Mtoto wa kigogo ahusishwa tukio la ubakaji hoteli ya KNCU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto wa kigogo ahusishwa tukio la ubakaji hoteli ya KNCU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jan 17, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Mtoto wa kigogo ahusishwa tukio la ubakaji hoteli ya KNCU

  Daniel Mjema,Moshi


  MTOTO wa mfanyabiashara mashuhuri wa mjini Moshi (jina tunalo), ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la kumlawiti mwanamme mmoja katika hoteli ya KNCU mjini Moshi baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.


  Mwanaume huyo alilawitiwa na wanaume watano katika chumba namba 53 cha hoteli hiyo baada ya kuwekewa mtego na mume wa mwanamke huyo ambaye pamoja na mkewe nao wameshitakiwa mahakamani.


  Mtoto wa mfanyabiashara huyo ambaye ni muuzaji maarufu wa bia na pombe kali za jumla alikamatwa juzi saa 9:00 alasiri na anatarajiwa kuunganishwa na watuhumiwa wengine watano katika kesi hiyo.


  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko jana alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kueleza kuwa kesho Jumatatu anatarajiwa kufikishwa mahakamani.


  "Tulimkamata jana(juzi) saa 9:00 alasiri na tumemwachia kwa dhamana wakati tukikamilisha taratibu za kumuunganisha na washtakiwa wenzake kesho Jumatatu"alisisitiza Kamanda Ng'hoboko.


  Watuhumiwa ambao tayari wamefikishwa mahakamani ni pamoja na Kelvine Mushi (32) na mkewe Vaileth Swai (30),na Kassim Mohamed(28), Albeth August (25) na Leon Kimambo(34) wote wakazi wa Mailisita wilayani Hai.


  Katika shtaka la kwanza, upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali,Hellen Moshi ulidai mahakamani kuwa washtakiwa hao watano walikula njama na kufanikisha kulawitiwa kwa mwanaumme huyo.


  Katika shtaka la pili, washtakiwa wanne ukimwondoa Vaileth, wanatuhumiwa kuwa Desemba 16,2009 saa 12:00 jioni, walitenda kosa la kumlawiti mwanaume huyo.


  Washtakiwa hao walikanusha mashtaka hayo na waliachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja ambao walitakiwa kusaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni au kuwasilisha hati za mali isiyohamishika.


  Habari zaidi zinadai kuwa kufumaniwa kwa mwanamume huyo kulitokana na mume wa mwanamke huyo kukamata simu ya mkewe na kuishikilia kwa siku na kuwasiliana na mwanamume huyo huku akijifanya ni mwanamke huyo.


  Mwanamume aliyetendewa unyama huo alipoteza fahamu katika purukushani za kupambana na watuhumiwa hao wasimkate uume wake na alipozinduka ndipo aliposhangaa amezungungwa na polisi na wafanyakazi wa hoteli hiyo
   
 2. O

  Omumura JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sheria ichukue mkondo wake!
   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Sababu za kutokutajwa jina lake wakati watuhumiwa wengine wametajwa ni nini?
   
 4. Guma Mlugaluga

  Guma Mlugaluga Member

  #4
  Jan 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wakuu, huyu kala vya wenzake, naye vyake vimeliwa, kosa gani la kuwapeleka mahakamani? Jamani, hebu tumuonee huruma na huyu jamaa aliyekuwa anaibiwa, yaani basi tu. Inauma sana. Aliye...tiwa simuhurumii, mbona wasichana wapo wengi sana, kwani lazima mke wa mtu?
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Duh, watu wamefikia hatua za kinyama namna hii ?? inasikitisha sana.
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Suala ni sheria za nchi zinasemaje. NUKTA.

  Hayo mengine sijui nimeibiwa sijui mke wangu hayo yataangaliwa kulingana na sheria zilizopo na itabainishwa nani mkosaji kwa mujibu wa sheria sio kwa mujibu wa maoni.
   
 7. Guma Mlugaluga

  Guma Mlugaluga Member

  #7
  Jan 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu Abdulhalim, naona hujaoa wewe. Kama unaye mke, hebu fikiria, ashakum si matusi, jamaa linahemea mkeo shingoni, utajisikiaje? Halafu mkeo anatoa ushirikiano wa kutosha! Duh! Basi acha sheria ichukue mkondo, lakini mkondo unaweza kuelekezwa kwa mlawitiwa vile vile, tehetehetehetehetehe.

  Mkuu bado najiuliza, sijui alikata na mauno! au aligangamala!
   
 8. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hii ndiyo dawa ya mipakashume,wao wake za watu tu. Me mwenyewe nikigundua mke wangu analiwa,lazima jamaa naye liwe,nitamkodia masela wamle tena nachukua na video,akisema tu na release video.

  Maana watu wamezidi kuhemea wake za watu.
   
 9. Guma Mlugaluga

  Guma Mlugaluga Member

  #9
  Jan 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Gooood! Mponjoli wewe mwanaume kama mimi.
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii safi sana jamaa wakimuweka rumende na masela watamlawiti tu
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Si unyama kaka, kula cha mtu ni Kifo. we hujui watu husema Kucheza na mke wa mtu ni sawa na kucheza na moto.? na mara nyingi watu hawa huonywa almost 3 times, ya nne mzee yanakufika maswahibu kama haya.

  Huyu jamaa bora asingeriport police maana yake siri imefichuka kwamba kavunjiwa duka na watu zaidi ya 5, aibu tupu bora angekauka akajitibia akapona yakaisha.
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Big thumb up! wangemkata uume ndiyo ingekuwa issue. but alichotendewa ni kumkomesha. Na je naye ana mke?
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sitetei kitendo cha kutembea na wake za watu. Il haki za kibinadamu zinaapply kwa wote tu, na ndio maana tunazo sheria tulizokubaliana zituongoze ili tuishi kwa amani.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Yaani una support barbarism kisa mwanamke??? Tena mwanamke kenda mwenyewe kuchojoa kwa mwanamme mwingine bila kushikiwa binduki wala kisu?? If it was my wife she is not worth it..Nitaendelea na ishu zangu tu maana we live only once mazee.
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenikumbusha miaka ya 2004 au 2005 mfanyabiashara maarufu alijitanua na mke wa mtu huko Kigoma alipokuwa na tender ya ujenzi wa nyumba za vyuo fulani mashuri nchini, jamaa akamtafutia wababe wakamtendea ufirauni na wakachukua video. Nakuambia yule mfanyabiashara alichanganikiwa na mwishowe alijiua na kuacha utajiri wake wote.
   
 16. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #16
  Jan 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  mh hv huyu mfanyabiashara ni machare investment au masuki?
   
 17. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Vipi kuhusu huyo mwanamke aliyekuwa anajua yeye ni mke wa mtu na akaamua kuvua nguo kwa mwanamme mwingine? Jee kama ndio tabia yake huyo mumewe atawalawiti wanaume wangapi? maana mke huyo anaweza kuendelea kugawa kama peremende maisha yake yote. Kitendo cha mume sio sahihi hata kidogo na hakita msaidia zaidi ya kumpeleka jela.
   
 18. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Ofoz kwa ujuzi mdogo wa sheria nilionao,hao waliomlawiti jamaa wanastahili kifungo cha maisha au jela miaka 30,Mwenye mke angekuwa na defence(provocation) iwapo angekuwa amefumania ghafla na kutenda kitu chochote kibaya kama kuua,kujeruhi n.k.Lakini hiyo inaonyesha jamaa alijua siku nyingi kama mke wake analiwa na akaplani kumkomoa mgoni wake.Ofcoz kuibiwa kunauma ndo maana sheria ikaconsider provocation,lakini hiyo ya kumlawiti mtu haikubaliki.
   
 19. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  hata mimi nina wasiwasi sana na huyu jamaa
   
 20. Guma Mlugaluga

  Guma Mlugaluga Member

  #20
  Jan 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Chakaza, wanawake wengi sana wanaisigina amri ya 6 na hawasitukiwi na mtu. Hapo ujue yule mwanamke alikuwa hamtaki jamaa, akamweleza mmewe, wakalitegea *****, wakalifanyizia. Siku hizi ni dili, hasa mjini. Yule sio ujanja wa mwanamme bali mke na mme wamemfanyizia.

  Sawasawa kabisa, iendelee hii tamu. Ukila, unaliwa!
   
Loading...