Mtoto aliyekataliwa na baba yake

Mtoto aliyekataliwa na baba yake

Vituka

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
2,268
Reaction score
1,267
Habari zanu wana JF,

Naombeni ushauri wenu katika hili lililonikuta, ni story ndefu ila in short miaka ya nyuma kipindi tukiwa tunasoma, our mom alikuwa anaishi na kabinti fulani, by that time she was 10 yrs na kiliacha shule kutokana na matatizo ya wazazi wake so kikawa home kinamsaidia mom kazi ndogondogo tu na kumpa mom kampani. Tulimchukulia kama mdogo wetu na tulimpenda sana. After two years my sis aliyekuwa anaishi DSM alijifungua so akamchukua kuishi nae ili amsaidie kazi. Kaka yetu mmoja by that time alikuwa anasoma alikuwa akiishi hapo kwa sister.

After two years binti akagundulika kuwa mjamzito na alipoulizwa nani mhusika alisema ni huyo kaka yangu ila yeye alikana kabisaaaaa!!!Binti wa watu akarudishwa kijijini na alijifungua mtoto wa kike akiwa na miaka 15. Mwaka juzi nilienda kijijini na nikabahatika kumuona huyo mtoto, honestly she resembles my brother kabisaaaaa!!! Nilimpigia na kumweleza kuhusu hilo but alisema kuwa yeye hahusiki na kama anafanana na yeye it is not his business. Huyo mtoto alikuwa anaishi maisha magumu sana imagine at the age of 12 hajaanza darasa la kwanza. ilimuomba mama yake nimchukue niishi nae na pia nimsaidie kwa vile yule kweli ni mtoto wa kaka yangu!

Kwa vile bro alishakataa hata nilipomwambia kuwa mtoto kafanana nae, sikumshirikisha uamuzi wangu niliouchukua wa kumlea huyo mtoto ila mom nilimshirikisha na hakuwa na tatizo na yeye toka zamani alishataka kumchukua ila bro alimkataza so ikabidi aheshimu uamuzi wake. Hadi sasa naishi nae na the girl is very inteligent, amini usiamini nilipompeleka shule walimpa mtihani na kugundua kuwa hakustahili kuanza drs la kwanza, wakampeleka la 3 now yupo la 5.

Last week mke wa huyo brother alikuja kwangu kunitembelea na kumuona yule mtoto, akaniuliza mtoto wa nani?Nikamjibu ni mtoto wa shemeji yangu ili kuua soo wasie gombana na mumewe. Sasa jana narudi toka job namkuta brother kwangu kafura vibaya sana na anadai mimi ninadharau kwa nini nimemchukua mtoto ambae sie wake na amedai kuwa mimi na yeye undugu wetu umeisha na akaondoka bila hata kuniaga.

Naombeni ushauri wenu katika hili mana that brother of mine ni mbabe balaa, yani ndugu wanamwogopa balaa isipokuwa mimi tu!!

Nawakilisha.
 
kwan wew huyo bro wako ndo anakupa kula kama sivyo mlee tu huyo mtoto mana ni wako pia achana na huyo brothr ako mana ameingliwa na roho ya kishetan huwez kataa mtoto wako
 
Walimweusi usiogope ubabe wa kaka yako vizuri wote wanamuogopa isipokuwa wewe tu humuogopi maadamu umeamua kumsaidia mtoto msaidie hiyo ni damu yenu hata mkimtelekeza atabaki kuwa ni mtoto wenu,hujui baadaye ndo atakuja kukusaidia au kumsaidia hata huyo baba yake aliye mkataa.Mungu azidi kukusaidia ili uweze kumsomesha na kumlea katika maadili mazuri.
 
Ulichofanya ni kizuri sana hata kama Bro wako
kamkana huyo mtoto,kumbuka hata Dini zina
taka tusaidie maskini,wasiojiweza.

Nadhani hata nawe unakiri kuwa ni mimba
ya Bro wako,pia kwa kuwa wewe unafanya
maisha yako bila kumtegemea mtu
endelea. Huyo atajirudi muda si mrefu.

Si lazima umsaidie ndugu yako,Dini zinatutaka
kumsaidia mtu yoyote ilimradi uwezo unao.
Si unajitegemea kimaisha usife moyo
endelea kumsaidia huyo mtoto.
 
ale kona zake, yeye anajua kuzaa tu na kutelekeza? we umefanya jambo jema, mlee huyo mtoto kama nafsi yako inavyokutuma, achana na vitisho vya huyo kaka yako nafsi yake inamsuta na anaona haya tu kukubali kwamba alifanya makosa enzi hizo!!1
 
Walimweusi,

Uamuzi wa kumchukua na kumsomesha huyo mtoto ni uamuzi mzuri sana na pongezi sana pia, kwangu mimi sioni ubaya wowote hilo ni jaribu tu na utashinda. Hata kama anamkataa kuwa si mtoto wake lakini wewe simamia uamuzi wako wa kuendelea kumsomesha na kumtunza, malipo yake ni makubwa sana na ndivyo tunavyotakiwa kufanya na kusaidia wengine ambao ni wahitaji wawe ndugu au jamaa au ...., mradi ni wahitaji na uwezo wa kuwasaidia tunao.

Wakati mwingine kukaa kimya huwa ni jibu zuri sana wala usimchukie huyo ndugu yako na hata kuonyesha hali yoyote isiyofaa kwake acha maisha yaendelee siku moja muda utaamua na ukweli huo utakuwa wazi.

Ubarikiwe sana.

Hata akikutisha
 
Huwa nashangaa mzazi wa namna hii??? Walimweusi mie nakushauri tu hebu jitahidi kwa vihela vyetu hivi hivi vidogo umsomeshe hadi panapo uhai wa Mola. Maana hujui kesho yako!. Hivi huyu baba nafsi mwake anasubiri kusikia mtoto wake kapata mafanikio ndio aje aseme mimi ni baba yako?? Usiogope vitisho kaza roho!
 
utabarikiwa sana na utapata mengi na faida nyingi kwa kupitia huyo mtoto. Fumba macho na ziba masikio juu ya chochote kibaya utakacho ambiwa juu ya huyo mtoto...hakika mfanye huyo mtoto awe mwanao atakuja kukusaidia
 
huwa siamini sana katika sadaka nizitoazo madhabahuni iwe msikitini au makanisani!!kam kweli naweza barikiwa kama kuwasaidia wenye shida mbalimbali ,wagonjwa na maskini naamini sana katika hili!!!
tena sadaka hii hufika direct kwa mungu maana yule apokeae hupokea kwa imani na kukuombea ubarikiwe .keep on kila kazi njema ina mavuno yake usiwajali binadamu ndugu yangu
ngoja nikupe kisa:
kuna kaka mmja alimpa ujauzito housegal ikajulikana kabisa ni yeye yule bwana akakataa kabisa ,dada yule akapoteza kibarua chake akarudi huko moshi vijijini hata pakuishi tabu! akajifungua mtoto utasema alikuwa na photokopy machine,kwa aibu wakamchukua yule mtoto nakumtelekeza yule dada bila msaada wowote!yule bwana akaoa huko botswana akawa anatamani sana mtoto wa kiume hakuwahi mpata akafikisha majike 5,watu wakmwambia face your ghost beforre u move forward kamwombe yule dada msamaha nakumjengea hata kibanda ,yule bwana akafuata ule ushauri after 1yrs alipata mtoto wa kiume .na yule mtoto wa housegal anamaliza engineering 4th yr.
nakushauri kaka yangu usimwache huyo mtoto msomeshe msaidie kila step mfahamishe mama yako ndio atakayetuelewa .siku moja utashuhudia machozi ya huyo kaka yako .mimi tunapoongea ndani kwangu kuna msichana wa kazi amejifungua tr7 na alipewa mimba na ndugu wa mume wangu mtoto yule amefanana kopy right na yule jamaa na mwanzo alikuwa anakana akaja kukubali kwa maandishi.
 
Kama sikosei, hofu yako ni ya kiuhusiano zaidi ... hali kama hizo zipo na migogoro mikubwa hutokea, it is a very risk game na hasa ukichukulia kufanana pekee haitoshi kuthibisha uhusika wa mtu lakini, ushahidi wa kimazingira bado unafanya nyota yako ing'ae, mimi binafsi nakuhesabia ushindi katika hili either awe ni wa kaka ama la!

Siku zote huwa naamini katika sheria, na sheria siku zote ndio "HAKI", in short, Bro seem anajua jinsi alivyokua imlicated kwenye hii ishu na anadhani kuwa mkali na kupiga biti kutamsaidia, as long as "alikula mzigo" na aka-kam inside then the risk ya yeye kuwa muhusika ni 51% so alitakiwa awe mpole! Kama ningekuwa ni yeye, ningekuwa mpole na kutafuta njia za kisayansi kudhibitisha kutokuwa kwa hatia kwangu ....ninginevyo anachofanya ni kuruka-ruka tu, kitu ambacho one day atatua! USIOGOPE, uhusiano wenu utaharibika sana kwa muda tu lakini soon atakukubali na kukupenda kuliko yeyete hapa duniani ......
 
bro wako ana maruhani.
asi alishamkataa uyo mtoto sasa wewe kuymchukua inamuhusunini?
alishasema ahusiki sasa uamuzi wa wewe kumlea ni km unamsaidia bnadamu mwngne yeyote hauna connection na undugu apo THOU ukweli ndo vile unamlea mwanenu

UYO KAKAKO GUILTNESS INAMTAFUNA
anataman sana angekubali nw anagekuwa huru na mtoto..na ivyo labda anasikia mtoto kichwan zipo bas apo dahh anawish arudishe miaka nyuma.....

achana nae...
undugu auvunjwi kzembe ivo
afta lo wat u did is right mbele za mungu na wanadamu
endelea kumlea mwenyewe atakuja siku kukuomba akae na mwane....not so long....DHAMIRA INAMUUMA...umwombe kibali cha kumchukua mtoto ..kiaje/kivvp asi alishakataa?
pambavu zake.....achana nae
 
huwa siamini sana katika sadaka nizitoazo madhabahuni iwe msikitini au makanisani!!kam kweli naweza barikiwa kama kuwasaidia wenye shida mbalimbali na maskini naamini sana katika hili!!!
tena sadaka hii hufika direct kwa mungu maana yule apokeae hupokea kwa imani na kukuombea ubarikiwe .keep on kila kazi njema ina mavuno yake usiwajali binadamu ndugu yangu
ngoja nikupe kisa:
kuna kaka mmja alimpa ujauzito housegal ikajulikana kabisa ni yeye yule bwana akakataa kabisa ,dada yule akapoteza kibarua chake akarudi huko moshi vijijini hata pakuishi tabu! akajifungua mtoto utasema alikuwa na photokopy machine,kwa aibu wakamchukua yule mtoto nakumtelekeza yule dada bila msaada wowote!yule bwana akaoa huko botswana akawa anatamani sana mtoto wa kiume hakuwahi mpata akafikisha majike 5,watu wakmwambia face your ghost beforre u move forward kamwombe yule dada msamaha nakumjengea hata kibanda ,yule bwana akafuata ule ushauri after 1yrs alipata mtoto wa kiume .na yule mtoto wa housegal anamaliza engineering 4th yr.
nakushauri kaka yangu usimwache huyo mtoto msomeshe msaidie kila step mfahamishe mama yako ndio atakayetuelewa .siku moja utashuhudia machozi ya huyo kaka yako .mimi tunapoongea ndani kwangu kuna msichana wa kazi amejifungua tr7 na alipewa mimba na ndugu wa mume wangu mtoto yule amefanana kopy right na yule jamaa na mwanzo alikuwa anakana akaja kukubali kwa maandishi.

umesema kweli mtupu na...... amhurumiaye masikini humkopesha Mungu naye atamlipa kwa tendo lake jema na dini nzuri ni kuwaona wagonjwa na kusaidia masikini neno linasema.
 
huwa siamini sana katika sadaka nizitoazo madhabahuni iwe msikitini au makanisani!!kam kweli naweza barikiwa kama kuwasaidia wenye shida mbalimbali na maskini naamini sana katika hili!!!
tena sadaka hii hufika direct kwa mungu maana yule apokeae hupokea kwa imani na kukuombea ubarikiwe .keep on kila kazi njema ina mavuno yake usiwajali binadamu ndugu yangu
ngoja nikupe kisa:
kuna kaka mmja alimpa ujauzito housegal ikajulikana kabisa ni yeye yule bwana akakataa kabisa ,dada yule akapoteza kibarua chake akarudi huko moshi vijijini hata pakuishi tabu! akajifungua mtoto utasema alikuwa na photokopy machine,kwa aibu wakamchukua yule mtoto nakumtelekeza yule dada bila msaada wowote!yule bwana akaoa huko botswana akawa anatamani sana mtoto wa kiume hakuwahi mpata akafikisha majike 5,watu wakmwambia face your ghost beforre u move forward kamwombe yule dada msamaha nakumjengea hata kibanda ,yule bwana akafuata ule ushauri after 1yrs alipata mtoto wa kiume .na yule mtoto wa housegal anamaliza engineering 4th yr.
nakushauri kaka yangu usimwache huyo mtoto msomeshe msaidie kila step mfahamishe mama yako ndio atakayetuelewa .siku moja utashuhudia machozi ya huyo kaka yako .mimi tunapoongea ndani kwangu kuna msichana wa kazi amejifungua tr7 na alipewa mimba na ndugu wa mume wangu mtoto yule amefanana kopy right na yule jamaa na mwanzo alikuwa anakana akaja kukubali kwa maandishi.

Nivea asante kwa ushauri ila namuonea huruma sana kaka yangu, kwanza yule mtoto huwa hataki kusikia habari za baba yake, ananijua mimi kama mama yake na mume wangu kama baba yake. She is happy and comfortable! Nina uhakika ipo siku atakuja kujutia uamuzi wake. Now ana watoto 4, wote wasichana, huyo first born wake yupo darasa la 7 ila bonge la kilaza kabadilisha shule hadi kachoka mwenyewe!! I belive Mungu ataniongoza katika kumlea huyu mtoto.
 
huwa siamini sana katika sadaka nizitoazo madhabahuni iwe msikitini au makanisani!!kam kweli naweza barikiwa kama kuwasaidia wenye shida mbalimbali ,wagonjwa na maskini naamini sana katika hili!!!
tena sadaka hii hufika direct kwa mungu maana yule apokeae hupokea kwa imani na kukuombea ubarikiwe .keep on kila kazi njema ina mavuno yake usiwajali binadamu ndugu yangu
ngoja nikupe kisa:
kuna kaka mmja alimpa ujauzito housegal ikajulikana kabisa ni yeye yule bwana akakataa kabisa ,dada yule akapoteza kibarua chake akarudi huko moshi vijijini hata pakuishi tabu! akajifungua mtoto utasema alikuwa na photokopy machine,kwa aibu wakamchukua yule mtoto nakumtelekeza yule dada bila msaada wowote!yule bwana akaoa huko botswana akawa anatamani sana mtoto wa kiume hakuwahi mpata akafikisha majike 5,watu wakmwambia face your ghost beforre u move forward kamwombe yule dada msamaha nakumjengea hata kibanda ,yule bwana akafuata ule ushauri after 1yrs alipata mtoto wa kiume .na yule mtoto wa housegal anamaliza engineering 4th yr.
nakushauri kaka yangu usimwache huyo mtoto msomeshe msaidie kila step mfahamishe mama yako ndio atakayetuelewa .siku moja utashuhudia machozi ya huyo kaka yako .mimi tunapoongea ndani kwangu kuna msichana wa kazi amejifungua tr7 na alipewa mimba na ndugu wa mume wangu mtoto yule amefanana kopy right na yule jamaa na mwanzo alikuwa anakana akaja kukubali kwa maandishi.

Hvi kwa nini huwa mnapenda kuishi na ndugu wa mume/mke pamoja? Ni tabia gani hyo?
 
Endelea kufanya ulichokifanya, na pia hata kama huyo Bro wako ni mbabe vip, tegemea ulinzi na baraka za MUNGU na pia kuna siku atakuja kukupigia magoti wewe pamoja na ubabe wake (Shika sana hii sentensi utakuja kutoa feedback baadaye)
 
hongera kwa uamuzi wa kumchukua huyo mtoto..maana ni damu yenu haswaa..hauna haja ya kuhofu juu ya kaka yako..yule ni mwanane tu..hata akikataa..na undugu hua hauishi ivo..kuna siku atajirudi tu,it is just a mattter of time
Habari zanu wana JF,

Naombeni ushauri wenu katika hili lililonikuta, ni story ndefu ila in short miaka ya nyuma kipindi tukiwa tunasoma, our mom alikuwa anaishi na kabinti fulani, by that time she was 10 yrs na kiliacha shule kutokana na matatizo ya wazazi wake so kikawa home kinamsaidia mom kazi ndogondogo tu na kumpa mom kampani. Tulimchukulia kama mdogo wetu na tulimpenda sana. After two years my sis aliyekuwa anaishi DSM alijifungua so akamchukua kuishi nae ili amsaidie kazi. Kaka yetu mmoja by that time alikuwa anasoma alikuwa akiishi hapo kwa sister.

After two years binti akagundulika kuwa mjamzito na alipoulizwa nani mhusika alisema ni huyo kaka yangu ila yeye alikana kabisaaaaa!!!Binti wa watu akarudishwa kijijini na alijifungua mtoto wa kike akiwa na miaka 15. Mwaka juzi nilienda kijijini na nikabahatika kumuona huyo mtoto, honestly she resembles my brother kabisaaaaa!!! Nilimpigia na kumweleza kuhusu hilo but alisema kuwa yeye hahusiki na kama anafanana na yeye it is not his business. Huyo mtoto alikuwa anaishi maisha magumu sana imagine at the age of 12 hajaanza darasa la kwanza. ilimuomba mama yake nimchukue niishi nae na pia nimsaidie kwa vile yule kweli ni mtoto wa kaka yangu!

Kwa vile bro alishakataa hata nilipomwambia kuwa mtoto kafanana nae, sikumshirikisha uamuzi wangu niliouchukua wa kumlea huyo mtoto ila mom nilimshirikisha na hakuwa na tatizo na yeye toka zamani alishataka kumchukua ila bro alimkataza so ikabidi aheshimu uamuzi wake. Hadi sasa naishi nae na the girl is very inteligent, amini usiamini nilipompeleka shule walimpa mtihani na kugundua kuwa hakustahili kuanza drs la kwanza, wakampeleka la 3 now yupo la 5.

Last week mke wa huyo brother alikuja kwangu kunitembelea na kumuona yule mtoto, akaniuliza mtoto wa nani?Nikamjibu ni mtoto wa shemeji yangu ili kuua soo wasie gombana na mumewe. Sasa jana narudi toka job namkuta brother kwangu kafura vibaya sana na anadai mimi ninadharau kwa nini nimemchukua mtoto ambae sie wake na amedai kuwa mimi na yeye undugu wetu umeisha na akaondoka bila hata kuniaga.

Naombeni ushauri wenu katika hili mana that brother of mine ni mbabe balaa, yani ndugu wanamwogopa balaa isipokuwa mimi tu!!

Nawakilisha.
 
Usijali ubabe wake ukisikia ufisadi wa roho za watu ndio huo,yeye kwani huyo mtoto anamzidishia nini akiwa hapo kwako au anampunguzia nini? anajua kosa alofanya na nafsi yake inamsuta ila bado hataki kukubali makosa,cha muhimu mlee huyo bint kwa mapenzi kama mtoto wako na mwenyezi mungu atakupa kheir yako na ipo siku huyo kakako atajuta kwa nini alimkataa...inshallah mungu akupe umri mrefu na akuzidishie kipato na akupe ushujaa wakuweza kuhimili kila mtihani...
 
Hvi kwa nini huwa mnapenda kuishi na ndugu wa mume/mke pamoja? Ni tabia gani hyo?
hatuishi nao ni wale wakupita likizo ya shule nk.binafsi sipendi kabis aila umaskini wa familia zetu ndio unapelekea hayo,hata wewe katika maisha hautaliepuka .huyo kijana alikuwa yuko likizo ya chuo ile ya june akapita home kuchukua ad na matumizi mengine maana ndio tunamsomesha akaacha na mimba hahahaahahahahaah dalaliiiii labda ukaishi mars kwakeli
 
Hvi kwa nini huwa mnapenda kuishi na ndugu wa mume/mke pamoja? Ni tabia gani hyo?

Ni ngumu kukwepa extended families in Africa my dia!Kwa mfano huyo brother alichaguliwa kusoma Azania na sister alikuwa anaishi karibu na shule so ili kuupunguza gharama ikabidi aishi na sister ili iwe rahisi kwake kwenda na kurudi shule.
 
Nivea asante kwa ushauri ila namuonea huruma sana kaka yangu, kwanza yule mtoto huwa hataki kusikia habari za baba yake, ananijua mimi kama mama yake na mume wangu kama baba yake. She is happy and comfortable! Nina uhakika ipo siku atakuja kujutia uamuzi wake. Now ana watoto 4, wote wasichana, huyo first born wake yupo darasa la 7 ila bonge la kilaza kabadilisha shule hadi kachoka mwenyewe!! I belive Mungu ataniongoza katika kumlea huyu mtoto.
trust me kumpata mtoto wa kiume itakuwa tabu sana mungu anamtengenezea mazingira ya aibu na fedheha ile ile aliyoipata yule hg.mwombe mungu uwe hai utashuhudia hao watoto watakavyotingwa mimba kabla ya ndoa nakutelekezwa japo hatuombei baya litokee.sioni sababu yakumkataa mtoto ambaye humfuti mavi wala humwogeshi wala kumfulia aisee
 
Back
Top Bottom