Mtoto wa Liyumba akamatwa na madawa ya kulevya yenye thaman ya Bil 9 Tsh

Kuna namna hapa, obviously. Sasa imani inaanza kunipaa. Kuna big chance Liyumba ni mtu powa sana ila kuna mpango mzima wa kumdemonize yeye na familia yake. This is bongo, semi-anarchy state.
 
Ukiona hivyo ujue walipishana kauli.Manake ni adimu sana vitu hivi kukamatwa
 
Wakikamata bangi wanateketeza kwa moto wakikamata unga hatujawahi ona wakiteketeza au ndo dili la mapolisi nao kushiba?
 
...vijana wanaangamia jamani, taifa laenda wapi hili! Shiiiit...
 
Hilo nalo neno... Nani wa kuchoma moto mijihela..?

Hizi dili za sembe ni za wadosi kapuku huwezi piga hata siku moja, na hapo hakuna kesi we subiria utaona kesi imeyeyuka kiana na hicho kidemu kinarudi uraiani kuendelea kupiga dili za hatari hizo.
 
huyo kachomwa tu na nanhiii....mbona hata nanhiii nasikia nae anafanya hayo makitu...?? nasikia waliwachoma wale wa pakistan waliokamatwa mbezi beach kisa walizinguana mgao....washua wengi hapa town wanajeuri kutokana na hayo mambo....R.I.P amina chifupa manake yawezekana kwenye ile list yake hawa nao walikuwemo.


Mh Zion una habari kamili!!
Waweza msaidia Nzowa kwa karibu zaidi!
 
Mimi mshamba ninaomba kuuliza matumizi hasa ya haya madawa..........ni hii hii tu ya mateja kuvuta au kuna matumizi mengine?
(Natanguliza samahani kama nimeuliza swali la kitoto)
 
Nafuatilia mzigo huu utahifadhiwa wapi,jamani polisi wa kituo hicho mbona watatajirika ghafla?
 
Ana miaka 21 tu, ameshikwa na heroin kilo 200 zenye thamani ya Shilingi bilioni 9. Amekamatwa huko Lindi jana. Kwa mujibu wa polisi kitengo cha madawa, hii imevunja rekodi tangu kitengo hicho kilipoanzishwa mwaka 1990. Kama binti wa Liyumba ni dealer, vp baba yake? Vp na wengine?

Source: Nipashe/Mwananchi.

hata babake alivunja rekod kwa kukutwa na sim
 
Mods waruhusu tuwataje hili wawekewe mitego,wale jamaa wa mbezi jogoo waliokamatwa na mapodaaaa ni watu wa bata ndefu asubuhi utawakuta wapo mbele ya gadeni na machupa ya litre 1.5 na magazeti wanakula upepo kwa ndani kuna DCM imepaki,na magari mengine madogo,hawa watu wanaua rasilimali watu wa taifa letu

wataje am a moderator
 
kwanini wamemkamatia TZ? Wangembeba na dawa zake wakamkamatie CHINA,ili tuletewe majivu ya kuzika,

hivi kama yule dada wa SA alikamatwa na 3kg akanyongwa je huyu wa 200kg si wange poteza kuwanzia kizazi chake yaani kuanzia baba,mama hadi wajukuu

ila kwa kuwa amekamatwa Tz utasikia tu hatuna ushahidi,ooh umri wake mdogo,oooh ni mtoto wa mkubwa,oooh haina shida tumezichukuwa dawa

CHINA OYEEEEEEEEEEE
Nawapenda sana WACHINA hakuna cha haki za binadamu ni sindano ya sumu tu
 
Hizi sio njama kweli? I sniff something, sio kama ya mtoto wa Mengi hii? Ngoja tuone...

JESHI la Polisi mkoani Lindi wakishirikiana na askari wa kupambana na kuzuia madawa ya kulevya kutoka jijini Dar es salaam, wamekamata jumla ya kilo 210 za madawa ya kulevya aina ya Heroine, yanayokadiliwa kuwa

na thamani ya Sh, 6.3 bilioni.Kaimu kamanda wa Polisi mkoani hapa, George Mwakajinga amewaambia waandishi wa habari hizi Ofisini kwake mjini hapa kuwa, madawa hayo yamekamatwa jana,saa 12:0 asubuhi, katika kijiji cha Mchinga mbili, wilaya ya Lindi.Amewataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na mwenye nyumba yaliyokutwa madawa hayo, aitwae Pendo Mohamedi Cheusi (67) mkazi na mkulima wa kijiji hicho na Hemedi Said (27) dereva na mkazi wa mtoni,jijini Dar

es salaam,ambaye pia ni mtoto wa mwenye nyumba yaliyokutwa madawa hayo.Wengine ni Isumaili Adamu kwa jina lingine Athuman Mohamedi Nyaubi (28) mfanyabiashara wa magari nchini Afrika ya kusini na mkazi wa Moroko jijini Dar es salaam na Morine Amatus (22) mkazi wa Mikocheni ‘B’ pia jijini Dar es salaam.Mwakajinga amesema madawa hayo yamekamatwa ndani ya nyumba ya Pendo Cheusi,yakiwa yamehifadhiwa ndani ya madumu yapatayo manane yaliyokuwa na ujazo wa lita 60 kila moja,tayari kusafirishwa kupelekwa nje ya nchi.Amesema mafanikio ya kukamatwa kwa madawa hayo,yamechangiwa na raia wema kutoa taarifa za siri ndani ya Jeshi hilo ,kisha kufanikisha kuyakamata.“Sisi Polisi kwa kushirikiana na kikosi kazi kilichokuwa kinaongozwa na mkuu wa upelelezi mkoa wa Lindi,ASP,Faustine P.Hokororo,walipofuatilia hatimaye jana tumefanikiwa kuyashika madawa hayo wakiwemo na wahusika” Alisema Mwakajinga.Mwakajinga amesema tayari madawa hayo, yamesafirishwa kupelekwa jijini Dar es salaam , kwa mkemia mkuu kwa ajili ya kuyapima, sanjari na kuyatunza wakati kesi ya watuhumiwa hao itakapokuwa ikiendelea

mahakamani.Kaimu kamanda huyo amesema watuhumiwa wawili kati ya wanne walioshikwa wamefiishwa mahakamani leo ambapo upelelezi zaidi ya madawa hayo ukiendelea.Pia Mwakajinga amewashukuru wale wote waliofanikisha kutoa taarifa ya kuwepo kwa madawa hayo, na kuongeza ni mara ya kwanza kwa mkoa wa Lindi kukamata madawa mengi kiasi hicho, huku akizidi kuwaomba

wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya dola kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa vitendo ambavyo vinakwenda kinyume na maadili ya nchi.

michuzi blog
 
" anatuhumiwa" hajahukumiwa bado, kwahiyo tusijudge moja kwa moja kwa hatua hii. kwani inawezekana bifu zinaendelea kwa mtindo huu, tusipokuwa makini tutakuwa tunashabikia jambo ambalo hatulijui undani wake. si mnakumbuka mzee mengi alivyowawahi kwenye mitego yao michafu? yaliishaje mnajua?
 
No si lazima Liyumba awe anahusika katika hili naomba nimtetee,liyumba ana yake lakini kwa hili hapana kutokana mazingira alokuwepo sasa,huyu dogo ni above 18,ni msichana mkubwa kabisa.Dogo atakuwa alitumwa kwenda kumpokea mtu dizaini mozambuque. ngoja niwang'ate sikio but sitaki maswali kwamba nimejuaje!

Iko hivi,wasfirisha wa madawa wana njia nyingi,za kuwakwepa askari,kinachofanyika hapa ni kwamba kuna mtu anaetumwa kwenda kuchukua mzigo pele(brazil)au musharaf(pakistan)kupitia iran,huyu akishapakia mzigo(dawa za kulevya)anapanda ndege mpaka may be Dubai au nchi za kusini mwa africa kama hapa kwa kesi ya mtoto wa Liyumba kutokana na aliposhikiwa hapo lindi inaonyesha kuna mtu alitoka shamba akashukia mozambique,huyu mtu alitoka na mzigo brazil ama pakistan/iran kazi yake inaisha baada ya kushuka airport ya moja ya nchi nilizozitaja hapo juu amabako hashuki ovyo ovyo lazima kunakua na mchongo wa kushukia hapo yani mabosi wake wanakuwa wameshaseti mambo hapo airport husika hivto jamaa anashuka hapo salama na kuingia mjini then anachukua hotel.Hapo sasa anatumwa kijana kama huyu wa liyumba kutoka hapa bongo na passport yake ya karatasi anasafiri kwa njia ya barabara napita boda ya tz na mozambique anagonga passport yake hiyo ya karatasi kama kawaida hapo boda then aningia mozambique anakwenda mpaka kweny hiyo hoteal aliyofikia yule aliyetoka shamba,hapo wanabadilisha na mzigo huyu dogo aliyetoka bongo anauchukua mzigo then anatambaa nao kivyake kwa njia ya barabara anapita pale boda anagonga muhuri wa kumtoa mozambique huyo anaingia zake Tanzania bila kushukiwa na yeyote kwa kuwa wanajua alienda mara moja mozambique tena na ppt ya karatasi,basi anasafiri mpaka dar anakabidhi mzigo anakula milioni zake 5! kwa safari hiyo ya siku kama 3 tu!lengo la kwenda kumpokea yule ni kuficha ile mihuri ya visa za pele au musharaf zisionekana maana visa za nchi hizo zinajulikana na watu wa madawa,brazili utaenda kufanya nini kama sio madawa tu..?

Habari ndio hiyo,maswali yanakaribishwa,naipenda nchi yangu,nimeamua kusaidia kidogo,ila usinilulize tu nimejuaje!

sasa wanazitoa vipi uwanja wa ndege? maana hapo kuna ulinzi wa hali ya juu,ama napo maboss wanahonga? lakini pia inaonekana kama dawa zilikuwa zikitakiwa kusafirishwa nje ya tz hapo chain yake hadi kufika lindi imekuwaje?
 
Back
Top Bottom