Mtoto analala akistuka anadai nyama yake

Habari zenu. Wakuu tangu wiki iliyopita, mwanangu (wa kike) amekuwa na tabia kwamba analala, usiku wa manane anamka ghafla huku anasema, 'nadai nyama yanguuu'. Atalia hivyo akidai nyama, na inaweza hata saa nzima akachukua kudai nyama. Na kimsingi sisi bajeti ya nyama ni mara 1 kwa wiki. Je hii itakuwa inaashiria nini?Au niongeze siku za kula nyama?Wenu Benokolongokonongose

Wewe dini gani? au unaamini nini?
Ili jibu langu lisikukwaze
 
Au ampikie hata kilo moja halaf wampe yote ale muwekeeni kwenye hotpot halaf mnapakulia kwenye sahani yake kila akimaliza muongezeenii akisema imetosha mnaacha kumpa,halaf muone usiku ataomba akiomba basi kuna kituu

khaa one kilo??peke yake?
 
Atakuwa anapenda nyama sana huyoo! Ila muombee jamani!!!
 
zoeshaneni kula na mboga za majani nyama kila siku sio nzuri mwanao atazoea tu ratiba ya kwa wiki mara moja ni sawa sio mbaya
 
Nyama nyama nyama zenyewe sumu tupu,jaribu kufuatilia kwa ukaribu kama walivyokueleza hapo juu kwa kujitahidi kumpa kiasi kikubwa kwa muda mfupi,then kama hakuna mabadiliko tafuta msaada wa kiroho kulingana na imani yako,ulimwengu umeharibika sana,kwanini asiote pipi?
 
kwa sababu ana miaka miwili ni mdogo sana inaonekana anapenda sana nyama sasa akilala huwa anaota ndoto za kula nyama kwa hiyo akistuka anakuwa bado na yale mawazo ya nyama sasa jitahidi kununua hata robo kwa ajili yake aizoee. pia sali sana
 
Habari zenu. Wakuu tangu wiki iliyopita, mwanangu (wa kike) amekuwa na tabia kwamba analala, usiku wa manane anamka ghafla huku anasema, 'nadai nyama yanguuu'. Atalia hivyo akidai nyama, na inaweza hata saa nzima akachukua kudai nyama. Na kimsingi sisi bajeti ya nyama ni mara 1 kwa wiki. Je hii itakuwa inaashiria nini?Au niongeze siku za kula nyama?Wenu Benokolongokonongose

naomba kuuliza kwanza, je mama yake ndiye unaishi nae au umeoa mke mwingine na anakusaidia kumlea hapo nyumbani kwako? kama jibu ni mama wa kambo basi usihangaike kuuliza we jua tu mtoto ananyanyasika wakati wa kula na akili yake inashindwa kuvumilia ndo maana anayasema usiku ndotoni,,,kama unaishi na mama yake mzazi basi usijiulize mara mbilimbili ni mambo ya kichawi tu hayo yana msumbua mtoto, tafuta njia sahihi ya kumtibu mwanao la sivyo itakugharimu.
 
Hii sredi imenichekesha sana japo haitakiwi
 
dalili mbaya sana hiyo, kiimani huyo atakuwa analishwa nyama usingizini, mpeleke kwenye maombi fasta!
 
Muombee huyo mtoto,kuna wachawi wanamsumbua usiku
 
hizo ni nguvu za giza, tafadhali tafuta msaada wa ki-Imani kwanza... kwanini iwe ni usiku tuu?

Habari zenu. Wakuu tangu wiki iliyopita, mwanangu (wa kike) amekuwa na tabia kwamba analala, usiku wa manane anamka ghafla huku anasema, 'nadai nyama yanguuu'. Atalia hivyo akidai nyama, na inaweza hata saa nzima akachukua kudai nyama. Na kimsingi sisi bajeti ya nyama ni mara 1 kwa wiki. Je hii itakuwa inaashiria nini?Au niongeze siku za kula nyama?Wenu Benokolongokonongose
 
Muda wa kula huwa anapenda nyama kuliko mboga nyingine?
 
Hahhhhha labda analishwa nyama na wachawiii wanampunja, muombee tu sio vizuri

Hata mimi naona kama siyo ishara nzuri hasa kwa mtoto kwa nn adai nyama usiku tu na siyo mchana kuna mamna hapo afanye maombi tu

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Mmmmh kuna waalakini hapo aisee hata kama yani mtoto aamke hivi hivi usiku wa mananr anadai nyama na nyama yenyewe anakula kwa week mara mara moja"mpeleke afanyiwe ma0mbi!
 
Au ampikie hata kilo moja halaf wampe yote ale muwekeeni kwenye hotpot halaf mnapakulia kwenye sahani yake kila akimaliza muongezeenii akisema imetosha mnaacha kumpa,halaf muone usiku ataomba akiomba basi kuna kituu

nawe ulikua unaliliaga nyama nini, nimependa trick yako ya kufanya utambuzi.
 
Habari zenu. Wakuu tangu wiki iliyopita, mwanangu (wa kike) amekuwa na tabia kwamba analala, usiku wa manane anamka ghafla huku anasema, 'nadai nyama yanguuu'. Atalia hivyo akidai nyama, na inaweza hata saa nzima akachukua kudai nyama. Na kimsingi sisi bajeti ya nyama ni mara 1 kwa wiki. Je hii itakuwa inaashiria nini?Au niongeze siku za kula nyama?Wenu Benokolongokonongose

cc: MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom