Yaani we acha tu. Kwa kifupi, mamsap alikuwa ananipa mzigo wa kumtunza na kumsomesha mwanaye wakati huyo mtoto ana baba mitaani anabangaiza tu....Mamsap akawa ananipiga mizinga na kumpa hela jamaa yake ili ajiweke vizuri na siku akiwa na maisha mazuri waje kurudiana. Nilipata funu kwa watu japo sina uhakika sana kwamba mamsap alikuwa anakula uroda na yule kibaka wake. Nilipomuacha ghafla wacha alie na kunilamu eti mtoto alikuzoea na kukuona wewe ndiyo babake, nitamwambia nini sasa? Nikamwambia mtafutitie baba yake halisi, analia na kusema yule baba yake ni fala tu hapo hapo bado analala naye....wanawake jamani. Yule demu alinipotezea muda sana na alikula hela zangu kumtunza fala wake.