiamua aidha chenye manufaa/kisicho na manufaa, kizuri/kibaya, Chenye kuleta furaha/huzuni, chenye kuleta mshikamano/utengano.

Kwa ufupi hashauriki, wala kuingiliwa maamuzi yake.

Katika uongozi nyanja zote kunatakiwa kuwe na viongozi ambao ni watu kamili, wanaokubali kurekebishwa, kukosolewa, kukubali na kupokea changamoto.
Uwepo wa viongozi ambao ni watu nusu kunaweza kupoteza kabisa picha halisi ya uongozi bora.

*Muwe na asubuhi njema*
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom