Mtoto wa Liyumba akamatwa na madawa ya kulevya yenye thaman ya Bil 9 Tsh

Habari gani hii sasa wapi majina ya watuhumiwa?walikamatwa trh?mwezi?mwaka?...otherwise ni uzushi wa magazeti ya Shigongo
 
Habari hii ni ya kweli na picha za dagaa waliokamatwa zilionyeshwa .....wangetajwa hao vigogo ingependeza kuwajua hata kama ni watuhumiwa tu kwani ndio ada ya kuhusishwa na uhalifu ingawa tutaambiwa upelelezi bado unaendelea lakini kwa dagaa upelelezi hauendelei.
 
Morine Liyumba, Ismail Adamu, Athuman Mohamed Nyaubi, Hemed Said, Pendo Mohamed Cheusi. Sio wa muhimu kwa sababu tayari wanajulikana kuwa walikamatwa na dawa za kulevya. Wa muhimu ni hao Vigogo unaoendelea kuhifadhi majina yao. Taja hao ndio uonekane shujaa. Vinginevyo, mimi binafsi naona kama ni njia ya kuongeza mauzo ya gazeti.
 
Hapa zitatembea pesa ndefu na hakuna atakaye fungwa....labda kwa kulipwa!
 
kama kamanda mkubwa wa jeshi letu anaishi kwa hofu kiasi hiki je mwananchi wa kawaida atawezaje kuwa huru

Mtasikia sasa hivi kapelekwa India, kama atakuwa na bahati.
nadhani mnakumbuka jinsi wakemia wakuu wanavyokufa vifo vya ajabu.
 
Habari imekaa kigegereka.

Nahisi mreta hii habari kapotea mlango alifikiri anaandika kwenye gazeti la udaku kumbe yupo JF.

Kasahau kuwa huku hakunaga kuremba,porojo na mbwembwe hata kama jina la raisi lipo au baba yako hapa jf we lipua tu.
Hakuna wa kukuchifupa hapa ni full maulinzi.
 
vigogo gani taja majina
mie nina wasiwasi na chanzo ninavyojua mie amani na global kwa ujumla ni magazeti ya udaku sasa kama wanataka kutuletea mambo ya kina wema sepetu humu jf wakome sie twajali chanzo na humu hakuna mafumbo
waende huko huko
 
source Global Publishers =udaku

hata hivyo Nzowa hana jipya

hivi ile issue ya mtoto wa mzee Mengi Nzowa si alihusika
 
SAKATA la Morine Liyumba ambaye ni binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba, kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga', linawahusisha vigogo 10 Bongo. Vyanzo visivyo na shaka vimelitajia Amani majina 10 ya vigogo ambao wanahusika katika mtandao ambao ndiyo uliokuwa unasafirisha madawa hayo ya kulevya kabla ya kukamatwa na Jeshi la Polisi Tanzania, Lindi.

Sawa..Ni issue ya few days ago..Sasa Amani ni nini? na kama wametajwa mbna hukuwaweka hapa tuone hayo majina as a copy and paste?? Wekeni mambo wazi kwani upuuzi wa baadhi ya Viongozi ni bora ukaanikwa hadharani ili wananchi tuone..Hata kama ni viongozi wa dini..Display their names for future...
A S 465.gif

 
Back
Top Bottom