Madaktari Muhimbili wamtoa mtoto kipande cha plastiki kwenye mapafu alichoishi nacho miezi 23

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanikiwa kutoa kipande cha plastiki kwenye pafu la kushoto la mtoto mwenye umri wa miaka 11, kupitia kifaa maalumu kinachoitwa Flexible Bronchoscopy.

Kifaa hicho kinatumia mpira laini wenye kamera ya uchunguzi wa mapafu bila kuhitaji mgojwa kupewa dawa za using ili.

Akizungumza kwa niaba ya timu ya watalaam Daktari Bingwa wa Mapafu Dkt. Mwanaada Kilima amesema kuwa mtoto huyo alikuja na dalili za kikohozi cha muda mrefu na siku zote amekuwa akiambiwa ana homa ya mapafu mpaka alipokuja Muhimbili na kupatiwa matibabu sasa kikohozi kimeacha na hali yake inaendelea vizuri na tunatarajia kumruhusu ili aende nyumbani kuendelea na maisha.

Mtoto.JPG
Kwa upande wa nama mzazi wa mtoto Edward Bi. Florence Joseph amesema kuwa wamekuwa wakihangaika Hospitali mbalimbali kwa mwaka mmoja na miezi kumi na moja bila kupata matibabu mpaka walipopewa rufaa kuja Muhimbili,

Bi. Florence ameshukuru kwa huduma nzuri na upendo wa hali ya juu aliopata kutoka kwa watoa huduma.
 
Kongole kwa hao madaktari, gharama zake ni sh ngapi?
 
Aliye mponja. Ni mungu wao wameokoa maisha tu
Wewe dada em tumia akili bc, sio kila jambo linatibiwa na maombi ndio maana Mungu akaweka madaktari ila ukikaa ndani kwako ukiwa unamuomba Mungu hawezi kukusaidia kamwe ndio maana ameweka watu wengine kusaidia wengine.
 
Back
Top Bottom