DOKEZO Mtoto Huyu ananyanyasika kingono

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,253
Ni Binti wa umri wa miaka 11 ambae yupo darasa la tano.

Binti huyu pamoja na umri wake mdogo lakini ameeathirika sana kisaikolojia kutokana na kutumika kingono kutoka kwa vijana wenye umri mkubwa.

Binti huyu mamake aliachana na Baba yake na kwenda kuolewa sehemu nyingine na kumuacha binti akiwa na Baba yake, kutokana na tabia ya baba yake ya ulevi na kutojitambua na kushindwa kumlinda mtoto wake huyo vijana walevi wa mtaani wakaanza kutumia mtoto huyo kingono tangu akiwa na umri wa miaka 9.

Mama mmoja jirani ambae pia ni mjane aliamua kumchukua mtoto huyo na kuishi nae japo kwa tabu kutokana na kwamba huyo mama ni mlevi na hana kipato maalumu zaidi ya vibarua vya hapa na pale.

Kilichonisikitisha ni baada ya kumuona binti huyo mdogo na pia mwenye umbo dogo kabisa ambae vijana wanamrubuni kwa kumpa kiasi cha shilingi 100, na sh 200 baada ya tendo.

Ilibidi niulizie kwanini mtoto huyo mdogo afanyiwe vitendo hivyo kila wakati tena kwa kujirudia? Ndipo nikaelezwa kuwa mtoto huyo hayupo sawa sawa kichwani.

Kuhusiana na swala la polisi kesi zilishapelekwa huko na inajulikana

Mwisho wa huyu mtoto utakuwaje?

Nimeshindwa kuweka picha ya mtoto ili kulinda maadili. Na utu wa mtoto
 
Umeshindwaje kujitolea kumlea huyo mtoto?
Sasa huku sisi tufanyeje?
Kumbuka ww ni mzazi pia
Sisi tunasaidia tulionao around
Na ww pia jitahidi kusaidia
 
hongera kwa kuchukua hatua hata hii ya kupaza sauti......

nakushauri toa mawasiliano ambayo wahusika wanaweza kukutafuta na kupata msaada zaidi wa kumsaidia mtoto......
 
Ni Binti wa umri wa miaka 11 ambae yupo darasa la tano.

Binti huyu pamoja na umri wake mdogo lakini ameeathirika sana kisaikolojia kutokana na kutumika kingono kutoka kwa vijana wenye umri mkubwa.

Binti huyu mamake aliachana na Baba yake na kwenda kuolewa sehemu nyingine na kumuacha binti akiwa na Baba yake, kutokana na tabia ya baba yake ya ulevi na kutojitambua na kushindwa kumlinda mtoto wake huyo vijana walevi wa mtaani wakaanza kutumia mtoto huyo kingono tangu akiwa na umri wa miaka 9.

Mama mmoja jirani ambae pia ni mjane aliamua kumchukua mtoto huyo na kuishi nae japo kwa tabu kutokana na kwamba huyo mama ni mlevi na hana kipato maalumu zaidi ya vibarua vya hapa na pale.

Kilichonisikitisha ni baada ya kumuona binti huyo mdogo na pia mwenye umbo dogo kabisa ambae vijana wanamrubuni kwa kumpa kiasi cha shilingi 100, na sh 200 baada ya tendo.

Ilibidi niulizie kwanini mtoto huyo mdogo afanyiwe vitendo hivyo kila wakati tena kwa kujirudia? Ndipo nikaelezwa kuwa mtoto huyo hayupo sawa sawa kichwani.

Kuhusiana na swala la polisi kesi zilishapelekwa huko na inajulikana

Mwisho wa huyu mtoto utakuwaje?

Nimeshindwa kuweka picha ya mtoto ili kulinda maadili. Na utu wa mtoto
Honhera kwa uwajibikaji.

Ni jambo jema kuchukua hatua stahiki kuhusu jambo hili ambalo halikubaliki katika zama hizi za dunia iliyostaarabika.

Fikisha taarifa hizi ustawi wa jamii, ama kituo cha polisi kilicho karibu nawe.

Hakika kupitia uwajibikaji kama huo tunaweza kutokomeza vitendo hivi vya unyanyasaji katika jamii tunazoishi.

Ahsante
 
Back
Top Bottom