Mtu kama alitoka mfano kada ya Ualimu kuwa Mkurugenzi, akitemwa kwenye uteuzi inakuwaje?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Wakuu nimejiuliza suala hilo sikupata jawabu.

Je, mtu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi kutoka kada za afya, ualimu au majeshini, siku akitemwa wakati wa uteuzi mpya, huwa anarudia kazi yake?

Kama harudii kazi yake je ni kwa nini? Au ni kama mtu aliyefukuzwa kazi?
 
Tangu Magufuli aingie ameharibu maana ya utumishi wa umma.
Haiwezekani uache kuteua wasomi na wazoefu kwenye masuala ya management wawe maDED unachagua uvccm wenye miaka 24
Ameharibu sana.
Tutamkumbuka kwa mabaya pia.
 
Wakuu nimejiuliza suala hilo sikupata jawabu.
Je mtu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi kutoka kada za afya,ualimu au majeshini,siku akitemwa wakati wa uteuzi mpya,huwa anarudia kazi yake?

Kama harudii kazi yake je ni kwa nini? Au ni kama mtu aliyefukuzwa kazi?
Afya, Ualimu, Uanajeshi ni taaluma zinazosomewa na hivyo kutunukiwa cheti cha kitaaluma. Mtu anapoteuliwa kuwa mkurugenzi kutokea kwenye fani hizo tajwa na nyinginezo, wanatambulika kuwa wameazimwa tu.... "Secondment".

Inapotokea mteuliwa kutemwa au kukamilisha kazi iliokusudiwa, ana hiali ya kurudi kwenye nafasi yake kitaaluma na kuendelea na kazi. Ni wachache sana wenye uthubutu wa kurudi chini baada ya kuonja asali. wengi huingia kwenye ule mzunguko wetu fyongo.... kukimbilia vyama vya upinzani, kugombea ubunge na udiwani, kuokoka na kuwa mhubiri mahiri n.k.
 
Itabidi ukapimwe akili mana kwa ukurugezi wote ujajiwekeze mpaka utamani kurudi kwenye kazi yako ya awali. Mfano ulikuwa teacher umepigwa chini ukurugezi urudi tena kushika chaki si utakuwa mwendawazimu
utoke kuendeshwa na v8,nyumba kubwa full ulinzi masaa yote,kikao hakifanyiki hadi wewe uwepo,Mshahara wake mmoja unaweza tumia hata miezi 3 mbele ila kama mwenzangu na mie huo mmoja unakaa nao hata miezi sita.

Sasa ndio uhuhudumu kwa nafasi iyo kama miaka 4 uje utolewe,je bado tu utakuwa na nguvu tena ya kuja kusumbuana na wanafunzi kusahihisha mitihani yao ama ndio ukimbizane na wanafunzi kuhusu usafi wa shule
 
Hivi vyeo ni dhamana, ukipata basi wekeza Sana kwenye rasilimali vitu na rasilimali watu. Huwezi jua yajayo
 
Tangu Magufuli aingie ameharibu maana ya utumishi wa umma.
Haiwezekani uache kuteua wasomi na wazoefu kwenye masuala ya management wawe maDED unachagua uvccm wenye miaka 24
Mama kama Mama ulichotufanyia kwimba itoshe kusema nakubali kuwa unaupiga mwingi ts ze best ded ever
 
Yeah unaruhusiwa kurudi kwenye taaluma uliyosomea

tatizo ni Ushakuwa mkurugenzi halafu urudi kwenye hizi 'staff' za wafanyakazi wenzio utapigwa majungu hd utajuta......
 
Wakuu nimejiuliza suala hilo sikupata jawabu.
Je mtu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi kutoka kada za afya,ualimu au majeshini,siku akitemwa wakati wa uteuzi mpya,huwa anarudia kazi yake?

Kama harudii kazi yake je ni kwa nini? Au ni kama mtu aliyefukuzwa kazi?
Hili swali nmeulizwa leo nmeshndwaa kujibu wanazengo
 
Wrong example,

mfano wako hauna uhalisia.

wewe utakuwaje DED wakati hata ukuu wa idara hujaufikia.

Yaani utoke shuleni unakofundisha ghafla uteuliwe DED straight!
au sijakuelewa.

Lakn kama uliteuliwa kuwa DED straight toka mtaani halaf teuzi yako ikatenguliwa na wewe proffessionally ni mwl culture ni ileile.

Wengi ma-DED's hufichwa kwny ofisi za RAS mikoani baada ya tenguzi huku wakiendelea kulipwa mishahara ileile wakisubl kustaafu.
 
Wakuu nimejiuliza suala hilo sikupata jawabu.
Je mtu akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi kutoka kada za afya,ualimu au majeshini,siku akitemwa wakati wa uteuzi mpya,huwa anarudia kazi yake?

Kama harudii kazi yake je ni kwa nini? Au ni kama mtu aliyefukuzwa kazi?
Tumia huo muda kuongeza Elimu yako🤝
 
Back
Top Bottom