Muda sahihi wa kuanza kumpa mtoto uji

sukariyawarembo

Senior Member
Aug 2, 2019
167
116
Wakuu za wakati huu,

Nina mtoto ana miezi mitano bado hatujamuanzisha chakula kingine ananyonya maziwa ya mama yake tu, ila shida ni kuwa amekuwa ananyonya muda wote anakaa kidogo anapata njaa ananyonya tena hadi mama yake amekonda (maziwa anayo ya kutosha).

Sasa tunajiuliza tumuanzishie uji lakini tunasita kwa sababu hospitali madktari wanasema hadi afikishe miezi 6 na huku mtaani wamama wanasema hata miezi minne tu anaruhusiwa kuanza kunywa uji. Tupo njiapanda ni mtoto wetu wa kwanza.

Naamini humu kuna wataalamu na wazoefu naombeni ushauri wenu.
 
Mrembo wangu mm a.k.a Toto la toto alianza na miezi 5 uji wa kuchuja. Baada ya miezi 5 akaanza uji kamili na mtori mwepesi. Sasa mrembo wangu anakula ugali kamili na baba yake.
Na sasa tunamsagia samaki na ndizi,viazi na supu ya samaki. Anapenda mno
Nyama pia na supu yake anapenda sana mpk nackia raha.
Pia ndio mtoto wng w kwanza.

KAZI ni kipimo Cha utu
 
uji wa kuchuja ndo ukoje
 
Muanzishie uji mwepesi taratibu taratibu au ukishindwa tumia maziwa ya formula
 
Mwamba unafeli pakubwa kufata ushauri wa madactari kwenye malezi ya mtoto.
Wao wenyewe hawafanyi hivyo bali wanalazimika kutoa ushauri huo kutokana na muongozo wa wizara ya afya. Mimi mtoto wangu wa kwanza nilizingatia sana ushauri wa daktari cha kishangaza dogo afya yake haikai vizuri sana na nilimpeleka bugando kuonana na daktari bingwa wa watoto alichonieleza baada ya kufanya checkup akaniambia dogo Hana shida yeyote ila achana na madactari unaumiza mtoto we ongea na bibi yake akufundishe namna ya kulea watoto.

Baada ya HAPO nikajifunza kitu, nilipopata mtoto wa pili Ile kafikisha miezi 2 na nusu nikaanza kumpa uji mwepesi Tena nimechanganya na maziwa na sichuji yaani dogo kafika miezi 6 tu ana afya nzuri na uzito wa kutosha hadi clinic wanamtolea mfano yeye mana Kila mwezi anaongezeka kilo 2 hadi 3 na ikapelekea kuwahi kutambaa na kutembea pia alikuwa haugui maranyingi.

Kwa sasa kwenye malezi najiongoza mwenyewe na sifati ushauri wa daktari juu malezi baada ya dactari bingwa wa watoto kunidokeza kitu.
Daktari atahusiku pale tu dogo anaumwa na nimempeleka hospital kupata matibabu.

Kiongozi mpe uji na maji safi na salama mtoto, na usikawie sana kumpa na chakula kingine chenye protein nyingi.
 
Mpatie Lactogen formula 1 huku unamnyonyesha pia

then akifikisha hio miezi sita umuanzishie vyakula mchanganyiko kidogokidogo na vilaini
 
Mrembo wangu mm a.k.a Toto la toto alianza na miezi 5 uji wa kuchuja. Baada ya miezi 5 akaanza uji kamili na mtori mwepesi. Sasa mrembo wangu anakula ugali kamili na baba yake.
Na sasa tunamsagia samaki na ndizi,viazi na supu ya samaki. Anapenda mno
Nyama pia na supu yake anapenda sana mpk nackia raha.
Pia ndio mtoto wng w kwanza.

KAZI ni kipimo Cha utu
hahahhahahaha vip mkuu ukipima DNA ukakuta ni wangu😁😆😅🤣😂
 
Mwamba unafeli pakubwa kufata ushauri wa madactari kwenye malezi ya mtoto.
Wao wenyewe hawafanyi hivyo bali wanalazimika kutoa ushauri huo kutokana na muongozo wa wizara ya afya. Mimi mtoto wangu wa kwanza nilizingatia sana ushauri wa daktari cha kishangaza dogo afya yake haikai vizuri sana na nilimpeleka bugando kuonana na daktari bingwa wa watoto alichonieleza baada ya kufanya checkup akaniambia dogo Hana shida yeyote ila achana na madactari unaumiza mtoto we ongea na bibi yake akufundishe namna ya kulea watoto.

Baada ya HAPO nikajifunza kitu, nilipopata mtoto wa pili Ile kafikisha miezi 2 na nusu nikaanza kumpa uji mwepesi Tena nimechanganya na maziwa na sichuji yaani dogo kafika miezi 6 tu ana afya nzuri na uzito wa kutosha hadi clinic wanamtolea mfano yeye mana Kila mwezi anaongezeka kilo 2 hadi 3 na ikapelekea kuwahi kutambaa na kutembea pia alikuwa haugui maranyingi.

Kwa sasa kwenye malezi najiongoza mwenyewe na sifati ushauri wa daktari juu malezi baada ya dactari bingwa wa watoto kunidokeza kitu.
Daktari atahusiku pale tu dogo anaumwa na nimempeleka hospital kupata matibabu.

Kiongozi mpe uji na maji safi na salama mtoto, na usikawie sana kumpa na chakula kingine chenye protein nyingi.
sawa kiongozi
,ndo mana dogo Hana mwili kabisa ni mwembamba sana eti tunajifariji tunasema amefuata mwili wangu, clinic akienda anaongezeka grams tu sio kilo
 
Wakuu za wakati huu,

Nina mtoto ana miezi mitano bado hatujamuanzisha chakula kingine ananyonya maziwa ya mama yake tu, ila shida ni kuwa amekuwa ananyonya muda wote anakaa kidogo anapata njaa ananyonya tena hadi mama yake amekonda (maziwa anayo ya kutosha).

Sasa tunajiuliza tumuanzishie uji lakini tunasita kwa sababu hospitali madktari wanasema hadi afikishe miezi 6 na huku mtaani wamama wanasema hata miezi minne tu anaruhusiwa kuanza kunywa uji. Tupo njiapanda ni mtoto wetu wa kwanza.

Naamini humu kuna wataalamu na wazoefu naombeni ushauri wenu.
mkuu kwani ww ulikunywa maziwa ya mama tu kwa miezi 6 na iko hivi watoto wanaoambiwa wapewe maziwa ya mama tu kwa muda huo ni wale waliozaliwa na wazazi waathirika ili kuepusha michubuko mdomoni wanashauri anyonye kwa miezi 6. mbali na hapo mpe mwanao chakula unachokula iwe ugali mpondee mpe iwe makande mchotee mchuzi ale yaani mpe vyakula vyote.... habari za kuwasililiza hawa madaktari wa mchongo mtoto atadhoofu na akili zitamuisha
 
Attachments

  • IMG_0380.jpeg
    IMG_0380.jpeg
    494.9 KB · Views: 6
mkuu kwani ww ulikunywa maziwa ya mama tu kwa miezi 6 na iko hivi watoto wanaoambiwa wapewe maziwa ya mama tu kwa muda huo ni wale waliozaliwa na wazazi waathirika ili kuepusha michubuko mdomoni wanashauri anyonye kwa miezi 6. mbali na hapo mpe mwanao chakula unachokula iwe ugali mpondee mpe iwe makande mchotee mchuzi ale yaani mpe vyakula vyote.... habari za kuwasililiza hawa madaktari wa mchongo mtoto atadhoofu na akili zitamuisha
asante mkuu
 
Back
Top Bottom