Mtoto genius

ora

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,198
1,122
Mtoto: Mwalimu mimi nataka
nisome darasa la 4 kwani hili la 2 halinifai.
Mwalimu: Kwa nini unasema hivo?
Mtoto: Nina akili...
Basi mwalimu kamueleza mkuu wa shule na mkuu kaitisha interview kwa dogo. Maswali ni haya....
Mwalimu: Kwenye ndege kuna matofali 157 tukitoa moja tukalidondosha chini yatabaki mangapi?
Dogo: Yatabaki 156.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka tembo
kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamuweka tembo kisha unafunga.
Mwalimu: Nipe hatua za kumuweka nyani
kwenye friji.
Dogo: Unafungua friji unamtoa tembo ulemuweka..unamueka nyani kisha unafunga friji.
Mwalimu: Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa simba, wanyama wote wameenda kasoro mmoja. Ni nani na kwa nini?
Dogo: Ni nyani kwa sababu tumemuweka
kwenye friji.
Mwalimu: Bibi kizee amevuka mto unaokuwaga na mamba na viboko wakali, aliwezaje?
Dogo: Aliweza kwani mamba na viboko nao walienda kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa simba.
Mwalimu: Ingawa bibi kizee alivuka mto, baadae alikufa. Unadhani kwa nini?
Dogo: Alidondokewa na lile tofali tulotoa kwenye ndege na kutupa chini.
Mwalimu mkuu: Mwalimu "Huyu Mtoto
akasome UDOM........"
 
Hey! that's a creativity test for real naona umei"twist" kidogo imekuwa joke hiyo test inadhihirisha namna gani creativity ya mtu inapungua kadri anavyopata elimu ya darasani the test was challenging for a corporate CEO and easy for a 5year old.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom