COURTESY
JF-Expert Member
- Jun 16, 2011
- 2,006
- 706
St Mathew Secondary School
S1071/0102
F
JESCA JOHN MAGUFULI
30
IV
CIV-D HIST-D GEO-D KISW-F ENGL-C B/MATH-F COMM-F
============
NECTA CSEE 2011
Hayo ni matokeo yake na sasa hivi anasoma UDOM.
======
Watanzania bado tukiwa katika sintofahamu juu ya wanafunzi 7,000+ waliofukuzwa chuo cha UDOM siyo vibaya tukaangalia namna gani HAKI inavyoweza kutendeka bila upendeleo wowote kwa kigezo cha uwezo au wadhifa.
Tunaamini kitendo cha binti wa Mhe Rais kusoma katika chuo cha ndani ya nchi yetu ni cha kiuungwana na cha kizalendo ingawa hatujui kama alikidhi vigezo au hapana.
Kwa kifupi binti huyu awali wakati anaanza masomo yake ya degree pale UDOM alipangwa kozi ya HRM (Human Resource Management).
Baada ya baba kupata wadhifa akawa amehama kozi kutoka HRM akahamia kozi mpya ya (Political Sciences and Public Administration) PSPA.
Katika suala la Malazi Mwaka wa kwanza alikaa kampasi ya chuo na baada ya baba kupata wadhifa kuwa rais anakaa Ikulu ndogo Chamwino mbali na kwamba anacho chumba chake chuoni na hakikai mtu.
Katika suala la usafiri. Analetwa chuoni na gari la Serikali aina ya VX ya kijani kila siku chuoni na kurudi.
Kwa kuweka tofauti zetu kando tujadili kwa mustakabali wa nchi yetu.
Nawasilisha!!
Chanzo: Class mate.