Mtoto wa nje ya ndoa

Amantogoyoka

Member
Jul 9, 2015
32
10
Mambo vp members,

Nilikuwa na house girl mtu mzima kama miaka 30 na ushee hivi, wakati huo nilikuwa naishi mbali na familia yangu kikazi, nimeishi na huyo house girl kwa muda mrefu kama miaka mitano lakini baada ya hapo uzalendo ukanishinda matokeo yake akawa amepata mimba na kuzaa mtoto wa kiume. sijawahi kumwambia mke wangu kuhusu jambo hili sasa naomba ushauri wenu nifanye nini? kwa sasa mtoto ana umri wa miaka 2 na sina mpango wa kuoa mke wa pili kwa vile ndoa yangu ni ya kikiristo
 
1. Endelea kulea wote wawili hadi siku Mungu atakapokuchukua;
2. Mwanzishie huyo mama mradi wa maana (sustainable)-mwanao atakuwa yuko safi.
3. Endelea kuwapenda tu (hata kama ni kwa remote control).

NB: Kama vipi mweleze mkeo kuwepo kwa mtoto huyo (hata kama hutamleta nyumbani). Hapa inategemea na mkeo alivyo-maana kwa wengine panaweza kuchimbika!
 
Duuu... Ndoa hizi shida tupuuu. Katika jambo la mwisho mie kukubali ni kulea mtoto wa nje aliyezaliwa wakati tumeoana. Ni mtazamo wangu.

Kitanda hakizai haramu mama awe wa siku nyingi awe wa juzi ni damu ya mumeo nani ndugu wa watoto wako. Cha muhimu ni kumsamehe mumeo tu na kuhakikisha hatatoka nje na kama ni kazi ya mbali basi aje karibu.
 
Hadi kuja kujishtaki hapa ina maana huyo mchepuko keshakukamata kisawa sawa...just be a man, kaa chini na mkeo mweleze kiutu uzima atakuelewa ili mwanao asiwe kuku mgeni pindi likitokea la kutokea kwako baada ya kuhitimisha kazi uliyotumwa na Mungu duniani!
 
1. Endelea kulea wote wawili hadi siku Mungu atakapokuchukua;
2. Mwanzishie huyo mama mradi wa maana (sustainable)-mwanao atakuwa yuko safi.
3. Endelea kuwapenda tu (hata kama ni kwa remote control).

NB: Kama vipi mweleze mkeo kuwepo kwa mtoto huyo (hata kama hutamleta nyumbani). Hapa inategemea na mkeo alivyo-maana kwa wengine panaweza kuchimbika!

umenena vyema...
 
Muache huyo aliyekuwa msaidizi wako aendelee kumlea, labda kama kuna tatizo. Vinginevyo utaanzisha balaa ndani ya ndoa na kuitia ndoa dosari kubwa sana.
 
mmmh kazi ipo hivi unaanzaje kumwambia sijui utaimba wimbo kama diamond :clap2:
 
Mmh hivi naanzaje kumuacha mume wangu aishi na house girl Peke yao? Mbona kutafuta kumsingizia shetani eeeeh
 
Muache huyo aliyekuwa msaidizi wako aendelee kumlea, labda kama kuna tatizo. Vinginevyo utaanzisha balaa ndani ya ndoa na kuitia ndoa dosari kubwa sana.

Kama ni dosari tayari ishatokea cha muhimu hapo ni kutatua tatizo tu
 
Ni vzr ukatafuta Muda mzuri na kwa unyenyekevu mkubwa ukamwambia mke jambo hili. Lakini ni vzr pia ukamweleza mzazi mwenzio kuwa mtoto ulie zaa nae asiwe kinga au ngao ya kutumiwa kama "kukunyanyasa".
 
Inaweza kabisa ikawa si kutatua tatizo bali kulifanya kuwa kubwa sana. Mume hajui reaction ya mkewe itakuwa vipi baada ya kufahamu kwamba wakati wamo kwenye ndoa kumbe alikuwa anamvua chupi mfanyakazi wa ndani tena kwa kipindi kirefu tu.

Kama ni dosari tayari ishatokea cha muhimu hapo ni kutatua tatizo tu
 
Kitanda hakizai haramu mama awe wa siku nyingi awe wa juzi ni damu ya mumeo nani ndugu wa watoto wako. Cha muhimu ni kumsamehe mumeo tu na kuhakikisha hatatoka nje na kama ni kazi ya mbali basi aje karibu.

Neno kitanda hakizai haram ni ndani ya ndoa na sio nje ya ndoa, mlee na toa huduma zote kwa mama na mtoto.
 
Wallah hakuna dosari mbaya kama kuzaa nje ya ndoa,maana nikovu lisilo futika milele ,bora kufumaniwa loo.
 
Back
Top Bottom