Mtu kama alitoka mfano kada ya Ualimu kuwa Mkurugenzi, akitemwa kwenye uteuzi inakuwaje?

Wakuu nimejiuliza suala hilo sikupata jawabu.

Je, mtu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi kutoka kada za afya, ualimu au majeshini, siku akitemwa wakati wa uteuzi mpya, huwa anarudia kazi yake?

Kama harudii kazi yake je ni kwa nini? Au ni kama mtu aliyefukuzwa kazi?
Kama ni mfuatiliaji utakuwa umemsikia Ummy Mwalimu akisema wakurugenzi wote waliotemwa waende ofisi ya RAS wakapangiwe majukumu mengine.
 
Itabidi ukapimwe akili mana kwa ukurugezi wote ujajiwekeze mpaka utamani kurudi kwenye kazi yako ya awali. Mfano ulikuwa teacher umepigwa chini ukurugezi urudi tena kushika chaki si utakuwa mwendawazimu
Inategemea muulize kwanza ticha anafundisha level gani na sehem gani? Alaf tuje tuconlude
 
Tangu Magufuli aingie ameharibu maana ya utumishi wa umma.

Haiwezekani uache kuteua wasomi na wazoefu kwenye masuala ya management wawe maDED unachagua uvccm wenye miaka 24
Utumishi umekuwa wa hovyo hovyo, hopeless kabisa... watumishi wanajituma kwenye halmashauri wakijua watakuja kuwa promoted kuwa DEDs kama muundo unavyotka, mara paap demu kutoka UVCCM analetwa, maujinga
 
Kama ulikuwa mtangazaji clouds FM je?
Inakuwa imekula kwako kwa nafasi ya Udc ama Urc,ndio maana inashauriwa U-ded ni awe ni muajiriwa serikalini ama kama ulikuwa haupo utumishi wa umma basi ukitolewa kwenye cheo icho unabaki ukouko kusubiri kupangiwa kazi nyingine
 
Kama ni mfuatiliaji utakuwa umemsikia Ummy Mwalimu akisema wakurugenzi wote waliotemwa waende ofisi ya RAS wakapangiwe majukumu mengine.
Halafu ukirudi bora uombe upelekwe kwenye mashirika,ukibaki ukouko Tamisemi salary yake inakuwa kama ya mhudumu wa ofisi sasa si bora urudi nyumbani kama ni mfugaji ufuge kama ni mtumishi wa mungu urudi kanisani ukawe mzee wa kanisa kama ni muislamu basi uwe katibu ama mweka hazina
 
Wakuu nimejiuliza suala hilo sikupata jawabu.

Je, mtu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi kutoka kada za afya, ualimu au majeshini, siku akitemwa wakati wa uteuzi mpya, huwa anarudia kazi yake?

Kama harudii kazi yake je ni kwa nini? Au ni kama mtu aliyefukuzwa kazi?
Unarudi kwenye kada yako! Na leo Ummy katoa maelekezo kwa hao waliotemwa kwamba waende wakaripoti kwa waajiri wao wa mwanzo ili wapangiwe majukumu. Kumbuka hata Shaban Kisu alivyotemwa kwenye u-DC alirudi TBC.
 
Wakuu nimejiuliza suala hilo sikupata jawabu.

Je, mtu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi kutoka kada za afya, ualimu au majeshini, siku akitemwa wakati wa uteuzi mpya, huwa anarudia kazi yake?

Kama harudii kazi yake je ni kwa nini? Au ni kama mtu aliyefukuzwa kazi?
Kwa nafasi ya DED unaenda kureport kwa katibu tawala RAS wa mkoa wako, yeye atakupangia kazi katika idara/kitengo anachoona utafaa, lkn pia anaweza akakupa dawati pasipo kazi yyt.

Kwa vyeo vya kisiasa visivyo vya (kitaalam) DC etc... nadhani unarudi kwenye kazi yako ya awali kwa maana ya mwajiri wako wa awali.
 
Afya, Ualimu, Uanajeshi ni taaluma zinazosomewa na hivyo kutunukiwa cheti cha kitaaluma. Mtu anapoteuliwa kuwa mkurugenzi kutokea kwenye fani hizo tajwa na nyinginezo, wanatambulika kuwa wameazimwa tu.... "Secondment".

Inapotokea mteuliwa kutemwa au kukamilisha kazi iliokusudiwa, ana hiali ya kurudi kwenye nafasi yake kitaaluma na kuendelea na kazi. Ni wachache sana wenye uthubutu wa kurudi chini baada ya kuonja asali. wengi huingia kwenye ule mzunguko wetu fyongo.... kukimbilia vyama vya upinzani, kugombea ubunge na udiwani, kuokoka na kuwa mhubiri mahiri n.k.
Duuu Kama na wewe ulitemwa afu ukagombea ubunge mkuu. Kiukweli inakuwa ngumu Sana. Na ndo Mana ukipata gepu cheza nalo poa sana.usikute ulikuwa unawakoromea wa chini yako ndo basi wanageuza maumivu yako kwako
 
Tangu Magufuli aingie ameharibu maana ya utumishi wa umma.

Haiwezekani uache kuteua wasomi na wazoefu kwenye masuala ya management wawe maDED unachagua uvccm wenye miaka 24
Matokeo yake hawa ma DED 'uvccm' unakuta utumishi hawaujui, kazi hawazijui! Wanalipuka lipuka tu wajioneshe
 
Duuu Kama na wewe ulitemwa afu ukagombea ubunge mkuu. Kiukweli inakuwa ngumu Sana. Na ndo Mana ukipata gepu cheza nalo poa sana.usikute ulikuwa unawakoromea wa chini yako ndo basi wanageuza maumivu yako kwako
:oops:Umekosea sana chief....Pole sana. Sihitaji Serikali au Mtu au kampuni iniajiri ili mkono uende kinywani. Kazi ya mikono yangu na akili niliyopewa na Allah ndio inayonifanya niyamudu maisha haya🤔 ...Pole sana Chief !!.;)
 
principle ni ile ile tuu ya kuhusu ukomo wa utumishi wa Umma
Mtumishi anakoma kuwa mtumishi wa Uma kwa kustaafu au kifo.
Hivyo hao wakurugenzi watapangiwa kazi nyingine na wataendelea kupata mishahara na stahiki zao hadi utumishi wao utakapo koma
 
Kwani unafikiri wakurugenzi wanalipwa kiasi gani? Ama unaongelea wakurugenzi wezi?
Itabidi ukapimwe akili mana kwa ukurugezi wote ujajiwekeze mpaka utamani kurudi kwenye kazi yako ya awali. Mfano ulikuwa teacher umepigwa chini ukurugezi urudi tena kushika chaki si utakuwa mwendawazimu
 
Wakuu nimejiuliza suala hilo sikupata jawabu.

Je, mtu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi kutoka kada za afya, ualimu au majeshini, siku akitemwa wakati wa uteuzi mpya, huwa anarudia kazi yake?

Kama harudii kazi yake je ni kwa nini? Au ni kama mtu aliyefukuzwa kazi?
Majibu:
1. Kama hajafika miaka 60 atarudi mkoani kwake kwa mwajiri wake RAS. Mara nyingi hawezi kurudi kushika chaki au kufunga vidonda au kupima viwanja. Kwaheshima hubakia mkoani kumsaidia RAS majukumu au kusoma magazeti.

2. Mshahara wake haubadiliki/haushuki bado ataendelea kulipwa mshahara wa mkurugenzi ila tu atakosa posho za ukurugenzi.

3. Kama mwanzoni hakuwa mtumishi wa umma, akitemwa basi atarudi alikokuwa kama kuosha magari au mganga wa kienyeji au barmaid
 
Unaendelea kubaki mtumishi wa umma. Ila una hiyari ya kuacha.

lakini ktk hali ya kawaida; nguvu ya kushika chaki unaitoa wapi baada ya kuhudumu ukurugenzi kwa miaka kadhaa

Kwa mtu anayependa kujifunza na kufanya kazi kwa weledi; kufanya kazi ya ukurugenzi inakupa uzoefu mkubwa hata kuweza kushinda ktk nafasi za juu za taasisi zingine; aidha private au government. Kwa hiyo haiwez kuwa mwisho wako. Shida iliyopo wengi hufanya kazi kwa mazoea.

kwa ufupi ukitenguliwa unabaki kuwa mtumishi wa umma
 
:oops:Umekosea sana chief....Pole sana. Sihitaji Serikali au Mtu au kampuni iniajiri ili mkono uende kinywani. Kazi ya mikono yangu na akili niliyopewa na Allah ndio inayonifanya niyamudu maisha haya🤔 ...Pole sana Chief !!.;)
Hujanielewa naona. Yaani mie nimeongea kuwa kulingana ulivyoongea na wewe Kama ulipita humo na saivi u mbunge vile.
Pia pole kwa kunielewa isivyo.
 
Hujanielewa naona. Yaani mie nimeongea kuwa kulingana ulivyoongea na wewe Kama ulipita humo na saivi u mbunge vile.
Pia pole kwa kunielewa isivyo.
Inawezekana sikukuelewa, namna ulivyotoa hukumu kwa kile kisichofanana na dhamira au hulka yangu.... Kama sasa tumeelewana basi... Maisha yaendelee !.👌👌
 
Back
Top Bottom