Mtoto ahoji kukaa mahabusu miaka miwili akisubiri kesi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,372
8,108
Mmoja wa watoto wanaohifadhiwa katika mahabusu ya watoto Upanga, jijini Dar es Salaam, amehoji kukaa mahabusu kwa miaka miwili sasa, akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake inayomkabili.

Mtoto huyo aliyekuwa mahabusu hapo kwa kukinzana na sheria akikabiliwa mashtaka ya mauaji, alibainisha hayo jana wakati wajumbe wa Tume ya Haki Jinai, iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuangalia namna ya kuboresha mfumo na taasisi zinazohusika na haki jinai ilipowatembelea.

Akizungumza na wajumbe hao, wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) mstaafu, Said Mwema, mtoto huyo alisema anakabiliwa na kesi ya jinai inayosikilizwa na Mahakama Kuu. Alisema amekaa mahabusu hapo kwa miaka miwili sasa akisubiri kesi yake hiyo.

“Mimi naitwa XY, nina kesi ya PI na mpaka sasa nina miaka miwili niko hapa kituoni. Lakini wanasheria wanaotutembelea wanasema kesi za watoto zinatakiwa kuisha ndani ya miezi sita. Tunaomba na sisi mtuangalie wenye kesi za aina hii,” alisema mtoto huyo.

Awali, meneja wa mahabusu hiyo, Darius Damas aliwaeleza wajumbe hao kuwa mahabusu ya watoto ilianzishwa mwaka 1962 kwa lengo la kuhifadhi watoto walioshtakiwa kwa kukinzana na sheria ili kuwapa mafunzo ya marekebisho ya tabia, wakati wakiendelea kusikiliza kesi zao mahakamani.

Alisema watoto wanaohifadhiwa kituoni hapo ni wale wanaokabiliwa na makosa ya mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha, wizi, kuingia nchini bila kibali.

Damas alisema kesi za watoto zinapaswa kuisha ndani ya miezi sita na kama kuna sababu za msingi, inaenda hadi miezi tisa.

Akijibu maswali ya wajumbe, alisema hawana tatizo la kuchelewa kwa upelelezi, kwa sababu watoto hupelekwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika, isipokuwa kesi za mauaji, kwa kuwa hizo zina utaratibu wake maalumu.

Wakati huo huo, tume hiyo ilitembelea Chuo cha Taaluma ya Urekebu (urekebishaji tabia) cha Jeshi la Magereza Ukonga na kushauri kuweka mfumo wa kufuatilia mwenendo wa maisha ya watu waliomaliza vifungo vyao ili kujua kama wamekuwa wema kwa jamii.
Ushauri huo ulitolewa na Mkuu wa Majeshi mstaafu, Inspekta Jenerali Ernest Mangu ambaye ni miongoni mwa wajumbe hao.

Awali, chuo hicho kiliwasilisha maoni yake yaliyojikita kwenye maboresho mbalimbali ya utendaji wa Jeshi la Polisi, ofisi ya DPP, mahakama, mfumo wa sheria, muundo wa taasisi ya magereza, uhaba wa bajeti na mahitaji ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

MWANANCHI
 
No arresting mpaka upelelezi uwe umekamilika na hii ndio sheria, ni vema mno middle class tukaanza kuishi kwa mujibu wa kisheria, huyu ni suspect ana haki zake kama mimi na wewe why 2yrs jela bila upelelezi kukamilika, pls President Samia fumua hili jeshi, ajiri young guy's, wawe trained vilivyo na wengine wapelekwe Namibia Botswana UK na USA (hasa wa DNA &observations, profiles, pathology),hii iwe ni crash program ya 48mths, wazee above 40yrs wote wa resigns, then tuone the way forward
 
Mkuu hili sio tatizo,tatizo Ni pale ambapo waliokuwa wakiulinda na kuutetea mfumo ndio wamepewa kazi ya kuuchunguza mfumo!! Huenda madam president amedhamiria kuubadili lkn ukweli Ni kuwa taifa lina mifumo chakavu
Taifa mfu hili.
Tunajiendea ali mradi jua linachomoza. We are dead on every bit.
 
No arresting mpaka upelelezi uwe umekamilika na hii ndio sheria, ni vema mno middle class tukaanza kuishi kwa mujibu wa kisheria, huyu ni suspect ana haki zake kama mimi na wewe why 2yrs jela bila upelelezi kukamilika, pls President Samia fumua hili jeshi, ajiri young guy's, wawe trained vilivyo na wengine wapelekwe Namibia Botswana UK na USA (hasa wa DNA &observations, profiles, pathology),hii iwe ni crash program ya 48mths, wazee above 40yrs wote wa resigns, then tuone the way forward
"....watoto hupelekwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika, isipokuwa kesi za mauaji, kwa kuwa hizo zina utaratibu wake maalumu..."
 
Ikiwa itabainika hakuua hiyo miaka 7 mtamlipa nini?

Sijui kwa nini sisi Watanzania tuna roho mbaya kiasi kwamba hatujali haki za wengine.

kesi inatakiwa iishe haraka kama akikutwa na hatia afungwe na akikutwa hana hatia aachiwe haraka.

hiyo ndio haki.
miwili bado michache sana, walau ifike 7+ ndiyo alalamike
 
"....watoto hupelekwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika, isipokuwa kesi za mauaji, kwa kuwa hizo zina utaratibu wake maalumu..."
Haya ndio mapungufu ya kisheria, kwani murder case ina tofauti gani?,huyu mtoto bado ni suspect sio mhalifu, nikipewa urais wa 24hrs makosa yote ya kijinai yatakua na bail, suspect lazima apelekwe kwa court of law within 48hrs, kama police hawawezi ili lazima mahakama itoe kibali cha kumzuia suspect for another 48hrs, no arrest until upelelezi umekamilika
 
Mtuhumiwa amefikia kituoni kwa kuuliwa na polisi,halafu mwanasiasa anatoa amri polisi waliofanya mauaji wachunguzwe na polisi wenzao .Ni balaa
Hili nalo ni tatizo ndio maana tunahitaji katiba mpya,itatupatia IPID, hawa ni kama MPs wa jeshi, watakua na uwezo wa kufungua docket, upelelezi, arresting power, na kumpandisha policeman mahakamani, ni lazima tuwe na FBI
 
Haya ndio mapungufu ya kisheria, kwani murder case ina tofauti gani?,huyu mtoto bado ni suspect sio mhalifu, nikipewa urais wa 24hrs makosa yote ya kijinai yatakua na bail, suspect lazima apelekwe kwa court of law within 48hrs, kama police hawawezi ili lazima mahakama itoe kibali cha kumzuia suspect for another 48hrs, no arrest until upelelezi umekamilika
Murder case ina tofauti gani are you serious?? Usinikumbushe Jeff Dahmer.

If the suspect pauses risks ya kuumiza wengine bora abaki huko huko. Yale mauaji ya watu 17 wa ukoo mmoja huko Musoma mwaka 2010, washtakiwa ungewaachia? Tena walidhamiria kuua ukoo wote kupoteza ushaidi, akaponea chupuchupu aliyejificha chini ya kitanda...

BTW usigombee urais pls.
 
Hili nalo ni tatizo ndio maana tunahitaji katiba mpya,itatupatia IPID, hawa ni kama MPs wa jeshi, watakua na uwezo wa kufungua docket, upelelezi, arresting power, na kumpandisha policeman mahakamani, ni lazima tuwe na FBI
Polisi akikutendea UOVU halafu ukamshtaki kwny mamlaka za polisi au za mahakama ni km vile umejiongezea wasiwasi wa kuishi.

Nchi Gani hii.
 
Back
Top Bottom