Mtoto atolewa Shanga kwenye Mapafu bila upasuaji Muhimbili Hospitali

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1705410176645.png

1705410189070.png

1705410197659.png

Wazazi wameaswa kufuatilia michezo ya watoto kwa karibu zaidi na kuwazuia kuweka vitu mdomoni, puani pamoja na masikioni ili kuwaepusha na madhara mbalimbali ikiwemo madhara ya kudumu na kifo.

Kauli hiyo imetolewa na Jopo la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo, Mapafu na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao wameshiriki kuondoa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Daktari Bingwa wa Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dkt. Mwanaada Kilima amesema, shanga hiyo iliingia kwenye pafu baada ya kumpalia mtoto alipokuwa akiichezea mdomoni takribani mwezi mmoja uliopita.

Dkt. Kilima amesema mtoto huyo alitaabika tangu wakati huo kwa kikohozi na kupumua kwa shida huku njia mbalimbali zikitumika kujaribu kuitoa na kugonga mwamba, ndipo wataalamu wa mapafu walipofanikiwa kuitoa bila madhara yoyote.

“Tulitumia mpira laini wenye kamera ya video ya mapafu (Flexible bronchoscope) na kifaa cha kukamatia (foreign body basket) na kufanikiwa kuitoa hivyo kumwepusha na upasuaji mkubwa ambao ungesababisha ama kutoa pafu au sehemu ya pafu” amesema Dkt. Kilima.

Dkt. Ramadhan Hamis, Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo ndiye aliyeoongoza jopo hilo kwa kushirikiana na Dkt. Charles Komba Bingwa wa Upasuaji Kifua pamoja na Dkt. Mwanaada Kilima Bingwa wa Mapafu na Mfumo wa Upumuaji.
 
Ndugu Zungu watanzania,

Tunaposema humu jukwaani kila siku kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu,imara na madhubuti wa Rais Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nuru ya wanyonge na nyota ya matumaini kuwa amefanya uwekezaji mkubwa katika Secta ya Afya tutaanza kueleweka vyema kwa sasa.

Hii ni baada ya jopo la madaktari bingwa wa kitanzania kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanya jambo la kishujaa na kupongezwa kabisa la kumtoa shanga katika pafu aliyokuwa ameimeza mtoto wa miaka mitano mwezi mmoja uliopita. Ambapo mtoto huyo aliimeza shanga hiyo kwa bahati mbaya baada ya kupaliwa wakati akiichezea mdomoni.

Shanga hiyo imetolewa kihodari na kitaalamu sana na kwa teknolojia ya hali ya juu sana mpaka unaweza fikiri kuwa zoezi hilo limefanyika kule Washington DC marekani kumbe ni hapa hapa katika ardhi ya Rais Mama Samia kipenzi cha watanzania wote wenye akili Timamu na wanaojitambua.

Ambapo madaktari hao wameeleza kuwa kama kusingefanyika utaalamu huo na kwa teknolojia hiyo ya hali ya juu ambapo waliingiza kifaa chenye camera na chenye uwezo wa kuinasa shanga hiyo basi ingelazimika kumfanyia upasuaji mkubwa ambao ungepelekea mambo mengine kama vile kutoa pafu au sehemu ya pafu na hivyo kuleta pancha kwa mtoto.

Madaktari hao jasiri na wenye mioyo ya kizalendo na wito wa kazi na wenye kuipenda kwa dhati kazi yao wametoa Rai kwa jamii kuwachunga vyema watoto hasa wanapokuwa wanacheza wenyewe au wanachezea vitu ,ili wasipeleke mdomoni na kumeza kwa bahati mbaya vitu wanavyochezea.

Haya yanafanyika huku Rais Samia akiwa tayari amewekeza na kutiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya afya kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya hospitali pamoja na kununua vifaa tiba,kusomesha wataalumu kama vile madaktari bingwa,kununua madawa na mambo mengine mengi sana. Ingekuwa zamani huko ungeshangaa mtoto huyu anaombewa michango kupitia vyombo vya habari kwa ajili ya kupelekwa Apollo India Lakini kwa sasa ni kama Apollo imehamia Muhimbili kwa kuwa huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini.ndio maana tunaona hata majirani zetu wanakimbilia Muhimbili na hospitali zingine zilizopo hapa nchini kupata matibabu .ambapo kwa mwaka jana zaidi ya mamia ya wagonjwa kutoka nje ya nchi walitibiwa hapa nchini .

Hongera sana madaktari wetu kwa kazi nzuri na ya kizalendo mnayoendelea kuifanya kuokoa maisha ya watanzania.chapeni kazi kwa moyo wenu wote na Mungu atawalipa kwa kazi yenu hiyo njema kabisa kwa watanzania. tunawapenda sana madaktari wetu na tunawaheshimuni sana. Mungu awe nanyi na awabariki sana.najuwa changamoto kama za kimaslahi huwa hazikosekani lakini muwe na subira na uvumilivu kwa kuwa Rais wenu na wetu Mh Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan ni mama wa upendo na huruma na anatambua kazi kubwa mnayoendelea kuifanya katika kujenga Taifa la watu wenye afya njema na nguvu,na hivyo ataendelea kuwaboresheeni marupurupu na maslahi yenu kwa kadri hali ya uchumi inavyoruhusu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Ndugu Zungu watanzania,

Tunaposema humu jukwaani kila siku kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu,imara na madhubuti chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nuru ya wanyonge na nyota ya matumaini kuwa amefanya uwekezaji mkubwa katika Secta ya Afya tutaanza kueleweka vyema kwa sasa.

Hii ni baada ya jopo la madaktari bingwa wa kitanzania kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanya jambo la kishujaa na kupongezwa kabisa la kumtoa shanga katika pafu aliyokuwa ameimeza mtoto wa miaka mitano mwezi mmoja uliopita. Ambapo mtoto huyo aliimeza shanga hiyo kwa bahati mbaya baada ya kupaliwa wakati akiichezea mdomoni.

Shanga hiyo imetolewa kihodari na kitaalamu sana na kwa teknolojia ya hali ya juu sana mpaka unaweza fikiri kuwa zoezi hilo limefanyika kule Washington DC marekani kumbe ni hapa hapa katika ardhi ya Rais Mama Samia kipenzi cha watanzania wote wenye akili Timamu na wanaojitambua. Ambapo madaktari hao wameeleza kuwa kama kisingefanyika utaalamu huo na kwa teknolojia hiyo ambapo waliingiza kifaa chenye camera na chenye uwezo wa kuinasa changa hiyo basi ingelamika kumfanyia upasuaji mkubwa ambao ungepelekea mambo mengine kama vile kutoa pafu au sehemu ya pafu na hivyo kuleta pancha kwa mtoto.

Madaktari hao jasiri na wenye mioyo ya kizalendo na wito wa kazi na wenye kuipenda kwa dhati kazi yao wametoa Rai kwa jamii kiwachunga vyema watoto hasa wanapokuwa wanachezea vitu ,ili wasipeleke mdomoni na kumeza kwa bahati mbaya.

Haya yanafanyika huku Rais Samia akiwa tayari amewekeza na kutiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya afya kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya hospitali pamoja na kununua vifaa tiba,kusomesha wataalumu kama vile madaktari bingwa,kununua madawa na mambo mengine mengi sana. Ingekuwa zamani huko ungeshangaa mtoto huyu anaombewa michango kwa ajili ya kupelekwa Apollo India Lakini kwa sasa ni kama Apollo imehamia Muhimbili .

Hongera sana madaktari wetu kwa kazi nzuri na ya kizalendo mnayoendelea kuifanya kuokoa maisha ya watanzania.chapeni kazi kwa moyo wenu wote na Mungu atawalipa kwa kazi yenu hiyo njema kabisa kwa watanzania.tunawapenda saba madaktari wetu na tunawaheshimuni sana. Mungu awe nanyi na awabariki sana.najuwa changamoto kama za kimaslahi huwa hazikosekani lakini muwe na subira na uvumilivu kwa kuwa Rais wenu na wetu Mh Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan ni mama wa upendo na huruma na anatambua kazi kubwa mnayoendelea kuifanya katika kujenga Taifa la watu wenye afya njema na nguvu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Mama ndo ameitoa hiyo shanga?
 
Hii leo itakuwa habari ya mjini utadhani katolewa na mganga wa kienyeji anajitangaza. Wenzetu wanatoa vitu vikubwa sisi shanga ndiyo habari ya kuu tena hosp ya Taifa utadhani ni zahanati imefanya hilo tendo kumbe angeenda kwa babu akatapishwa na shanga ingetoka.
Acha wivu wako wewe mdogo wangu .uwe na moyo wa uungwana wa kupongeza pale mazuri yanapofanyika katika Taifa letu na siyo kutamani mazuri yatokee kwa wengine halafu kwetu yatokee na kufanyika mabaya tu. hiyo inakuwa ni roho ya kichawi na kishetani.
 
Kwamba shanga ni jambo kubwa sn, watoto wangapi wamewahi kumeza shs mia, 50 n.k wanaachwa wakienda haja kubwa zinatoka?
 
View attachment 2873546
View attachment 2873547
View attachment 2873548
Wazazi wameaswa kufuatilia michezo ya watoto kwa karibu zaidi na kuwazuia kuweka vitu mdomoni, puani pamoja na masikioni ili kuwaepusha na madhara mbalimbali ikiwemo madhara ya kudumu na kifo.

Kauli hiyo imetolewa na Jopo la Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo, Mapafu na Mfumo wa Upumuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao wameshiriki kuondoa shanga ya plastiki iliyokuwa imekwama katika pafu la kulia la mtoto mwenye umri wa miaka mitano.

Daktari Bingwa wa Mapafu na Mfumo wa Upumuaji, Dkt. Mwanaada Kilima amesema, shanga hiyo iliingia kwenye pafu baada ya kumpalia mtoto alipokuwa akiichezea mdomoni takribani mwezi mmoja uliopita.

Dkt. Kilima amesema mtoto huyo alitaabika tangu wakati huo kwa kikohozi na kupumua kwa shida huku njia mbalimbali zikitumika kujaribu kuitoa na kugonga mwamba, ndipo wataalamu wa mapafu walipofanikiwa kuitoa bila madhara yoyote.

“Tulitumia mpira laini wenye kamera ya video ya mapafu (Flexible bronchoscope) na kifaa cha kukamatia (foreign body basket) na kufanikiwa kuitoa hivyo kumwepusha na upasuaji mkubwa ambao ungesababisha ama kutoa pafu au sehemu ya pafu” amesema Dkt. Kilima.

Dkt. Ramadhan Hamis, Bingwa wa Upasuaji wa Kifua na Moyo ndiye aliyeoongoza jopo hilo kwa kushirikiana na Dkt. Charles Komba Bingwa wa Upasuaji Kifua pamoja na Dkt. Mwanaada Kilima Bingwa wa Mapafu na Mfumo wa Upumuaji.
Hongera kwa Madaktari waliohusika - Mungu awabariki kwa kazi mliyofanya na awazidishie neema zake tele.
 
Ni kazi yao waache wafanye
Uwe muungwana na mwenye moyo wa kupongeza.kwani wangapi wanashindwa kutekeleza majukumu yao licha ya kuwa ni kazi zao? Kwani wangeshindwa kumuokoa na kumtoa huyo mtoto hiyo shanga mpaka akapoteza maisha unafikiri ungewafanya nini watakapokwambia wamepambana lakini wameshindwa kuokoa maisha ya mtoto? Kwanini watanzania baadhi yenu mnakuwa na wivu sana mazuri yanapofanyika hapa nchini? Kwanini mnataka mazuri yawe kwa majirani pekee na siyo hapa? Vipi tukio hilo lingefanyika kenya? Si mngekuja na midomo yenu kutoa pongezi na kubeza wataalamu wetu?
 
Ndugu Zungu watanzania,

Tunaposema humu jukwaani kila siku kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu,imara na madhubuti wa Rais Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nuru ya wanyonge na nyota ya matumaini kuwa amefanya uwekezaji mkubwa katika Secta ya Afya tutaanza kueleweka vyema kwa sasa.

Hii ni baada ya jopo la madaktari bingwa wa kitanzania kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanya jambo la kishujaa na kupongezwa kabisa la kumtoa shanga katika pafu aliyokuwa ameimeza mtoto wa miaka mitano mwezi mmoja uliopita. Ambapo mtoto huyo aliimeza shanga hiyo kwa bahati mbaya baada ya kupaliwa wakati akiichezea mdomoni.

Shanga hiyo imetolewa kihodari na kitaalamu sana na kwa teknolojia ya hali ya juu sana mpaka unaweza fikiri kuwa zoezi hilo limefanyika kule Washington DC marekani kumbe ni hapa hapa katika ardhi ya Rais Mama Samia kipenzi cha watanzania wote wenye akili Timamu na wanaojitambua.

Ambapo madaktari hao wameeleza kuwa kama kusingefanyika utaalamu huo na kwa teknolojia hiyo ya hali ya juu ambapo waliingiza kifaa chenye camera na chenye uwezo wa kuinasa shanga hiyo basi ingelazimika kumfanyia upasuaji mkubwa ambao ungepelekea mambo mengine kama vile kutoa pafu au sehemu ya pafu na hivyo kuleta pancha kwa mtoto.

Madaktari hao jasiri na wenye mioyo ya kizalendo na wito wa kazi na wenye kuipenda kwa dhati kazi yao wametoa Rai kwa jamii kuwachunga vyema watoto hasa wanapokuwa wanacheza wenyewe au wanachezea vitu ,ili wasipeleke mdomoni na kumeza kwa bahati mbaya vitu wanavyochezea.

Haya yanafanyika huku Rais Samia akiwa tayari amewekeza na kutiririsha zaidi ya Trilioni sita katika Secta ya afya kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya hospitali pamoja na kununua vifaa tiba,kusomesha wataalumu kama vile madaktari bingwa,kununua madawa na mambo mengine mengi sana. Ingekuwa zamani huko ungeshangaa mtoto huyu anaombewa michango kupitia vyombo vya habari kwa ajili ya kupelekwa Apollo India Lakini kwa sasa ni kama Apollo imehamia Muhimbili kwa kuwa huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini.ndio maana tunaona hata majirani zetu wanakimbilia Muhimbili na hospitali zingine zilizopo hapa nchini kupata matibabu .ambapo kwa mwaka jana zaidi ya mamia ya wagonjwa kutoka nje ya nchi walitibiwa hapa nchini .

Hongera sana madaktari wetu kwa kazi nzuri na ya kizalendo mnayoendelea kuifanya kuokoa maisha ya watanzania.chapeni kazi kwa moyo wenu wote na Mungu atawalipa kwa kazi yenu hiyo njema kabisa kwa watanzania. tunawapenda sana madaktari wetu na tunawaheshimuni sana. Mungu awe nanyi na awabariki sana.najuwa changamoto kama za kimaslahi huwa hazikosekani lakini muwe na subira na uvumilivu kwa kuwa Rais wenu na wetu Mh Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan ni mama wa upendo na huruma na anatambua kazi kubwa mnayoendelea kuifanya katika kujenga Taifa la watu wenye afya njema na nguvu,na hivyo ataendelea kuwaboresheeni marupurupu na maslahi yenu kwa kadri hali ya uchumi inavyoruhusu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Duh,
Mzee una shida, heb jichunguze
 
Back
Top Bottom