Mtoto kautaka: unakukumbusha nini?

Mtoto kautaka: unakukumbusha nini?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
368,210
Reaction score
851,785
Kesi maarufu ya "Wabakaji wa Dodoma" iliyohusisha binti wa miaka 17 kutoka Yombo Dovya, Dar es Salaam, ilihitimishwa kwa watuhumiwa wakuu kupatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Watuhumiwa hao walipatikana na hatia ya makosa ya kubaka kwa kundi na kulawiti.

Mruhumiwa mkuu alikuwa NYUNDO

 
Its mshana again

Cc Smart911
Basi nasusa kupost
1779639162822.jpg
 
Clinton Damas, anayefahamika zaidi kama "Nyundo," alikata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga hukumu ya kifungo cha maisha jela.Alifungwa maisha na wenzake watatu—
Amin Lema (Kindamba), Nickson Jackson
(Machuche), na
Praygod Mushi—baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumwingilia kinyume na maumbile binti mmoja mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.

Rufaa yao ilianza kusikilizwa Juni 2025 mbele ya Jaji Amir Mruma, na Mahakama ilipanga kutoa uamuzi wake mnamo Oktoba 2025.
 
Hata hivyoClinton Damas (maarufu kama Nyundo) na wenzake hawakushinda rufaa yao kwa maana ya kuachiwa huru.

Mahakama Kuu ilitoa uamuzi ufuatao kuhusu rufaa yao:

Kosa la Kulawiti:
Mahakama ilikubali rufaa yao na kufuta shtaka la kulawiti kwa kundi (kwa sababu kosa hilo halikutambulika kisheria jinsi lilivyofunguliwa).

Kosa la Kubaka:
Mahakama ilitupilia mbali rufaa yao na kubariki hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka kwa kikundi.

Kwa matokeo haya, Nyundo pamoja na wenzake watatu (Amin Lema 'Kindamba', Nickson Jackson 'Machuche', na Praygod Mushi) wataendelea kutumikia kifungo cha maisha gerezani.
 
Connection ya Gigy money
Gigy Money Amekanusha: Katika mahojiano mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kama TikTok na Instagram, msanii huyo ameweka wazi kuwa video chafu zinazosambazwa sio zake na wala hafanani na mtu aliyemo kwenye video hizo.
 
Walichomfanyia Yule binti ndio situation anayokutana nayo mtu anayeingia mikononi mwa wasiojulikana, ukisalimika Sana ndo wanakutupa porini ukiwa hai au somewhere wakati huo tayari washakuvuruga mitambo ya sehemu za siri vibaya, hawana cha jinsia...wako watoto wa mbwa wanaojiita wazazi but wanafanya hizo kazi.
 
Walichomfanyia Yule binti ndio situation anayokutana nayo mtu anayeingia mikononi mwa wasiojulikana, ukisalimika Sana ndo wanakutupa porini ukiwa hai au somewhere wakati huo tayari washakuvuruga mitambo ya sehemu za siri...
 
Back
Top Bottom