Mawardat
JF-Expert Member
- Apr 27, 2021
- 25,857
- 136,481
Mie na siasa wapi na wapš¤£Nawe kachukue fomu
Mie mshabiki maandazi TUš
Mie na siasa wapi na wapš¤£Nawe kachukue fomu
Sio sbb , makonda wa wapi?Mtoto wa Jennista hana nafasi ya kushinda hiyo nafasi labda hao Kamati Kuu ya CCM wampitishe kwa lazima.
Peramiho siyo kwao, kwao ni Mbinga alikozika mama yake na baba yake.
Muambieni ajiandae kisailolijia, yale maneno ya akina Spika Zungu yalikuwa story za msibani tu
Atashinda mpende msipende..Mtoto wa Jennista hana nafasi ya kushinda hiyo nafasi labda hao Kamati Kuu ya CCM wampitishe kwa lazima.
Peramiho siyo kwao, kwao ni Mbinga alikozika mama yake na baba yake.
Muambieni ajiandae kisailolijia, yale maneno ya akina Spika Zungu yalikuwa story za msibani tu
Tz hakuna uchaguziVictor Mhagama, mtoto wa marehemu Jenista Mhagama, amejitosa kuwania kurithi nafasi ya ubunge ya Peramiho iliyoshikiliwa na mama yake kwa zaidi ya miaka 20 kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hatua hiyo inamfanya Victor kuingia katika orodha ya watoto wa vigogo kadhaa wa siasa ndani ya chama hicho waliojitosa kuwania kurithi majimbo ya wazazi wao waliopofariki dunia.
Miongoni mwa watoto hao, yumo Omar Kigoda, aliyewahi kuchukua fomu kuwania ubunge wa Handeni, baada ya baba yake, Abdallah Kigoda, kufariki dunia akiwa mbunge wa jimbo hilo.
Mwingine ni Goodluck Mtinga, mtoto wa kwanza wa marehemu Celina Kombani, aliyewania ubunge wa jimbo la Ulanga Mashariki, baada ya kifo cha mama yake akiwa na wadhifa huo.
Vivyo hivyo, ilitokea kwa Geofrey Mgimwa, mtoto wa Dk William Mgimwa, aliyewania ubunge wa Kalenga baada ya baba yake kufariki dunia akiliongoza jimbo hilo.
Aidha, Salum Turky naye alijitosa kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo, baada ya baba yake, Turkey Taufiq, aliyekuwa Mbunge wa Mpendae, kufariki dunia.
Hata hivyo, Victor atachuana na makada wengine watano wa CCM, wakiwamo viongozi wa chama hicho Songea Vijijini, waliojitosa kuwania kuteuliwa kuwania ubunge katika jimbo hilo.
Dalili za uamuzi wa Victor kuwania nafasi hiyo ya kumrithi mama yake, zilionekana tangu siku ya ibada ya kuaga mwili wake iliyofanyika mkoani Ruvuma.
Spika wa Bunge, Mussa Zungu, alimpigia chapuo ingawa kwa mafumbo. āMkuu wa mkoa uko hapa, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi upo hapa, na nyota mtoto wetu (Victor) yupo hapa. Nafikiri nikisema hivyo mmenielewa. Mmenielewa?ā alisema Zungu.
Soma pia PostGE2025 - Ruvuma: Spika Mussa Zungu anataka mtoto wa Jenista Mhagama kupendekezwa Ubunge jimbo la Peramiho?
Kufanyika kwa mchakato huo wa uchukuaji na urejeshaji fomu katika jimbo hilo kunatokana na kubaki wazi kwa nafasi ya ubunge wa Peramiho tangu Jenista alipofariki dunia Desemba 11, mwaka jana.
Akizungumzia hilo leo Jumapili, Januari 18, 2026, Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini, Juma Nambaila, amesema uchukuaji na urejeshaji fomu umeanza leo Jumapili, Januari 18, na utafungwa kesho, Jumatatu, Januari 19.
Amewataja waliochukua fomu pamoja na Victor ni Emilly Ngaponda, Scholar Ngonyani, Clemence Makaburi, Allen Mhagama na Rosemery Mashauri.
Amewataka wanachama wenye sifa na nia ya kugombea kuzingatia maelekezo ya chama na kuhakikisha fomu zinarejeshwa ndani ya muda uliopangwa.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini, Schoral Daniel, amesema anaamini ana uzoefu kwenye uongozi.
Amesema analijua vema jimbo hilo kwa kuwa alishirikiana na Jenista kutatua kero za wananchi wa Peramiho, na hivyo anaamini atakuwa na uwezo wa kushughulikia changamoto zao kwa ufanisi.
Chanzo: Mwananchi
Bila shaka nitakuwa mlinzi wa dunia.Wewe utaishi milele?
Nimeshindwaaa mahii, ššššHaya mahiii nimetulia.
Na kapita kweli.Mbingaš
Huyo mtoto anapita bila kipingamizi.
Nilisema hawezi shindwa,maana walishapanga kumuweka,haya akae nae akifa atapokea mwanae,yaani ni mwendo wa kurithishana,,wengine wakalime mahindi.Na kapita kweli.
Poleee mahiii....Nimeshindwaaa mahii, šššš
Ahsanteee mahii, ššššPoleee mahiii....
Karibu wakati mwingine š
ššššš kwa kweli.Nilisema hawezi shindwa,maana walishapanga kumuweka,haya akae nae akifa atapokea mwanae,yaani ni mwendo wa kurithishana,,wengine wakalime mahindi.
Technically hii ni pasi ya kisigino.
Nchimbi aliongoza Songea Mjini miaka 10 ni mzaliwa wa Songea? Wakati ni mmatengo wa Mbinga??
Joseph Mhagama aliongoza Madaba kwani mzawa wa kule? Wakati yeye ni mtu wa Manda Mbinga.
Victor anachukua hili jimbo.
Mtoto wa Jennista hana nafasi ya kushinda hiyo nafasi labda hao Kamati Kuu ya CCM wampitishe kwa lazima.
Peramiho siyo kwao, kwao ni Mbinga alikozika mama yake na baba yake.
Muambieni ajiandae kisailolijia, yale maneno ya akina Spika Zungu yalikuwa story za msibani tu
Bado unamtegemea huyu dogo Victor Mhagama ashinde??Sio sbb , makonda wa wapi?
Anyway, atapata sbb wameamua kumpa sio sbb ya wapiga kura
Njooni muangalie kama huyo mtoto wenu amepitaMbingaš
Huyo mtoto anapita bila kipingamizi.
Kapita wapi?Na kapita kweli.
Kwanza simjuiBado unamtegemea huyu dogo Victor Mhagama ashinde??
Kwani ulitaka wafuate mawazo yako?Kwanza simjui
Ila nilitoa maoni kutokana na huu upuuzi wa ccm kuamua wanachotaka