Mtoto wa Karume, Asha Abeid Amani Karume ajiunga CUF

Kwa wale tunaotaka kumfahamu mtoto wa Karume maekezo hayo

Na Mansour Yussuf Himid.

Leo nami nimeamua kutoa mawazo yangu kupitia kwenye ukumbi huu. Kwa wale wasionifahamu mimi ni Mansoor Yussuf Himid nimezaliwa Novemba 3 mwaka 1967 Kisiwa cha Unguja ni Mzanzibari kwa mama na baba, kama walivyo Wazanzibari wengine wazee wangu wana asili ya pande mbili Bara na Arabuni. Baba yangu mzazi ana asili ya Bara ambapo upande wa baba ni mnyasa na upande wa mama ni mmanyema na mama ana asili ya Arabuni (Oman), lakini ni mseto wa aina yake maana anadamu ya Ki-manyema,ki-somali,ki-ngazija, hali hii si ya ajabu kwa Wazanzibari bali ni kawaida tu na ndio hali inayo tutambulisha Wazanzibari.

Mimi ni Mtanzania kama walivyo wazee na ndugu zangu na wanangu na mke wangu Asha Abeid Amani Karume, kama unajiuliza Karume yupi ni huyo huyo unayemfikiria wewe ni Marehemu Abeid Amani Karume, Baba wa Taifa la Zanzibar , mungu amlaze pema peponi na amsamehe kwa mapungufu yake na amjaalie aendelea kutajwa kwa kheri na wema kama anavyo tajwa sasa.

Marehemu mzee Karume ana haki ya kuitwa Baba wa Taifa la Tanzania pia na wala mshishangae kwani Marekani Taifa la kupigiwa mfano kwa historia na misingi yake imara ya haki za binadamu,demokrasia na utawala bora , wana baba wa Taifa (Founding fathers) zaidi ya mmoja.

Kwa wengine nikiwemo mie kutothaminiwa kwa marehemu Bwana Abeid Amani Karume kwa kuitwa muasisi tu tena wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wala sio Nchi au Taifa la Zanzibar au Tanzania ni kutothamini mchango wake katika kuasisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani bila ya Zanzibar hakuna Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni sehemu ya kero za Muungano wetu.

Tuelewe kuwa kwa kumthamini marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, hatuondoshi nafasi ya Marehemu Mwalimu Julius kambarage Nyerere hata kidogo,nafasi ya Mwalimu ni kubwa mno (iconic) kwa wengine iliotukuka (saintly) sio tu kwa Tanzania na Afrika bali mwenyezi mungu amemjaalia Mwalimu kuthaminiwa na kupendwa na mataifa duniani kote,mpaka hii leo miaka kadha baada kufariki kwake, sababu za kupendwa kwa Mwalimu akiwa miongoni mwa viongozi wachache duniani wenye hadhi kama yake ni nyingi kwa leo si dhamira yangu kueleza wasifu wa Marehemu Mwalimu Nyerere
 
  • Thanks
Reactions: OTG
Sasa Bw. Mansour tufanyeje ? Tumekusikia wewe ni mtanzania mwenye asili ya Oman na umeoa mtoto wa Karume.So what ? au Kuoa mtoto wa Karume ni prestige ? Utambulisho huu kwetu watannzania masikini unatusaidia nini sisi ? au huko zanzibar husikiki tena kwa hiyo unaanza kujinasibu na unyasa , ubara na kuoa kwa kwa Rais ?
 
Back
Top Bottom