Mtoto wa Liyumba akamatwa na madawa ya kulevya yenye thaman ya Bil 9 Tsh

Na Mwandishi Wetu

SAKATA la Morine Liyumba ambaye ni binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga', linawahusisha vigogo 10 Bongo. Vyanzo visivyo na shaka vimelitajia Amani majina 10 ya vigogo ambao wanahusika katika mtandao ambao ndiyo uliokuwa unasafirisha madawa hayo ya kulevya kabla ya kukamatwa na Jeshi la Polisi Tanzania, Lindi.

Vimedai kuwa mtoto wa Liyumba na vijana wengine waliokamatwa ni ‘dagaa' na kuongeza kwamba ‘papa' wapo, siku wakitajwa taifa litatikisika kwa sababu majina yao ni makubwa na hadhi yao kijamii ipo juu.

"Hali ni mbaya, inasikitisha kwa sababu taifa linawaheshimu lakini wao ndiyo wahalifu. Wanaendesha mitandao hatari ya kuuza ‘unga'. Vijana ambao ni nguvu kazi wanaharibika na kugeuka mateja kwa sababu yao," kilisema chanzo chetu ambacho kinahifadhiwa jina. Chanzo kingine kiliongeza: "Inatakiwa safari hii serikali iwe makini kwelikweli. Imeshaamua, kwa hiyo isisite kuchukua uamuzi mgumu. Hatutaki kuona majina ya watu yanaachwa kwenye hili sakata la kukamatwa kwa mtoto wa Liyumba. Wote wafikishwe mahakamani."

Amani limetajiwa majina ya vigogo 10 ambao wanadaiwa kuwemo kwenye mtandao uliokuwa unasafirisha madawa ya kulevya kabla ya kukamatwa Lindi wiki iliyopita lakini yanahifadhiwa kwa sababu ya kukwepa kuvuruga upelelezi wa kipolisi.

Morine, alikamatwa pamoja na mfanyabiashara wa magari, Ismail Adamu au kwa jina lingine, Athuman Mohamed Nyaubi, 28, raia wa Tanzania anayeishi Afrika Kusini. Mwingine aliyekamatwa ni dereva, Hemed Said, 27, mkazi wa Mtoni, Temeke, Dar es Salaam na Pendo Mohamed Cheusi, 67, mkazi wa Lindi ambaye ni mmiliki wa nyumba ambayo ilikutwa na madawa hayo.

Kwa upande mwingine, wananchi waliozungumza na Amani, wamemtaka Rais Jakaya Kikwete adumishe ulinzi kwa Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa. Wamesema kuwa Nzowa anapambana na watu wazito ambao wana fedha nyingi lakini kazi yake ina manufaa makubwa kwa nchi kutokana na kitendo cha idara yake kuwaokoa vijana na janga la matumizi ya madawa hayo. Nzowa aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa amekuwa akipokea simu mbalimbali za vitisho kutoka kwa watu asiowafahamu kutokana na kazi yake.

Alipoulizwa anafanya nini ili kujihami na watu hao, alisema mara nyingi huwa anamtegemea Mungu. "Mimi namtegemea sana Mungu na ndiyo maana mara zote utanikuta nikiwa na Kitabu cha Biblia Takatifu na huwa nasoma Zaburi ya 23."


Source
: Global Publishers
Pumbavuuu !!!! Si muwatajee tuu. Huu ujinga mpaka lini ???
 
source Global Publishers =udaku

hata hivyo Nzowa hana jipya

hivi ile issue ya mtoto wa mzee Mengi Nzowa si alihusika
hivi hii issue ya mtoto wa mengi ilikauje??? mwenye uelewa nayo aishushe hapa wakuu.
 
hii laana ya wazazi itaendelea tu kwao hao wauza unga na watengezaj kwa kutuharibia watoto wetu....watu wanaopenda haramu hata wawe na pesa kiasi gani hawaridhiki na isitoshe pesa zao zinaishia ktk anasa za dunia..
 
Tanzania tukiendekeza huu ujinga hatutaijenga hii nchi kamwe. nani kasema hela za unga zinajenga na kuinufaisha nchi? Tunapoteza muda wetu bila sababu. Tuingie kwenye biashara za kueleweka. Kenya wanauza maua, mazao ya kilimo etc! Why not us???
Mkuu umeongea point lakini upande ule watakupinga mkuu .....am sorry
 
Back
Top Bottom