Mtoto afukuzwa shule kwa kumuuliza mwalimu 'dagaa anaitwaje kwa kiingereza'

Tunamhukumu mwalimu wa watu bureee...haya wataalam wa lugha, dagaa kwa kidhungu? twasubiri, tusije ulizwa na wanetu halafu majibu yakawa kama hayo ya mwalimu!

Mwalimu kafukuza mwanafunzi shule, sasa head wa house nikishindwa kujibu "what is dagaa" sijui inabidi mtoto nimhamishie kwa shangazi yake akafunzwe maadili??

Jamani wenye lugha tusaidieni fasta maana mambo haya yanataka wito!
 
Huyu mwalim hana mbinu za kujibu maswali, na inaonyesha kama hana jibu la swali aliloulizwa ana panic haraka badala ya kutafuta solution, kama Laurence alivyosema hapo juu, angetakiwa amrudishie yeye mwenyewe swali hilo au angemuambia nakupa home work kesho saa 4 nipatie jibu, au kumbe wewe unapenda dagaa ee!! kwani kuna dagaa wa aina ngapi? akishindwa unampa home work unamuambia unapaswa ujue aina za dagaa kwanza kwa hiyo nenda kesho uniletee aina za dagaa halafu nitakuambia dagaa wanaitwaje kwa kiingereza. Hapo hawezi kugundua kwamba hujui na kesho utampa jibu sahihi

mkuu ww ni mwalimu nn?!
 
tichaaaaaa wewe ni mnoma yaani unamchapa mwanafunzi na kumfukuza shule kisa kaukliza dagaa kwa kingereza anaitwaje? je angeulizia samaki anaitwaje si ndio ungemtanguliza mbele za haki kabisa!!!! eenh ama kweli kiingereza kilikuja na MELI!
 
Natamani ningekuwa mzazi wa huyu mtoto! hakika na mimi ningehakikisha namcharaza viboko huyu ticheli! dah!
 
Najaribu kufikiri namna huyo Mwalimu alivyokuwa akiongea kwa ki-english.
Wee pupils you know me? I will beat you and go speak to your father. You play play with me, I am another. Mmmhh"

ooooh dia my mbavu ohoohohohohohho. uuuuwii you pipo yuu jamani their faza cant wash young coconut (hawafui dafu) kwa mwalimu hata wakienda kwa serikali za mitaa. loooh hali ni tete.
 
Mwanafunzi wa shule ya msingi Kakuyu amefukuzwa shule kwa kumuuliza mwalimu wake wa Kiingereza ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo kuwa dagaa kwa Kiingereza anaitwaje?

Mwalimu huyo aliposhindwa kujibu swali hilo alihamaki, akamcharaza mtoto huyo bakora sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake na akahitimisha kwa kumwandikia barua ya kumfukuza shule kwa madai ya utovu wa nidhamu na kutumiwa kama kibaraka wa maadui wa mwalimu huyo.

My Take:
jamani elimu yetu Tanzania ni wapi inakoelekea?
Je tuna walimu ama tuna maamuma?

Tumpe pole sana huyo mwanafunzi...inaonyesha yuko mdadisi sana, na hawa ndo vijana tunaowataka.
ngoja nimpe jibu...dagaa wanaitwa sardines or seafood.
 
mkuu ww ni mwalimu nn?!
Hapana mkuu, ila nimewahi kufundisha sana sunday school kanisani, watoto wana maswali hadi unaweza kuchanganyikiwa, kuna siku waliniuliza "mwalim, hapo zamani kulikuwa na utupu wakati Mungu anaumba dunia, ina maana kulikuwa hakuna kitu chochote duniani, sasa huyu Mungu wakati anaumba hiyo dunia alikaa wapi?
 
<br />
<br />

small fish

lol si kweli... hapo wanakamusi wame generize moja kwa moja ukicheki kwenye kamusi jina la kwanza wameweka small fish ! hehehe ... dagaa anaitwa sardines kwa kitaalamu na ndio jina linavyotumika
 
Mitoto haona adabu inapaswa kucharazwa bakora za kutosha, linadhani muhimu sana kujua jina la kiinglish la dagaa kuliko kujisomea, pilipili mbuzi mkubwa
 
Huyu mwalim hana mbinu za kujibu maswali, na inaonyesha kama hana jibu la swali aliloulizwa ana panic haraka badala ya kutafuta solution, kama Laurence alivyosema hapo juu, angetakiwa amrudishie yeye mwenyewe swali hilo au angemuambia nakupa home work kesho saa 4 nipatie jibu, au kumbe wewe unapenda dagaa ee!! kwani kuna dagaa wa aina ngapi? akishindwa unampa home work unamuambia unapaswa ujue aina za dagaa kwanza kwa hiyo nenda kesho uniletee aina za dagaa halafu nitakuambia dagaa wanaitwaje kwa kiingereza. Hapo hawezi kugundua kwamba hujui na kesho utampa jibu sahihi
<br />
<br />
Hizo ndizo mbinu mkuu kama mwl unahisi swali haulijui
 
Hebu niambieni wakuu,
Hata mimi sijui dagaa kwa kungereza anaitwaje!!

Anaitwa SARDINE....

Sasa huyu mwalimi kweli ana haki na uhalali wa kuitwa mwalimu (achia mbali uwaalimu mkuu)???? Halafu tunasema watoto wetu ni WAJINGA; HAWANA VIPAJI nk. Kipaji hata kama mtoto anacho; kitakuzwa vipi chini ya uangalizi wa Mwalimu KIAZI KAMA HUYU????? MUNGU SAIDIA WANAFUNZI WATANZANIA!!!!
 
Nyerere tumlaumu kwenye hili. How come me English speaking don't??
 
Back
Top Bottom