Mtoto katika ndoa hudumisha mahusiano?

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
29,047
10,695
Nina jamaa zangu wawili ambao wako kwenye ndoa, mmoja ni zaidi ya miaka tisa,lakini hawajafanikiwa kupata mtoto.Japo hawasemi lakini kwa kuwatazama na jinsi watu wanavyonong'ona penbeni inaonyesha kabisa hawako happy kwenye ndoa zao.Je ni kweli kwamba mkipata mtoto huifanya ndoa yenu iwe imara zaidi?Mi binafsi nachukulia kama mipango ya Mungu tu, labda watafanikiwa mbele ya safari.
 
ni kweli mtoto ktk ndoa ni mipango ya mungu, lakini kwa namna nyingine mtoto huzidisha furaha ktk ndoa. kuna jamaa yangu waligombana na mkewe walikaa siku nne bila kusemeshana, sasa wana mtoto wao miaka 5 akawa amejua kuwa baba na mama hawasemi, siku hiyo jioni wamerudi tu mtt akawadaka leo tuna kikao mniambie nani mchokozi kamchokoza mwenzake ili nimchape fimbo, wkt huo kanasema kameshika bakora mkononi. jamaa na mkewe walicheka sana na yakawa yamekwisha.
 
Unapooa tegemea yote mawili kupata mtoto au kutopata mtoto mapema. haijalishi ni nani ana matatizo maana matatizo yako pande zote siku hizi. Ukifanikiw akupata mtoto ni jambo la kumshukuru Mungu. Ila kuna ndoa ambazo ni imara japo hawajafanikiwa kupata mtoto na hawaoni hilo ni tatizo maana mtoto ni mipango pia ya Mungu. Ni kweli ni furaha sana kuwa na mtoto na nakiri ni kiunganishi kizuri sana kwenye ndoa. Ni raha sana kwa wanandoa mnapoona mtoto anazaliwa, anakua, na mabadiliko mbalimbali kwa mtoto. Na vile vile hata kama ni mdogo hajaelewa lolote mkigombana ndani ya nyumba anaelewa kabisa kuwa baba na mama hawako sawa.
 
watoto wana raha yake kwa kweli,kuna siku mtoto wangu wa miezi kadhaa aliniona nikilia huku nimempakata baada ya baba yake kuniudhi sana(nilishindwa kujizuia kulia japokuwa nilikuwa nimebeba mtoto) akaniangaliaaaaa.......then akachukua kitambaa nilichokuwa nimemshikia akanipangusa machozi daaaah yani nilihisi furaha ya ajabu na nikaacha kulia nikamshangaa Mungu!! watoto wanaleta furaha kwenye ndoa.
 
ni kweli mtoto ktk ndoa ni mipango ya mungu, lakini kwa namna nyingine mtoto huzidisha furaha ktk ndoa. kuna jamaa yangu waligombana na mkewe walikaa siku nne bila kusemeshana, sasa wana mtoto wao miaka 5 akawa amejua kuwa baba na mama hawasemi, siku hiyo jioni wamerudi tu mtt akawadaka leo tuna kikao mniambie nani mchokozi kamchokoza mwenzake ili nimchape fimbo, wkt huo kanasema kameshika bakora mkononi. jamaa na mkewe walicheka sana na yakawa yamekwisha.

Dah hii kali mkuu.
 
Kweli...watoto wana nafasi yao kubwa tuu katika ndoa....kwakila hatua ya mtoto ya ukuaji wake ni faraja kwa wazazi wake...wanafurahisha sana sana.. na kuwaleta pamoja zaidi wazazi.....hii ni kwa wale wazazi wanaojua majukumu yao sio kila mzazi
 
kama ulioa,upate watoto,usipowapata ndoa yako itakuwa mashakani....ila kama uliingia ndoani out of love ukijua watoto ni matokeo tu hata usipowapata ndoa yako haitayumba!
 
Hata wanaooana kwa upendo kukosa mtoto bado ni mtihani sema wao tofauti na wasio na upendo ni kuwa varangati lao litatokea baadae sana. Ni ngumu watu wakae for 20 years bila mtoto tena kwa amani. Inawezekana wapo ila ni ngumu. Na si kwa mume tu hata wife anaweza kuanzisha vituko including kununa, kutokuwa na raha ambavyo vyote ni sumu ya ndoa.
kama ulioa,upate watoto,usipowapata ndoa yako itakuwa mashakani....ila kama uliingia ndoani out of love ukijua watoto ni matokeo tu hata usipowapata ndoa yako haitayumba!
 
uhusiano wa furaha na maridhiano ndani ya familia mtoto ana nafasi ndogo sana............................wazazi kamwe hawawezi kukubali mtoto awafanye wao kuwa jela ya kuamua kuishi pamoja au la..............................................mahusiano kati ya wahusika wenywe tu yanajitosheleza.................au vinginevyo vile..............................................
 
<br />
<br />
Well said!!
 
Back
Top Bottom