Mtoto huyu anateseka, msaidieni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto huyu anateseka, msaidieni!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Michael Amon, Apr 8, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Mtoto Farid Rashid mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 8 anasumbuliwa na tatizo la kuziba kwa mirija inayosafirisha haja ndogo( mkojo) kati ya Figo na Kibofu cha mkojo.

  [​IMG]

  Baba Mzazi (Rashid Said) wa mtoto huyo anawaomba msaada wadau mbalimbali ili aweze kumpeleka mtoto Farid nchini India kwa matibabu zaidi.

  "Mwanangu anajisaidia kwa maumivu makali, sema kweli ni mateso makubwa kwa mtoto, naomba mnisaidie mwanangu apate matibabu" hayo ni maneno ya baba mzazi wa Farid (Rashid Said).

  Akizungumza hivi karibuni Baba Mzazi Rashid Said amesema amemzungusha kwa matibabu mtoto Farid katika hospital mbalimbali za hapa nchini bila mafanikio ikiwa ni pamoja na kulazwa zaidi ya miezi mitatu(3) katika hospitali ya taifa ya Muhibili.

  Katika juhudi za wazazi wa Farid kutafuta misada, wamefanikiwa kupata tiketi moja (1) ya ndege, dola 1,500 pamoja na Shilingi Milioni moja (1) lakini bado haitoshi.

  Hata hivyo tayari wamefanikiwa kupata hati za kusafiria (Passport) na VISA ya nchini India ambayo inakoma (expire) 19-06-2012.

  Hivyo anaomba msaada wa kupata tiketi nyingine pamoja na gharama za matibabu.

  Nambari ya simu ya baba mzazi ni 0655-000556
   
 2. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Mkuu ni bora itafutwe njia mbadala ya kumsaidia bcoz siku hizi matapeli kibao,binafsi nimeguswa na ninamchango wangu wa tsh 10,000.But I can't call,i can't send money simple like that,ngoja nitulie niangalie njia mbadala ya yeye kupata msaada bila watu kua na shaka.
  Ntarudi punde!!
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Poa mkuu. Nimekupata.
   
 4. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Nimerudi mkuu!
  Afanye haya yafuatayo:
  1.Hiyo picha hapo juu itumike na itafutwe picha nyingine ya mtoto iwekwe pia.
  2.Aweke passports copy hapa na visa copy
  3.Aweke transifer details zote-bank na other transifer details kama makampuni ya simu yani Tigo pesa,m pesa,airtel money.
  4.Physical address zake ni muhimu sana.
  5.Baadhi ya vyeti vya hospital alivyotumia muhimbili.
  6.Barua ya kuthibitisha kwamba anatakiwa kwenda india.
  7.Barua ya serikali za mitaa kuthibitisha uhalali wa makazi yake.
  8.Kiasi kinachohitajika.
  Kwa vielelezo hivyo vichache natumai atapata msaada wa faster sana.
  Kwa kumalizia ningependa kujua mchango wangu wa tsh10,000 ntauwakilisha vp?
  Poleni kwa matatizo na inshaallah allah atampa mgonjwa siha njema soon.
  Wabilah tawfiq!
  Aslm alykm.
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Apr 9, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Poa. Ngoja nitawasiliana naye nione kama kuna uwezekano wa kuweka hizo details zake hapo ili asije akatuibia. Shukrani sana kwa wazo lako zuri mkuu.
   
Loading...