Mtoto anatakiwa kunyonya maziwa ya mama kwa muda gani?

Gnixc_33

Member
Dec 6, 2021
8
6
Habari,

Huu ni uzi kwa ajili ya watoto naomba kuuliza kama. Una uzoefu au wewe ni Dr. Naomba kuelimishwa.

Je, mtoto mchanga anatakiwa kunyonya maziwa ya mama kwa muda gani? Kuna watu wanasema miezi 6 bila chochote. Ukimpa maji ataumwa tumbo ukimpa chakula mapema namaanisha uji, hatofanana na mtoto aliyenyonya maziwa miezi 6 bila kula chochote sina ufahamu nami nina mtoto kwa sasa haitaji kujifunza.

Karibuni kwa Maoni
 
Je, mtoto mchanga anatakiwa kunyonya maziwa ya mama kwa muda gani? Kuna watu wanasema miezi 6 bila chochote. Ukimpa maji ataumwa tumbo
Miaka 2.
 
Habari,

Huu ni uzi kwa ajili ya watoto naomba kuuliza kama. Una uzoefu au wewe ni Dr. Naomba kuelimishwa.

Je, mtoto mchanga anatakiwa kunyonya maziwa ya mama kwa muda gani? Kuna watu wanasema miezi 6 bila chochote. Ukimpa maji ataumwa tumbo ukimpa chakula mapema namaanisha uji, hatofanana na mtoto aliyenyonya maziwa miezi 6 bila kula chochote sina ufahamu nami nina mtoto kwa sasa haitaji kujifunza.

Karibuni kwa Maoni
Miaka miwili
 
Baada ya miezi 6 unaweza kuanza kumpa vyakula laini kama vile biskuti unaiwekea na maziwa ila maziwa ya Mama anatakiwa anyonye kwa muda wa miaka miwili.
 
Inategemea kama mtoto anashiba. Watoto wengi hawashibi hasa wa kiume na hivyo lazima wapewe uji hata akiwa ni wiki moja. Uji wa muhogo uliochujwa kwa kitambaa kisafi kwa kijiko. Mtoto kama hashibi unamuona analia sana. Hivyo unampa kidogo utaona ananyamaza na kuuchapa usingizi

Muwe mnauliza akinamama watu wazima masuala haya, si akina Nakadori wanaofikiria madushe tu kila wakati
 
Inategemea kama mtoto anashiba. Watoto wengi hawashibi hasa wa kiume na hivyo lazima wapewe uji hata akiwa ni wiki moja. Uji wa muhogo uliochujwa kwa kitambaa kisafi kwa kijiko. Mtoto kama hashibi unamuona analia sana. Hivyo unampa kidogo utaona ananyamaza na kuuchapa usingizi
Duh!!!!

Mama ale chakula cha kutosha, maziwa ya mama pekee yanatosha miezi sita ya mwanzo!!!
 
Baada ya miezi sita unamuanzishia uji mwepesi usio na mchanganyiko wa vitu vingi, mf. Unga wa ugali tu unatengenezea uji...Kwa mwezi mmoja tumbo lizoee Kisha unaanza kuongeza vingine sijui cerelac, ugali, smoothies, mitori, bokoboko n.k (huku akiendelea kunyonya Hadi 2yrs)

Hayo ya kuchuja na kitambaa nobody got time for that 😂
 
Baada ya miezi sita unamuanzishia uji mwepesi usio na mchanganyiko wa vitu vingi, mf. Unga wa ugali tu unatengenezea uji...Kwa mwezi mmoja tumbo lizoee Kisha unaanza kuongeza vingine sijui cerelac, ugali, smoothies, mitori, bokoboko n.k (huku akiendelea kunyonya Hadi 2yrs)

Hayo ya kuchuja na kitambaa nobody got time for that
Sawa mkuu
 
Kihosptal wanasema miezi 6 ya mwanzo mtoto anyonye tu. Lakini kuna sababu ambazo mama anaweza akamuanzishia mtoto formula au viuji kabla ya miezi 6. Na kuacha kunyonyesha inategemea na sababu kila mtu na mtoto wake ila wanashauri miaka miwili.
 
Habari,

Huu ni uzi kwa ajili ya watoto naomba kuuliza kama. Una uzoefu au wewe ni Dr. Naomba kuelimishwa.

Je, mtoto mchanga anatakiwa kunyonya maziwa ya mama kwa muda gani? Kuna watu wanasema miezi 6 bila chochote. Ukimpa maji ataumwa tumbo ukimpa chakula mapema namaanisha uji, hatofanana na mtoto aliyenyonya maziwa miezi 6 bila kula chochote sina ufahamu nami nina mtoto kwa sasa haitaji kujifunza.

Karibuni kwa Maoni

Minimum miezi sita ila mimi watoto wangu wote naona mama zao wamewanyonyesha angalau miaka miwili kila mmoja.
 
Back
Top Bottom