mtoto ni wa baba au ni wa mama?

mtoto ni wa baba au ni wa mama?

Fatma Bawazir

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2010
Posts
491
Reaction score
180
mume alimpa talaka mkewe wakaenda mahakamani ili mahakama iamue ni nani anapaswa kuishi na mtoto ?

MKE : akasema mtoto ni wakwangu kwa maana nilibeba mimba miezi 9 nikapata uchungu kujifungua na
kumyonyesha mtoto,

MUME: nae akasimama akauliza hivi nikichukua ATM card nikaingiza kwenye ATM
mashine ikatoa pesa sasa pesa zitakuwa ni za ATM au ni za kwangu?

wana jf hebu tusaidieni jibu hakimu aamue nini hapo
 
Jamaa alimujibu vizuri sana kwa kutumia mfano kwa makibila mengi nchini tanzania na tamaduni zao mtoto huwa ni wa baba isipokuwa kwa wachaga na wanyakusa mtoto huwa wa mama
 
jibu ni pesa ni za mwenye atm,ila benk ilisaidia kutunza.
 
Mtoto ni wa mama na mjomba sababu only them can be 100% sure they share the same blood na huyo mtoto.
Hujaona mtu anatumia ATM card ambayo sio yake? hizo pesa bado anaziita zake?
 
Mtoto ni mali ya Muumba siku yoyote akimwitaji hao wawili si wao
 
Mahakama bado inafikiri na kungoja ushauri wa wazee wa baraza wa JF.
 
FF bwana, nimecheka sana na majibu yako. Mtoto ni wa baba na mama, lakini kwa sababu ya ushetani wa kuachana bila hofu ya mungu kwamba hao watoto watanyanyasika ndiyo maana watu wazima tunabaki kusema eti ni wa baba au mama.Ikitokea mnaishi raha bila devil anaitwa talaka basi mtoto ni wa baba na mama.
 
Jamaa alimujibu vizuri sana kwa kutumia mfano kwa makibila mengi nchini tanzania na tamaduni zao mtoto huwa ni wa baba isipokuwa kwa wachaga na wanyakusa mtoto huwa wa mama

kwayati plizi,mbona wachaga kila inshu?a yuu kirezi?heey!amu askin yuu,answa mii,oke?
 
huyo baba nae ndo nini kutoa mafano kama hiyo?????hapo hakimu alikua na kazi ya ziada kidogo..............
 
Anyway;kibaiolojia mtoto ni wa baba na mama,tena nusu kwa nusu!
Peleka mada kwenye JF doktaz nitakujibu!!!!
Ila hapa kwenye jokes itoshe kusema hata kama mtu ameiba ATM card,bado pesa itakuwa ya mwenye ATM card!!!!!
 
Mtoto ni wa mama na mjomba sababu only them can be 100% sure they share the same blood na huyo mtoto.
Hujaona mtu anatumia ATM card ambayo sio yake? hizo pesa bado anaziita zake?

no no no, as far as know ni kwambwa anayeweka damu kwa mtoto ni baba na ndo maana DNA inapimwa kwa baba tu.
russianroulette umenidanganya.
 
no no no, as far as know ni kwambwa anayeweka damu kwa mtoto ni baba na ndo maana DNA inapimwa kwa baba tu.
russianroulette umenidanganya.

Kwanini DNA inapimwa kwa baba tu? ukipata jibu utajuwa mtoto ni wa nani.
 
Mtoto ni wa mama, Baba si mpaka awe wake, kama si wake jee? Kuna mwanamke nnamjuwa anakiri kabisa kuwa mwanae hajui babake nani kwani alikuwa na wanaume watatu na wote anatembea nao, alikuwa anataka kuhakikisha wa nani lakini anashindwa kuwaambia wale wanaume wakafanye DNA. Hapo sasa. Huo ndio ujira wa zinaa, amebaki mtoto hajui babake na ilhali wako hai.

Kwa hayo nahitimisha kuwa mtoto wa halali ni wa baba na mama, mtoto wa zinaa ni wa mama pekee.
 
Kwanini DNA inapimwa kwa baba tu? ukipata jibu utajuwa mtoto ni wa nani.
ndivyo ilivyo faiza kwa mama hakuna haja ya kupima ila kwa baba si unajua wengine wankataa watoto wao, any way mi
sio mtalaamu sana ila najua baba ndio anaweka damu kwa mtoto.
 
Mtoto ni wa mama na mjomba sababu only them can be 100% sure they share the same blood na huyo mtoto.
Hujaona mtu anatumia ATM card ambayo sio yake? hizo pesa bado anaziita zake?

Kibongobongo mtoto ni wa yule alielipa mahari, labda DNA mashine imzingue. Na akigundua alipwe fidia ya kuchakachuliwa kama huyo mwizi wa ATM card alivyoihadaa ATM MASHINE hadi ikakubali Likard liingia lifanye madudu yake na kutoa fedha haramu atakavyofanywa aki detectiwa.
 
Acheni uzushi tufanye uamuzi wa kibaologia baba kampa mama yai (x) likarutubishwa na (x) ya mama ya kaungana na kumtengeneza mtoto
so hakimu jibu rahisi tu mtoto ni wa wote baba na mama. Na huyo baba aliye uliza swali la atm muulize kama ela ni za kwake mbona kila akichanja atm card ina mchaji kiasi fulani kwan akieka 1000000 hatozitoa zote? So jibu ndo hilo anayepinga atoe vigezo stahiki
 
Mtoto wa wote wa baba na mama. Hakuna baba bila mama na hakuna mama bila ya baba. Tendo la uumbaji ni shirikishi. Angekuwa mtoto wa baba peke yake kama angekaa katika tumbo lake na angekuwa wa mama peke yake kama mtoto angepatikana bila ya kufanya tendo la ndoa na mumewe. wajamani mambo mazito haya tuheshimiane wake kwa waume kila mmoja wetu ni muhimu.
 
Back
Top Bottom