Mtoto anapojihusisha na Sanaa humjengea uwezo wa ujasiri, utambuzi na ubunifu

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
IMG_20210401_084620_584.jpg
Mwanzo wa ukuaji wa watoto hutegemea mikakati au njia anuwai, ambazo mara nyingi hutegemea mazingira ya kucheza na kufurahi, hapa bila kutambua elimu ya sanaa hutolewa. Walimu wa watoto katika ufundishaji hutegemea zaidi sanaa, kufanikiwa kwa utoaji wa elimu kwa watoto kunategemea uelewa wa walimu wa jinsi ya kutumia aina mbalimbali za sanaa kama njia ya kufundishia.

Ufundishaji wa miaka ya zamani ulikuwa unategemea zaidi sanaa katika kufundisha watoto kuhusu elimu na ujuzi mbalimbali. Kwa mfano, watoto walikuwa wanafundishwa kuwa na ujasiri kwa kutumia hadithi na nyimbo au ngoma. Mfundishaji alikuwa anawasilisha ujumbe kupitia sanaa.

Katika kipindi hiki cha ukuaji wa teknolojia ni muhimu zaidi kutumia sanaa kumpa mtoto nafasi ya kuelezea hisia zake ama ujuzi wake. Unaweza kumuandalia mtoto wako mazingira ya kutumia sanaa kama nyenzo ya mawasiliano, kwa mfano, kwa kutumia michoro. Hapa mtoto mwenyewe huitumia sanaa.

Umuhimu wa Sanaa kwa Watoto

Sanaa husaidia watoto kugundua na kujenga dhana ya utambuzi na ubunifu, na kutambua hisia zake. Kwa mfano, kupitia Sanaa ya uchoraji mtoto hufanya maamuzi ya uchaguzi wa rangi, namna ya kujenga mchoro wake, na kufanya maamuzi juu ya vifaa gani vya kutumia. Hivyo vyote humjenga katika kujenga ujasiri na maamuzi binafsi

Vile vile sanaa inahusishwa na kukuza ujuzi wa lugha na mawasiliano kwa watoto. Huwasilisha sura mbalimbali kutoka katika jamii na tamaduni.

Sanaa inaweza kusaidia kubadilisha hali ya watoto ambazo zinaweza kuboresha afya ya mihemko na mtazamo. Watoto hufurahushwa na sanaa, hivyo mtoto anaweza kubadili hali ya huzuni na kuwa na furaha kupitia sanaa anayokutana nayo.

Aidha, sanaa ya ni sehemu muhimu ya mtaala wa watoto kutokana na umuhimu na faida inayowajenga watoto katika misingi ya ukuaji bora. Hivyo, inashauriwa mtoto ajengewe mazingira ya kujihusisha na sanaa akiwa nyumbani na shuleni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom